2.Surat Ta'ha |
Imeshuka Madina | Ina aya 135 |
Utangulizi | Orodha ya Sura | Faharasa |
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0
1. T'AHA!
1
2. Hatukukuteremshia Qur'ani ili upate mashaka.
2
3. Bali ni mawaidha kwa wenye kunyenyekea.3
4. Materemsho yatokayo kwa aliye umba ardhi na
mbingu zilizo juu.
4
5. Arrahmani, Mwingi wa Rehema, aliye tawala juu
ya Kiti cha Enzi.
5
6. Ni vyake vyote viliomo mbinguni na viliomo
katika ardhi, na viliomo baina yao, na viliomo chini ya ardhi.
6
7. Na ukinyanyua sauti kwa kusema...basi hakika
Yeye anajua siri na duni kuliko siri.
7
8. Mwenyezi Mungu! Hapana mungu isipo kuwa Yeye.
Yeye ana majina mazuri kabisa.
8
9. Na je! Imekufikia hadithi ya Musa?
9
10. Alipo uona moto, akawaambia watu wake: Ngojeni!
Mimi nimeuona moto, huenda nikakuleteeni kijinga kutoka huo moto, au nikapata
uongofu kwenye moto.
10
11. Basi alipo ufikia akaitwa: Ewe Musa!
11
12. Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua
viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la T'uwa.
12
13. Nami nimekuteua wewe; basi sikiliza unayo
funuliwa.
13
14. Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana
mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Sala kwa ajili ya kunikumbuka
Mimi.
14
15. Hakika Saa itakuja bila ya shaka. Nimekaribia
kuificha, ili kila nafsi ilipwe kwa iliyo yafanya.
15
16. Kwa hivyo asikukengeushe nayo yule ambaye
haiamini na akafuata pumbao lake ukaja kuhiliki.
16
17. Na nini hicho kilichomo mkononi mwako wa
kulia, ewe Musa?
17
18. Akasema: Hii ni fimbo yangu; naiegemea na
ninawaangushia majani kondoo na mbuzi wangu. Tena inanifaa kwa matumizi
mengine.
18
19. Au ni kama mvua kubwa itokayo mbinguni, ina
giza na radi na umeme; wakawa wakitia vidole vyao masikioni mwao kwa ajili
ya mingurumo, kwa kuogopa kufa. Na Mwenyezi Mungu amewazunguka makafiri.
19
20. Akaitupa. Mara ikawa nyoka anaye kwenda mbio.
20
21. Akasema: Ikamate, wala usiogope! Tutairudisha
hali yake ya kwanza.
21
22. Na uambatishe mkono wako kwenye ubavu. Utatoka
mweupe pasipo kuwa na madhara yoyote. Hiyo ni ishara nyengine.
22
23. Ili tukuonyeshe baadhi ya ishara zetu kubwa.
23
24. Nenda kwa Firauni; kwani hakika yeye amepindukia
mipaka.
24
25. (Musa) akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie
kifua changu,
25
26. Na unifanyie nyepesi kazi yangu,
26
27. Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu,
27
28. Wapate kufahamu maneno yangu.
28
29. Na nipe waziri katika watu wangu,
29
30. Harun, ndugu yangu.
30
31. Kwake yeye niongeze nguvu zangu.
31
32. Na umshirikishe katika kazi yangu.
32
33. Ili tukutakase sana.
33
34. Na tukukumbuke sana.
34
35. Hakika Wewe unatuona.
35
36. Akasema: Hakika Umepewa maombi yako, ewe
Musa!
36
37. Na hakika tulikwisha kufanyia hisani mara
nyengine...
37
38. Pale tulipo mfunulia mama yako yaliyo funuliwa,
38
39. Ya kuwa mtie katika kisanduku, na kisha kitie
mtoni, na mto utamfikisha ufukweni. Atamchukua adui yangu naye ni adui
yake. Na nimekutilia mapenzi yanayo tokana kwangu, na ili ulelewe machoni
mwangu.
39
40. Dada yako alipo kwenda na akasema: Je! Nikujuulisheni
mtu wa kuweza kumlea? Basi tukakurejesha kwa mama yako ili macho yake yaburudike,
wala asihuzunike. Na ulimuuwa mtu, nasi tukakuokoa katika dhiki, na tukakujaribu
kwa majaribio mengi. Ukakaa miaka kwa watu wa Madyana. Kisha ukaja kama
ilivyo kadiriwa, ewe Musa!
40
41. Na nimekuteuwa kwa ajili ya nafsi yangu.
41
42. Nenda, wewe na ndugu yako, pamoja na ishara
zangu, wala msichoke kunikumbuka.
42
43. Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia
mipaka.
43
44. Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia
au akaogopa.
44
45. Wakasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika sisi
tunaogopa asije akapindukia mipaka juu yetu au kufanya jeuri.
45
46. Akasema: Msiogope! Hakika Mimi ni pamoja
nanyi. Nasikia na ninaona.
46
47. Basi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi
ni Mitume wa Mola wako Mlezi! Basi waache Wana wa Israili watoke nasi,
wala usiwaadhibu. Sisi tumekuletea ishara itokayo kwa Mola wako Mlezi.
Na amani itakuwa juu ya aliye fuata uwongofu.
47
48. Hakika tumefunuliwa sisi kwamba hapana shaka
adhabu itamsibu anaye kadhibisha na akapuuza.
48
49. (Firauni) akasema: Basi Mola wenu Mlezi ni
nani, ewe Musa?
49
50. Akasema: Mola wetu Mlezi ni yule aliye kipa
kila kitu umbo lake, kisha akakiongoa.
50
51. Akasema: Nini hali ya karne za kwanza?
51
52. Akasema: Ilimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi
katika Kitabu. Mola wangu Mlezi hapotei wala hasahau.
52
53. Na tulipo mpa Musa Kitabu na pambanuo ili
mpate kuongoka.
53
54. Kuleni, na mchunge wanyama wenu. Hakika katika
hayo zipo ishara kwa wenye akili.
54
55. Na mlipo sema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka
tumwone Mwenyezi Mungu waziwazi. Ikakunyakueni radi nanyi mnaangalia.
55
56. Na hakika tulimwonyesha ishara zetu zote.
Lakini alikadhibisha na akakataa.
56
57. Akasema: Ewe Musa! Hivyo umetujia kututoa
katika nchi yetu kwa uchawi wako?
57
58. Basi sisi hakika tutakueletea uchawi kama
huo. Basi weka miadi baina yetu na wewe, ambayo tusiivunje sisi wala wewe,
mahali patapo kuwa sawa.
58
59. Akasema: Miadi yenu ni siku ya Sikukuu; na
watu wakusanywe kabla ya adhuhuri.
59
60. Basi Firauni akarudi na akatengeneza hila
yake, kisha akaja.
60
61. Musa akamwambia: Ole wenu! Msimzulie Mwenyezi
Mungu uwongo, asije akakufutilieni mbali kwa adhabu. Na mwenye kuzua lazima
ashindwe!
61
62. Basi wakazozana kwa shauri yao wenyewe kwa
wenyewe, na wakanong'ona kwa siri.
62
63. Wakasema: Hakika hawa wawili ni wachawi,
wanataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wao, na waondoe mila zenu
zilizo bora kabisa.
63
64. Kwa hivyo kusanyeni hila zenu zote, kisha
mfike kwa kujipanga safu, na kwa yakini atafuzu kweli kweli leo atakaye
shinda.
64
65. Wakasema: Ewe Musa! Je! Utatupa wewe, au
tutakuwa sisi wa kwanza kutupa?
65
66. Akasema: Bali tupeni nyinyi! Tahamaki kamba
zao na fimbo zao zikaonekana mbele yake, kwa uchawi wao, kuwa zinapiga
mbio.
66
67. Basi Musa akaingia khofu nafsi yake.
67
68. Tukasema: Usikhofu! Hakika wewe ndiye utakaye
shinda.
68
69. Na kitupe kilicho katika mkono wako wa kulia;
kitavimeza walivyo viunda. Hakika walivyo unda ni hila za mchawi tu, na
mchawi hafanikiwi popote afikapo.
69
70. Basi wachawi wakaangushwa wanasujudu. Wakasema:
Tumemuamini Mola Mlezi wa Harun na Musa!
70
71. (Firauni) akasema: Oh! Mnamuamini kabla sijakupeni
ruhusa? Hakika yeye ndiye mkubwa wenu aliye kufundisheni uchawi. Basi kwa
yakini nitakukateni mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakutundikeni
misalabani katika vigogo vya mitende, na hapo kwa yakini mtajua ni nani
katika sisi aliye mkali wa kuadhibu na kuiendeleza adhabu yake.
71
72. Wakasema: Hatutokukhiari wewe kuliko ishara
waziwazi zilizo tujia, na kuliko yule aliye tuumba. Basi hukumu utavyo
hukumu; kwani wewe unahukumu haya ya maisha ya duniani tu.
72
73. Hakika sisi tumemuamini Mola wetu Mlezi ili
atusamehe makosa yetu na uchawi ulio tulazimisha kuufanya. Na Mwenyezi
Mungu ndiye Mbora na Mwenye kudumu zaidi.
73
74. Hakika ataye mjia Mola wake Mlezi naye ni
mkhalifu, basi kwa yakini, yake huyo ni Jahannamu. Hafi humo wala haishi.
74
75. Na atakaye mjia naye ni Muumini aliye tenda
mema, basi hao ndio wenye vyeo vya juu.
75
76. Bustani za milele zipitazo mito kati yake,
wadumu humo. Na hayo ni malipo ya mwenye kujitakasa.
76
77. Na tulimfunulia Musa: Toka usiku na waja
wangu, na uwapigie njia kavu baharini. Usikhofu kukamatwa, wala usiogope.
77
78. Firauni akawafuata pamoja na majeshi yake.
Basi kiliwafudikiza humo baharini kilicho wafudikiza.
78
79. Na Firauni aliwapoteza watu wake wala hakuwaongoa.
79
80. Enyi Wana wa Israili! Hakika tulikuokoeni
na adui yenu, na tukakuahidini upande wa kulia wa mlima. Na tulikuteremshieni
Manna na Salwa.
80
81. Kuleni katika vitu vizuri hivyo tulivyo kuruzukuni,
wala msiruke mipaka katika hayo, isije ikakushukieni ghadhabu yangu. Na
inaye mshukia ghadhabu yangu basi huyo ameangamia.
81
82. Na hakika Mimi ni Mwingi wa Kusamehe kwa
anaye tubia, na akaamini, na akatenda mema, tena akaongoka.
82
83. Na nini kilicho kutia haraka ukawaacha watu
wako, ewe Musa?
83
84. Akasema: Hao wapo nyuma yangu wananifuatia.
Na nimefanya haraka kukujia, Mola wangu Mlezi, ili uridhike.
84
85. (Mwenyezi Mungu) akasema: Sisi tumewatia
mtihani watu wako baada yako, na Msamaria amewapoteza.
85
86. Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na
kusikitika. Akasema: Enyi watu wangu! Kwani Mola wenu Mlezi hakukuahidini
ahadi nzuri? Je, umekuwa muda mrefu kwenu au mmetaka ikushukieni ghadhabu
ya Mola wenu Mlezi, ndio maana mkavunja miadi yangu?
86
87. Wakasema: Sisi hatukuvunja miadi yako kwa
khiari yetu, lakini tulibebeshwa mizigo ya mapambo ya watu, basi tukaitupa.
Na hivyo ndivyo alivyo toa shauri Msamaria.
87
88. Na akawaundia ndama, kiwiliwili chenye sauti.
Na wakasema: Huyu ndiye mungu wenu, na mungu wa Musa, lakini alisahau.
88
89. Je! Hawakuona kuwa hakuwarudishia neno, wala
hakuweza kuwadhuru wala kuwafaa?
89
90. Na hakika Harun alikwisha waambia kabla yake:
Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmetiwa mtihanini tu kwa kitu hiki. Na kwa
yakini Mola wenu Mlezi ni Arrahmani, Mwingi wa Rehema. Basi nifuateni mimi,
na t'iini amri yangu!
90
91. Wakasema: Hatutaacha kumuabudu mpaka Musa
atapo rejea kwetu.
91
92. (Musa) akasema: Ewe Harun! Ni nini kilicho
kuzuia, ulipo waona wamepotea,
92
93. Hata usinifuate? Je, umeasi amri yangu?
93
94. Akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike
ndevu zangu, wala kichwa changu. Kwa hakika naliogopa usije sema: Umewafarikisha
Wana wa Israil, na hukungojea kauli yangu.
94
95. (Musa) akasema: Ewe Msamaria! Unataka nini
?
95
96. Akasema: Niliona wasiyo yaona wao, nikashika
gao katika unyao wa Mtume. Kisha nikalitupa. Na hivi ndivyo ilivyo nielekeza
nafsi yangu.
96
97. (Musa) akasema: Basi ondoka! Na kwa yakini
utakuwa katika maisha ukisema: Usiniguse. Na hakika una ahadi kwako isiyo
vunjwa. Na mtazame huyo mungu wako uliye endelea kumuabudu - Sisi kwa hakika
tutamchoma moto, kisha tutamtawanya baharini atawanyike.
97
98. Hakika Mungu wenu ni Allah, Mwenyezi Mungu,
tu. Hapana Mungu isipo kuwa Yeye. Ujuzi wake umeenea kila kitu.
98
99. Namna hivi tunakuhadithia katika khabari
za yaliyo tangulia. Na hakika tumekuletea kutoka kwetu mawaidha ya kukumbukwa.
99
100. Atakaye jitenga nayo, basi kwa yakini Siku
ya Kiyama atabeba mzigo.
100
101. 101. Wadumu humo. Na ni mzigo muovu kwao kuubeba
Siku ya Kiyama!
101
102. Siku litakapo pulizwa barugumu, na tukawakusanya
wakhalifu Siku hiyo, hali macho yao ya kibuluu.
102
103. Watanong'onezana wao kwa wao: Hamkukaa
ila siku kumi tu.
103
104. Sisi tunajua zaidi watakayo yasema, atakapo
sema mbora wao katika mwendo: Nyinyi hamkukaa ila siku moja tu.
104
105. Na wanakuuliza khabari za milima. Waambie:
Mola wangu Mlezi ataivuruga vuruga.
105
106. Na ataiacha tambarare, uwanda.
106
107. Hutaona humo mdidimio wala muinuko.
107
108. Siku hiyo watamfuata muitaji asiye na upotofu.
Na sauti zote zitamnyenyekea Arrahmani Mwingi wa Rahema. Basi husikii ila
mchakato na mnong'ono.
108
109. Siku hiyo uombezi haufai kitu, ila wa aliye
mruhusu Arrahmani Mwingi wa Rehema na akamridhia kusema.
109
110. Yeye anajua yaliyo mbele yao, na yaliyo
nyuma yao. Wala wao hawawezi kumjua Yeye vilivyo.
110
111. Na zitadhalilika nyuso mbele ya Aliye Hai
Milele, Mwangalizi Mkuu. Na atakuwa ameharibikiwa mwenye kubeba dhulma.
111
112. Na anaye tenda mema, naye ni Muumini, basi
hatakhofu kudhulumiwa wala kupunjwa.
112
113. Na namna hivi tumeiteremsha Qur'ani kwa
Kiarabu, na tumekariri humo maonyo ili wapate kuogopa na kujilinda na iwaletee
makumbusho.
113
114. Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki.
Wala usiifanyie haraka hii Qur'ani, kabla haujamalizika ufunuo wake. Na
sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu.
114
115. Na hapo zamani tuliagana na Adam, lakini
alisahau, wala hatukuona kwake azma kubwa.
115
116. Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam!
Wakasujudu, isipo kuwa Iblisi, alikataa.
116
117. Tukasema: Ewe Adam! Hakika huyu ni adui
yako na wa mkeo. Basi asikutoeni katika Bustani hii, mkaingia mashakani.
117
118. Hakika humo hutakuwa na njaa wala hutakuwa
uchi.
118
119. Na hakika hutapata kiu humo wala hutapata
joto.
119
120. Lakini Shet'ani alimtia wasiwasi, akamwambia:
Ewe Adam! Nikujuulishe mti wa kuishi milele na ufalme usio koma?
120
121. Basi wakaula wote wawili, na uchi wao ukawadhihirikia
na wakaanza kujibandika majani ya Bustani. Na Adam akamuasi Mola wake Mlezi,
na akapotea njia.
121
122. Kisha Mola wake Mlezi akamteuwa, naye akamkubalia
toba yake, naye akamwongoa.
122
123. Akasema: Ondokeni humu nyote, hali ya kuwa
ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi
atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.
123
124. Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu,
basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua
hali ya kuwa kipofu.
124
125. Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua
kipofu, nami nilikuwa nikiona?
125
126. (Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo
hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa.
126
127. Na hivi ndivyo tutakavyo mlipa kila apitaye
kiasi, na asiye amini ishara za Mola wake Mlezi. Na hakika adhabu ya Akhera
ni kali zaidi, na inadumu zaidi.
127
128. Je! Haikuwabainikia tu; vizazi vingapi
tuliviangamiza kabla yao, nao wanatembea katika maskani zao? Hakika katika
hayo zimo ishara kwa wenye akili.
128
129. Na lau kuwa si neno lililo kwisha tangulia
kutoka kwa Mola wako Mlezi na muda ulio wekwa, bila ya shaka inge fika
adhabu (hapa hapa).
129
130. Yavumilie haya wayasemayo. Na umtakase
Mola wako Mlezi kwa kumsifu kabla ya kuchomoza jua, na kabla halijachwa,
na nyakati za usiku pia umtakase, na ncha za mchana ili upate ya kukuridhisha.
130
131. Wala usivikodolee macho tulivyo wastareheshea
baadhi ya watu miongoni mwao, kwa ajili ya mapambo ya duniani, ili tuwajaribu.
Na riziki ya Mola wako Mlezi ni bora na inadumu zaidi.
131
132. Na waamrishe watu wako kusali, na uendelee
mwenyewe kwa hayo. Sisi hatukuombi wewe riziki, bali Sisi ndio tunakuruzuku.
Na mwisho mwema ni kwa mchamngu.
132
133. Na walisema: Kwa nini hakutuletea muujiza
kutoka kwa Mola wake Mlezi? Je! Haikuwafikilia dalili wazi ya yaliyomo
katika Vitabu vya kale?
133
134. Na lau kuwa tuliwaangamiza kwa adhabu kabla
yake, wangeli sema: Ewe Mola wetu Mlezi! Kwa nini usituletee Mtume tukazifuata
ishara zako kabla hatujadhilika na kuhizika.
134
135. Sema: Kila mmoja anangoja. Basi ngojeni!
Hivi karibuni mtajua nani mwenye njia sawa na nani aliye ongoka.
135
Sura Nyingine | Faharasa |