54.Suurat Al-Qamar |
Imeshuka Makka | Ina aya 55 |
Utangulizi | Orodha ya Sura | Faharasa |
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0
1. Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!
1
2. Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi
kuendelea.
1
3. Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye
kuthibiti.
3
4. Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio.
4
5. Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu!
5
6. Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo
chusha;
6
7. Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio tawanyika,
7
8. Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu.
8
9. Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na
wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa.
9
10. Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi nimeshindwa,
basi ninusuru!
10
11. Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika.
11
12. Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo
lilio kadiriwa.
12
13. Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba.
13
14. Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa.
14
15. Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye
kumbuka?
15
16. Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu.
16
17. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika.
Lakini yupo anaye kumbuka?
17
18. Kina A'di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo
yangu?
18
19. Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi
mfululizo,
19
20. Ukiwang'oa watu kama vigogo vya mitende vilio ng'olewa.20
21. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?
21
22. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani nyepesi kufahamika;
lakini yupo anaye kumbuka?
22
23. Thamudi waliwakanusha Waonyaji.
23
24. Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo
sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa!
24
25. Ni yeye tu aliye teremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali
huyu ni mwongo mwenye kiburi!
25
26. Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi.
26
27. Hakika Sisi tutawapelekea ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame
tu na ustahamili.27
28. Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya
maji itahudhuriwa na aliye khusika.
28
29. Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja.
29
30. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu!
30
31. Hakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa
ya kujengea uwa.
31
32. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kwa kukumbuka,
lakini yupo akumbukaye?
32
33. Kaumu Lut'i nao waliwakadhibisha Waonyaji.
33
34. Hakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo kuwa wafuasi
wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri.34
35. Kwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anaye shukuru.
35
36. Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia
shaka hayo maonyo.
36
37. Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia:
Onjeni basi adhabu na maonyo yangu!
37
38. Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea.
38
39. Basi onjeni adhabu na maonyo yangu!<
39
40. Na hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye
kumbuka?
40
41. Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni.
41
42. Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika kama anavyo
shika Mwenye nguvu Mwenye uweza.42
43. Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni
kuwa nyinyi hamtiwi makosani?
43
44. Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu.
44
45. Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma.
45
46. Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi
na chungu zaidi.
46
47. Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu.
47
48. Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso
wa Jahannamu!
48
49. Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.
49
50. Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho.
50
51. Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye
kumbuka?
51
52. Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni.
52
53. Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa.
53
54. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito.
54
55. Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.
55
Sura Nyingine | Faharasa |