Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
107.Surat Al-Maau'n

Imeshuka Makka Ina aya 7
Utangulizi Sura Nyingine Faharasa


KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0



1. Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo? 1



2. Huyo ndiye anaye msukuma yatima, 2



3. Wala hahimizi kumlisha masikini. 3



4. Basi, ole wao wanao sali, 4



5. Ambao wanapuuza Sala zao; 5



6. Ambao wanajionyesha, 6



7. Nao huku wanazuia msaada. 7


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani