Al Qaaria'h Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
101.Surat Al-Qaaria'h

Imeshuka Makka Ina aya 11
Utangulizi Orodha ya Sura KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. Inayo gonga! 1


2. Nini Inayo gonga? 2


3. Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga? 3


4. Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika; 4


5. Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa! 5


6. Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, 6


7. Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza. 7


8. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, 8


9. Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! 9


10. Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo? 10


11. Ni Moto mkali! 11


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani