Al Ghaashiyah Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
88.Surat Al-Ghaashiyah

Imeshuka Makka Ina aya 26
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?1


2. Siku hiyo nyuso zitainama, 2


3. Zikifanya kazi, nazo taabani. 3


4. Ziingie katika Moto unao waka 4


5. Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka. 5


6. Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba. 6


7. Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa. 7


8. Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu. 8


9. Zitakuwa radhi kwa juhudi yao, 9


10. Katika Bustani ya juu. 10


11. Hawatasikia humo upuuzi.Humo imo chemchem inayo miminika. 11


12. Humo imo chemchem inayo miminika. 12


13. Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa, 13


14. Na bilauri zilizo pangwa, 14


15. Na matakia safu safu, 15


16. Na mazulia yaliyo tandikwa. 16


17. Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa? 17


18. Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa? 18


19. Na milima jinsi ilivyo thibitishwa? 19


20. Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa? 20


21. Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji. 21


22. Wewe si mwenye kuwatawalia. 22


23. Lakini anaye rudi nyuma na kukataa, 23


24. 24


25. Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao. 25


26. Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao! 26


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani