1.Surat Al-Kafirun |
Imeshuka Makka | Ina aya 6 |
Utangulizi | Orodha ya Sura | Faharasa |
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0
1. Sema: Enyi makafiri! 1
2. Siabudu mnacho kiabudu; 2
3. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. 3
4. Wala sitaabudu mnacho abudu. 4
5. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. 5
6. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu. 6
Sura Nyingine | Faharasa |