Al Infit'aar Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
82.Surat Al-Infit'aar

Imeshuka Makka Ina aya 19
Utangulizi Sura Nyingine Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. Mbingu itapo chanika, 1


2. Na nyota zitapo tawanyika, 2


3. Na bahari zitakapo pasuliwa, 3


4. Na makaburi yatapo fukuliwa, 4


5. Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma. 5


6. Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? 6


7. Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha, 7


8. Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga. 8


9. Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo. 9


10. Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu, 10


11. Waandishi wenye hishima, 11


12. Wanayajua mnayo yatenda. 12


13. Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema, 13


14. Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni; 14


15. Wataingia humo Siku ya Malipo. 15


16. Na hawatoacha kuwamo humo. 16


17. Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? 17


18. Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? 18


19. Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu. 19


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani