Al Qadr Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
97.Surat Al-Qadr

Imeshuka Makka Ina aya 5
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu. 1


2. Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri? 2


3. Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. 3


4. Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. 4


5. Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri. 5


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani