76.Suuratul Al Insan |
Imeshuka Madina | Ina aya 31 |
Utangulizi | Sura Nyingine | Faharasa |
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0
1. Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba
hakuwa kitu kinacho tajwa.
1
2. Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba
hakuwa kitu kinacho tajwa.
2
3. Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye
kukufuru.
3
4. kika HaSisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto
mkali.
4
5. Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyo changanyika
na kafuri,
5
6. Ni chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike
kwa wingi.
6
7. Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea
sana,7
8. Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima,
na wafungwa.
8
9. Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki
kwenu malipo wala shukrani.
9
10. Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida
na taabu.
10
11. Basi Mwenyna raha na furahaezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha.
11
12. Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo
subiri.
12
13 Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali
wala baridi kali.
13
14 Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia
mpaka chini.
14
15 Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae,
15
16 Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo.
16
17 Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi.
17
18 Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil.
18
19 Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasio pevuka, ukiwaona
utawafikiri ni lulu zilizo tawanywa.
19
20 Na utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa.
20
21 Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri
nzito ya at'ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha
kinywaji safi kabisa.
21
22 Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa.
22
23 Hakika Sisi tumekuteremshia Qur'ani kidogo kidogo.
23
24 Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimt'ii miongoni
mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru.
24
25 Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni;
25
26 Na usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati mrefu.
26
27 Kwa hakika watu hawa wanapenda maisha ya kidunia, na wanaiacha
nyuma yao siku nzito.
27
28 Sisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na tukitaka
tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao.
28
29 Hakika haya ni mawaidha; basi anaye taka atashika Njia ya kwenda
kwa Mola wake Mlezi.
29
30 Wala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi
Mungu ni Mwenye ilimu, Mwenye hikima.
30
31 Humuingiza amtakaye katika rehema yake. Na wenye kudhulumu amewawekea
adhabu iliyo chungu.
31
Sura Nyingine | Faharasa |