Al Takaathur Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
102.Surat At-Takaathur

Imeshuka Makka Ina aya 8
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. Kumekushughulisheni kutafuta wingi, 1


2Mpaka mje makaburini! 3. Sivyo hivyo! Mtakuja jua! 3


4. Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua! 4


5. Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini, 5


6. Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu! 6


7. Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini. 7


8. Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema. 8


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani