21.Suuratul Anbiyaa |
Imeshuka Makka | Ina aya 112 |
Utangulizi | Orodha ya Sura | Faharasa |
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0
1. IMEWAKARIBIA watu hisabu yao, nao wamo katika mghafala wanapuuza.
1
2. Hayawafikilii mawaidha mapya kutoka kwa Mola wao Mlezi ila huyasikiliza
na huku wanafanya mchezo.
2
3. Zimeghafilika nyoyo zao. Na wale walio dhulumu hunong'onezana
kwa siri: Ni nani ati huyu isipo kuwa ni binaadamu tu kama nyinyi! Mnauwendea
uchawi hali nanyi mnaona?
3
4. Alisema: Mola wangu Mlezi anayajua yasemwayo mbinguni na katika
ardhi. Na Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.
4
5. Lakini wao walisema: Hizo ni ndoto za ovyo ovyo, bali amezizua
tu, bali huyo ni mtunga mashairi. Basi atuletee miujiza kama walivyo tumwa
wale wa mwanzo.
5
6. Hawakuamini kabla yao watu wa mji tulio uangamiza. Basi, je, wataamini
hawa?
6
7. Na kabla yako hatukuwatuma ila watu wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo).
Basi waulizeni wenye ilimu ikiwa nyinyi hamjui.
7
8. Wala hatukuwafanya miili isiyo kula chakula, wala hawakuwa wenye
kuishi milele.
8
9. Kisha tukawatimizia miadi, na tukawaokoa wao na tulio wataka,
na tukawateketeza walio pita mipaka.
9
10. Na hakika tumekuteremshieni Kitabu ambacho ndani yake yamo makumbusho
yenu. Je! Hamzingatii?
10
11. Na mingapi katika miji iliyo kuwa ikidhulumu tumeiteketeza, na
tukawasimamisha baada yao watu wengine.
11
12. Basi walipo ihisi adhabu yetu, mara wakaanza kukimbia.
12
13. Msikimbie! Na rejeeni kwenye zile zile starehe zenu, na maskani
zenu, mpate kusailiwa!
13
14. Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa madhaalimu.
14
15. Hakikuacha hicho kuwa kilio chao mpaka tukawafanya kama walio
fyekwa, wamezimika.
15
16. Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yao kwa mchezo.
16
17. Kama tungeli taka kufanya mchezo tunge jifanyia Sisi wenyewe,
lau kwamba tungeli kuwa ni wafanyao mchezo.
17
18. Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja na mara ukatoweka.
Na ole wenu kwa mnayo yazua.
18
19. Na ni vyake Yeye tu Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na katika
ardhi. Na walioko kwake hawafanyi kiburi wakaacha kumuabudu, wala hawachoki.
19
20. Wanamtakasa usiku na mchana, wala hawanyong'onyei.
20
21. Au wamepata miungu katika ardhi inayo fufua?
21
22. Lau wangeli kuwamo humo miungu wengine isipo kuwa Mwenyezi Mungu
basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingeli fisidika. Subahana 'Llah
Ametakasika Mwenyezi Mungu, Bwana wa A'rshi (Kiti cha Enzi), na hayo wanayo
yazua.
22
23. Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanao hojiwa kwa wayatendayo.
23
24. Au wanawaabudu miungu mingine badala yake? Sema: Leteni ushahidi
wenu! Haya ni ukumbusho wa hawa walio nami, na ukumbusho wa walio kabla
yangu. Lakini wengi wao hawaijui kweli, na kwa hivyo wanapuuza.
24
25. Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba
hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu.
25
26. Na wanasema: Arrahman, Mwingi wa Rehema, ana mwana! Subhanahu,
Ametakasika na hayo! Bali hao (wanao waita wana) ni watumwa walio tukuzwa.
26
27. Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri zake.
27
28. Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawamwombei
yeyote ila yule anaye mridhia Yeye, nao kwa ajili ya kumwogopa wananyenyekea.
28
29. Na yeyote kati yao atakaye sema: Mimi ni mungu, badala yake,
basi huyo tutamlipa malipo yake Jahannamu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo wenye
kudhulumu.
29
30. Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa
zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho
hai? Basi je, hawaamini?
30
31. Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thibiti ili isiwayumbishe,
na tukaweka humo njia pana ili wapate kuongoka.
31
32. Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyo hifadhiwa, lakini wanazipuuza
Ishara zake.
32
33. Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote
katika anga vinaogelea.
33
34. Nasi hatukumjaalia mwanaadamu yeyote kabla yako kuwa na maisha
ya milele. Basi je! Ukifa wewe, wao wataishi milele?
34
35. Kila nafsi itaonja mauti; na tunakujaribuni kwa mtihani wa shari
na kheri. Na kwetu Sisi mtarejeshwa.
35
36. Na wakikuona walio kufuru hawakufanyi wewe ila ni kitu cha maskhara
tu, (wakisema): Je! Ndiye huyu anaye itaja miungu yenu? Na hali wao wanakataa
kumkumbuka Arrahman, Mwingi wa Rehema!
36
37. Mwanaadamu ameumbwa na haraka. Nitakuonyesheni Ishara zangu.
Basi msinihimize.
37
38. Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?
38
39. Lau wangeli jua wale walio kufuru wakati ambao hawatauzuia Moto
kwenye nyuso zao wala migongo yao, na wala hawatanusuriwa!
39
40. Bali utawafikia kwa ghafla, na utawashitua na wala hawataweza
kuurudisha, wala hawatapewa muhula!
40
41. Na Mitume walio kabla yako walikwisha dhihakiwa. Kwa hivyo wale
walio wafanyia maskhara yaliwafika yale waliyo kuwa wakiyafanyia dhihaka.
41
42. Sema: Nani anaye kulindeni usiku na mchana na Arrahmani Mwingi
wa Rehema? Bali wao wanapuuza kumkumbuka Mola wao Mlezi.
42
43. Au wao wanao miungu watao weza kuwakinga nasi? Hao hawawezi kujinusuru
nafsi zao, wala hawatalindwa nasi!
43
44. Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu
kwao. Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza ncha zake?
Basi je! Hao ni wenye kushinda?
44
45. Sema: Mimi nakuonyeni kwa Wahyi. Na viziwi hawasikii wito wanapo
onywa.
45
46. Na wanapo guswa na mpulizo mmoja tu wa adhabu itokayo kwa Mola
wako Mlezi, bila ya shaka wao husema: Ole wetu! Hakika tulikuwa wenye kudhulumu.
46
47. Nasi tutaweka mizani za uadilifu kwa Siku ya Kiyama. Basi nafsi
haitadhulumiwa kitu chochote. Hata ikiwa ni uzito wa chembe ya khardali
tutaileta. Nasi tunatosha kuwa washika hisabu.
47
48. Na kwa yakini tuliwapa Musa na Haaruni kipambanuzi, na mwangaza,
na makumbusho kwa wachamngu,
48
49. Ambao wanamkhofu Mola wao Mlezi faraghani, na wanaiogopa Saa
ya Kiyama.
49
50. Na haya ni makumbusho yaliyo barikiwa, tuliyo yateremsha. Basi
je! Mnayakataa?
50
51. Na hakika tulikwisha mpa Ibrahim uwongofu wake zamani, na tulikuwa
tunamjua.
51
52. Alipo mwambia baba yake na watu wake: Ni nini haya masanamu mnayo
yashughulikia kuyaabudu?
52
53. Wakasema: Tumewakuta baba zetu wakiyaabudu.
53
54. kasema: Bila ya shaka nyinyi na baba zenu mmekuwa katika upotofu
ulio dhaahiri.
54
55. Wakasema: Je! Umetujia kwa maneno ya kweli au wewe ni katika
wachezao tu?
55
56. Akasema: Bali Mola wenu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi
ambaye ndiye aliye ziumba. Na mimi ni katika wenye kuyashuhudia hayo.
56
57. Na Wallahi! Nitayafanyia vitimbi masanamu yenu haya baada ya
mkisha geuka kwenda zenu.
57
58. Basi akayavunja vipande vipande, ila kubwa lao, ili wao walirudie.
58
59. Wakasema: Nani aliye ifanyia haya miungu yetu? Hakika huyu ni
katika walio dhulumu.
59
60. Wakasema: Tumemsikia kijana mmoja akiwataja. Anaitwa Ibrahim.
60
61. Wakasema: Je! Wewe umeifanyia haya miungu yetu, ewe Ibrahim?
61
62. Wakasema: Je! Wewe umeifanyia haya miungu yetu, ewe Ibrahim?
62
63. Akasema: Bali amefanya hayo huyu mkubwa wao. Basi waulizeni ikiwa
wanaweza kutamka.
63
64. Basi wakajirudi nafsi zao, wakasema: Hakika nyinyi mlikuwa madhaalimu!
64
65. Kisha wakarejea kwenye ule ule upotovu wao wakasema: Wewe unajua
kwamba hawa hawesemi.
65
66. Akasema: Basi nyinyi mnawaabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu wasio
kufaini kitu wala kukudhuruni?
66
67. Aibu yenu nyinyi na hivyo mnavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu!
Basi nyinyi hamtii akilini?
67
68. Wakasema: Mchomeni moto, na muinusuru miungu yenu, ikiwa nyinyi
ni watendao jambo!
68
69. Sisi tukasema: Ewe moto! Kuwa baridi na salama kwa Ibrahim!
69
70. Wao walimkusudia maovu, lakini Sisi tukawafanya wao ndio walio
khasiri.
70
71. Na tukamwokoa yeye na Luut'i tukawapeleka kwenye nchi tulio ibariki
kwa ajili ya walimwengu wote.
71
72. Naye tukampa Is-haq, na Yaaqub kuwa ni ziada. Na wote tukawajaalia
wawe watu wema.
72
73. Na tukawafanya maimamu wakiongoa watu kwa amri yetu. Na tukawafunulia
watende kheri, na washike Sala, na watoe Zaka; na walikuwa wanatuabudu
Sisi tu.
73
74. Na Luut'i tukampa hukumu na ilimu na tukamwokoa na ule mji ulio
kuwa ukifanya maovu. Hakika hao walikuwa watu wabaya, wachafu.
74
75. Na tukamuingiza katika rehema yetu. Hakika yeye ni miongoni mwa
watenda mema.
75
76. Na Nuhu alipo ita zamani, nasi tukamuitikia, na tukamwokoa yeye
na watu wake kutokana na shida kubwa.
76
77. Na tukamnusuru na watu walio zikanusha Ishara zetu. Hakika hao
walikuwa watu wabaya. Basi tukawazamisha wote.
77
78. Na Daud na Suleiman walipo kata hukumu katika kadhiya ya konde
walipo lisha humo mbuzi wa watu usiku. Na Sisi tulikuwa wenye kushuhudia
hukumu yao hiyo.
78
79. Tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na
ilimu. Na tuliifanya milima na ndege kuwa pamoja na Daud imnyenyekee na
imtakase Mwenyezi Mungu. Na Sisi ndio tulio fanya hayo.
79
80. Na tukamfundisha kuunda mavazi ya vita kwa ajili yenu ili yakuhifadhini
katika kupigana kwenu. Je! Mtakuwa wenye kushukuru?
80
81. Na tukamsahilishia Suleiman upepo wa kimbunga wendao kwa amri
yake kwenye ardhi tuliyo ibarikia. Na Sisi ndio tunao jua kila kitu.
81
82. Na pia mashet'ani wanao mpigia mbizi na kufanya kazi nyenginezo.
Na Sisi tulikuwa walinzi wao.
82
83. Na Ayyubu, alipo mwita Mola wake Mlezi, akasema: Mimi yamenipata
madhara. Na Wewe ndiye unaye rehemu kuliko wote wanao rehemu.
83
84. Basi tukamwitikia, na tukamwondolea madhara aliyo kuwa nayo,
na tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao kuwa ni rehema inayo toka
kwetu, na ukumbusho kwa wafanyao ibada.
84
85. Na Ismail, na Idris, na Dhulkifli - wote walikuwa miongoni mwa
wanao subiri.
85
86. Na tukawaingiza katika rehema yetu. Hakika wao walikuwa katika
watu wema.
86
87. Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhibika, na akadhani ya kwamba
hatutakuwa na uwezo juu yake. Basi aliita katika giza: Hapana mungu isipo
kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye
kudhulumu.
87
88. Basi tukamwitikia na tukamwokoa kutokana na dhiki. Na hivyo ndivyo
tunavyo waokoa Waumini.
88
89. Na Zakariya alipo mwita Mola wake Mlezi: Mola wangu Mlezi! Usiniache
peke yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanao rithi.
89
90. Na mwanamke aliye linda uke wake, na tukampulizia katika roho
yetu, na tukamfanya yeye na mwanawe kuwa ni Ishara kwa walimwengu.
90
91. Na mwanamke aliye linda uke wake, na tukampulizia katika roho
yetu, na tukamfanya yeye na mwanawe kuwa ni Ishara kwa walimwengu.
91
92. Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu
Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.
92
93. Nao wakalikata jambo lao hili mapande mapande baina yao. Wote
watarudi kwetu.
93
94. Na atendaye mema naye ni Muumini basi haitakataliwa juhudi yake.
Na hakika Sisi tunamwandikia.
94
95. Na haiwi kwa wana-mji tulio uangamiza, ya kwamba hawatarejea,
95
96. Mpaka watapo funguliwa Juju na Maajuju wakawa wanateremka kutoka
kila mlima;
96
97. Na miadi ya haki ikakaribia. Hapo ndipo yatapo kodoka macho ya
walio kufuru (na watasema:) Ole wetu! Bila ya shaka tulikuwa tumeghafilika
na haya, bali tulikuwa wenye kudhulumu.
97
98. Hakika nyinyi na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni
kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu.
98
9. Lau kuwa hawa ni miungu, wasingeli ingia. Na wote watadumu humo.
99
100. Lao wao humo ni kupiga mayowe, na wala hawatasikia (jenginelo).
100
101. Ama wale ambao wema wetu umewatangulia, hao watatenganishwa
na hayo.
101
102. Hawatausikia mvumo wake, na wao watadumu katika yale zinayo
yatamani nafsi zao.
102
103. Hicho Kitisho Kikubwa hakito wahuzunisha. Na Malaika watawapokea
(kwa kuwaambia): Hii ndiyo Siku yenu mliyo kuwa mkiahidiwa!
103
104. Siku tutakapo zikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi za vitabu.
Kama tulivyo anza umbo la mwanzo tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu
yetu. Hakika Sisi ni watendao.
104
105. Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu,
ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.
105
106. Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.
106
107. Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.
107
108. Sema: Hakika imefunuliwa kwangu ya kwamba hakika Mungu wenu
ni Mungu Mmoja tu. Je! Mmesilimu?
108
109. Na kama wakigeuka, basi sema: Nimekutangazieni sawa sawa, wala
sijui yako karibu au mbali hayo mliyo ahidiwa.
109
110. Hakika Yeye anajua kauli ya dhaahiri na anajua myafichayo.
110
111. Wala sijui pengine huu ni mtihani tu kwenu na starehe mpaka
muda kidogo.
111
112. Sema: Mola wangu Mlezi! Hukumu kwa haki. Na Mola wetu Mlezi
ni Mwingi wa Rehema, aombwaye msaada juu ya mnayo yazua;
112
Sura Nyingine | Faharasa |