Al Balad Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
90.Surat al-Balad

Imeshuka Makka Ina aya 20
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. Naapa kwa Mji huu! 1


2.Nawe unaukaa Mji huu. 2


3. Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. 3


4. Hakika tumemuumba mtu katika taabu. 4


5. Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? 5


6. Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. 6


7. Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? 7


8. Kwani hatukumpa macho mawili? 8


9. Na ulimi, na midomo miwili? 9


10. Na tukambainishia zote njia mbili? 10


11. Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. 11


12. Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? 12


13. Kumkomboa mtumwa; 13


14. Au kumlisha siku ya njaa 14


15. Yatima aliye jamaa, 15


16. Au masikini aliye vumbini. 16


17. Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. 17


18. Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. 18


19. Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. 19


20. Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande. 20


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani