At Tin Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
95.Surat At-Tin

Imeshuka Makka Ina aya 8
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. Naapa kwa tini na zaituni! 1


2. Na kwa Mlima wa Sinai! 2


3. Na kwa mji huu wenye amani! 3


4. Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa. 4


5. Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini! 5


6. Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha. 6


7. Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo? 7


8. Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote? 8


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani