Ash sharh Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
94.Surat Ash-Sharh'

Imeshuka Makka Ina aya 8
Utangulizi Sura Nyingine Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. 1. Hatukukunjulia kifua chako? 1


2. Na tukakuondolea mzigo wako, 2


3. Ulio vunja mgongo wako? 3


4. Na tukakunyanyulia utajo wako? 4


5. Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi, 5


6. Hakika pamoja na uzito upo wepesi. 6


7. Na ukipata faragha, fanya juhudi. 7


8. Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie. 8


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani