Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Ya-sin

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Ya-Sin: Hizi ni harufi mbili zilizo anzia Sura hii kwa mujibu wa mpango wa Qur'ani katika kuanzia baadhi ya Sura kwa harufi moja moja.
Rudi kwenye sura

* 2. Ninaapa kwa Qur'ani yenye kukusanya hikima na ilimu yenye manufaa.
Rudi kwenye sura

* 3. Hakika wewe, Muhammad, ni katika wale ambao Mwenyezi Mungu amewatuma kwa watu wawapelekee Uwongofu na Dini ya Haki.
Rudi kwenye sura

* 4. Juu ya Njia Iliyo Sawa, nayo ndiyo Dini ya Kiislamu.
Rudi kwenye sura

* 5. Ni mteremsho wa Mwenye nguvu Mwenye kushinda kila kitu, ambaye hapana mtu awezae kumzuia chochote akitakacho. Mwenye kuwarehemu waja wake, kwa kuwatumia watu wa kuwaongoza njia ya kuokoka.
Rudi kwenye sura

* 6. Ili uwaonye watu ambao baba zao wa karibu hawakupata kuonywa, na kwa hivyo wamesahau yanayo wajibikia kwa Mwenyezi Mungu, na kwa nafsi zao, na kwa watu.
Rudi kwenye sura

* 7. Sisi tulikwisha jua kuwa wengi wao hawatakhiari Imani. Basi yale tuliyo kuwa tunayajua yamewafikiana na yaliyo kwao. Basi haitakuwapo Imani kutoka kwao.
Rudi kwenye sura

* 8. Sisi tumewafanya hao wanao kakamia juu ya ukafiri ni kama walio tiwa minyororo shingoni mwao, ikawafika videvuni mwao. Na mikono yao ikawa imefungwa kwenye vichwa vyao, vikawa vimenyanyuka juu na macho yao yameinama. Basi hawawezi kuvizungusha vichwa vyao wapate kuona.
Rudi kwenye sura

* 9. Na tumewafanya wale walio zuwiwa wasione Ishara na dalili ni kama walio fungwa baina ya kuta mbili, na macho yao yakagubikwa, wasione yaliyo mbele yao wala yaliyo nyuma yao.
Rudi kwenye sura

* 10. Na ni sawa kwao ukiwahadharisha au ukito wahadharisha, hawaamini hao.
Rudi kwenye sura

* 11. Hakika wanao nafiika kwa kuhadharisha kwako ni wale wanao ifuata Qur'ani na wakamkhofu Arrahman, ijapo kuwa hawamwoni. Basi watu hawa wape bishara njema kuwa Mwenyezi Mungu atawasamehe madhambi yao, na atawalipa malipo mema kwa vitendo vyao.
Rudi kwenye sura

* 12. Hakika Sisi tunawahuisha maiti, na tunayaandika yote waliyo yatenda na wakayakadimisha duniani, na walio yabakisha humo kuwa ni athari, mabaki, yao baada ya kufa kwao. Na kila kitu kimo katika Kitabu kilicho wazi.
Rudi kwenye sura

* 13. Ewe Nabii! Watajie watu wako kisa cha mji mmoja.(1) Kwani hicho ni kama kisa chao. Waliwaendea Wajumbe walio tumwa ili wawahidi. (1) Baadhi wa wafasiri wanasema mji huo ni Antiokia.
Rudi kwenye sura

* 14. Tuliwatuma wajumbe wawili, wakawakadhibisha. Tukawaongeza nguvu kwa kumpeleka mwengine wa tatu. Basi hawa watatu wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu!
Rudi kwenye sura

* 15. Wale watu wa mji wakasema kuwajibu: Nyinyi si chochote ila ni wanaadamu kama sisi. Na Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema hakuteremsha wahyi wowote kwa mwanaadamu. Nyinyi ni watu mnao sema yasiyo kuwapo.
Rudi kwenye sura

* 16. Wale Wajumbe wakasema: Mola wetu Mlezi aliye tutuma anajua kuwa hakika sisi bila ya shaka tumetumwa kwenu.
Rudi kwenye sura

* 17. Na sisi hatuna waajibu wowote ila kufikilisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu ufike kwa uwazi.
Rudi kwenye sura

* 18. Wana mji wale wakasema: Sisi tunaona kuwa nyinyi mnatuletea ukorofi. Na tunaapa, lau kuwa hamsiti na huo wito wenu hapana shaka tutakupopoeni kwa mawe, na hapana shaka mtapata kwetu adhabu kali yenye kutia uchungu.
Rudi kwenye sura

* 19. Wale Wajumbe wakasema: Ukorofi mnao nyinyi wenyewe, kwa hizo kufuru zenu. Badala ya kuwaidhika kwa mambo yenye kheri kwenu wenyewe, mnatutuhumu sisi kuwa ni wakorofi, na mnatutishia kutupa adhabu chungu? Lakini nyinyi ni watu mlio pindukia mipaka ya Haki na Uadilifu.
Rudi kwenye sura

* 20. Akaja mtu kutoka huko mwisho wa mji akiwakimbilia wale wanamji, akawaambia: Wafuateni hawa walio tumwa kwenu na Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura

* 21. Wafuateni watu wasio taka kwenu ujira wowote kwa kukunasihini na kukuongozeni, na hali wao wenyewe wameongoka, na nyinyi mtapata manufaa kwa kufuata njia ya kheri na mafanikio!
Rudi kwenye sura

* 22. Na kitu gani cha kunizuia hata nisimuabudu yule aliye niumba, na ambaye kwake Yeye, si kwa mwenginewe, ndio mtarejea?
Rudi kwenye sura

* 23. Je! Niishike kwa kuiabudu badala ya Mwenyezi Mungu, miungu mingine isiyo nifaa kitu kuniombea kwao, pindi Mwenyezi Mungu akinitakia madhara? Wala hawataniokoa nayo yakinishukia hayo madhara.
Rudi kwenye sura

* 24. Basi hakika mimi nikiiabudu miungu mingine badala yake Yeye, nitakuwa katika upotovu ulio dhaahiri.
Rudi kwenye sura

* 25. Hakika mimi ninamsadiki Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni, na ndiye Mwenye kutawala mambo yenu. Basi nisikilezeni na mnit'ii.
Rudi kwenye sura

* 26,27. Kuwa ni malipo ya Imani yake na wito wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ataambiwa: Ingia Peponi! Naye, hali yuko katika kivuli cha neema na hishima, atasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua alivyo nighufiria Mola wangu Mlezi na kunipa hishima, nao wakaamini kama nilivyo amini mimi.
Rudi kwenye sura

* 26,27. Kuwa ni malipo ya Imani yake na wito wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ataambiwa: Ingia Peponi! Naye, hali yuko katika kivuli cha neema na hishima, atasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua alivyo nighufiria Mola wangu Mlezi na kunipa hishima, nao wakaamini kama nilivyo amini mimi.
Rudi kwenye sura

* 28. Na Sisi hatukawaangamiza kwa kuwapelekea maaskari kutoka mbinguni. Wala huo sio mtindo wetu kupeleka majeshi tunapo yahiliki mataifa.
Rudi kwenye sura

* 29. Kuteketezwa kwao hakukuwa ila ni kwa ukelele mmoja tu tulio wapelekea. Na mara wao wakawa ni maiti, kama moto ulio zimwa.
Rudi kwenye sura

* 30. Ee khasara yao, inayo faa kusikitikiwa! Hatuwapelekei waja wangu Mtume ila wao huwa wakimfanyia maskhara.
Rudi kwenye sura

* 31. Kwani wao hawayazingatii mataifa mengi yaliyo tangulia tuliyo yahiliki? Hakika hao hawarejei tena kwenye maisha yao ya duniani.
Rudi kwenye sura

* 32. Hapana katika mataifa yaliyo tangulia na yajayo ila wote watakusanywa mbele yetu, nao wamelazimishwa kuhudhuria mbele yetu.
Rudi kwenye sura

* 33. Na dalili kwao ya uweza wetu wa kufufua ni kuangalia vipi ardhi yenye ukame tunavyo ihuisha kwa maji, na kutoa ndani yake nafaka wanazo zila.
Rudi kwenye sura

* 34,35. Na humo tukafanya vitalu na mabustani ya mitende na mizabibu, na tukapasua humo chemchem ya kumwagia maji kwenye miti yake, na ikatoa matunda, na wao wakala katika hayo. Na hayo si kazi ya mikono yao. Basi kwa nini hawatoi haki ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yao kwa kumuamini na kumshukuru?
Rudi kwenye sura

* 34,35. Na humo tukafanya vitalu na mabustani ya mitende na mizabibu, na tukapasua humo chemchem ya kumwagia maji kwenye miti yake, na ikatoa matunda, na wao wakala katika hayo. Na hayo si kazi ya mikono yao. Basi kwa nini hawatoi haki ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yao kwa kumuamini na kumshukuru?
Rudi kwenye sura

* 36. Wa kutakasika ni Mwenyezi Mungu aliye umba kila kitu kwa mpango wa ume na uke, katika mimea na katika nafsi zao watu, na katika vitu ambavyo watu hawavijui. Hii harufi Min , yaani "Katika" katika Aya hii ni ya kubainisha. Maana yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ameumba madume na majike katika viumbe vyake vyote, sawa sawa katika mimea, na wanyama, na wanaadamu na vyenginevyo ambavyo watu hawavijui na hawavioni.
Rudi kwenye sura

* 37. Na Ishara pia ya kuwepo Mwenyezi Mungu na uweza wake, ni huu usiku ambao tunautoa ndani yake mchana, kama kuivua nguo inayo sitiri. Mara utaona watu wamo gizani lilio wazunguka kila upande.
Rudi kwenye sura

* 38. Na jua linakwenda katika njia yake maalumu. Mwenyezi Mungu amekwisha kadiria kwa zama na mahala. Huo ndio mpango wake Mwenye kushinda kwa uweza wake, Mwenye kuvizunguka vitu vyote kwa ujuzi wake.
Rudi kwenye sura

* 39. Na mwezi kwa mpango wetu tumeujaalia una vituo vyake. Mwanzo wa mwezi unakuwa mdogo na mwembamba. Kisha kila usiku unazidi kukua mpaka unatimia kuwa mbaamwezi. Tena unaingia kupungua vile vile, mpaka ukawa kama karara la mtende linapo kuwa kongwe limepindana na limekuwa manjano.
Rudi kwenye sura

* 40. Haipelekei jua likaacha sharia zake likakutana na mwezi, na likaingia katika njia zake. Wala usiku hauwi kuushinda mchana ukauzuia usije, bali vyote viwili hivyo hupeana zamu. Na vyote, jua na mwezi, na vyenginevyo vyote vinaogelea katika njia zao za mbinguni, wala haviachi njia. Hakika Aya hizi tukufu zinabainisha ukweli wa ki-ilimu ambao wataalamu walikuwa hawaujui ila mwanzo wa karne ya kumi na nne ya kuzaliwa Nabii Isa. Na jua ni moja katika nyota za mbinguni, nalo kama nyota zilizo baki lina mwendo wake wenyewe. Lakini linakhitalifiana na nyota nyengine kwa kuwa lipo karibu na dunia, na kwa kuwa lina kundi la sayari na miezi ya mikia na sayari ndogo ndogo zinazo lifuata daima, na zinat'ii mvuto wake. Kwa hivyo zinakuwa hizo zinazunguka kwa kufuatana kwa utungo kama sura ya yai. Na mkusanyo wote huu unakwenda angani pamoja na jua kwa mvuto wake. Kwa ufupi jua, na ardhi, na mwezi na sayari zote na vyombo vyote hivyo vinakwenda angani kwa mbio maalumu, na kuelekea jiha maalumu. Na yaonekana kuwa jua na mkusanyo wote huo wake, na nyota zilizo karibu nalo zipo katika mkusanyo ulio tanda katika mbingu inayo itwa kwa Kiarabu Sadiimu almajarrah, au kwa Kiingereza Nebula course. Na imebainika kwa masomo ya kisasa sehemu zote za hiyo Nebula zinaizunguka kati yake kwa mbio ya kunasibiana na kinyume cha umbali wake kutoka hapo kati. Pia imeonakana kuwa jua na ardhi na sayari zake na nyota zilio karibu nayo, vyote hivyo vinakwenda mbio, na upande maalumu. Mbio zake zinafika kilomita 700 kila nukta moja. Na kunatimia kuzunguka kwake kukizunguka hicho kituo cha kati kwa kiasi ya miaka milioni 200 ya muangaza. Na kiini cha maneno ni kuwa Aya tukufu iliyo taja kuwa jua linakwenda kwa kiwango chake, hawakujua wataalamu uzuri wake wa ndani mpaka katika mwanzo wa karne hii. Wala hayamkini jua kuupata mwezi, kwani kila kimojapo kinakwenda katika njia zake mbali mbali, basi ni muhali kukutana, kama ilivyo kuwa ni muhali kupitana usiku na mchana. Hayo ingeli takikana ardhi izunguke juu ya msumari-kati wake kutoka mashariki kwendea magharibi, kinyume na ilivyo hivi sasa kutoka magharibi kwendea mashariki. Na mwezi katika kuizunguka kwake ardhi, na ardhi kulizunguka jua, huenda pamoja na mkusanyo wa nyota unao itwa Manaazil Alqamar au Lunar system. Na katika robo ya mwanzo na ya mwisho wa mwezi huonekana sura yake kama karara kongwe au kole lilio kauka, linapo kuwa kongwe na kunyauka.
Rudi kwenye sura

* 41. Na Ishara nyengine kwao ni kuwa Sisi tuliwapakia wanaadamu katika jahazi ilio jaa bidhaa zao na riziki zao.
Rudi kwenye sura

* 42. Na tukawaumbia mfano wa hiyo marikebu na vyenginevyo wanavyo vipanda kadhaalika.
Rudi kwenye sura

* 43. Na tukitaka kuwazamisha, tunawazamisha. Na wala hawapati wa kuwaopoa, wala hawapati wa kuwaokoa wasiangamie.
Rudi kwenye sura

* 44. Lakini Sisi hatuwazamishi, kwa sababu ya rehema inayo tokana nasi, na ili tuwastareheshe kwa muda ulio kwisha kadiriwa.
Rudi kwenye sura

* 45. Na wanapo ambiwa: Yaogopeni mfano wa yaliyo wapata mataifa yaliyo kwisha pita kwa kukadhibisha kwao, na iogopeni adhabu ya Akhera ambayo itakupateni kwa kushikilia kwenu ukafiri, kwa kutaraji kuwa asaa Mola wenu Mlezi akakurehemuni mkimcha Yeye, wao hupuuza.
Rudi kwenye sura

* 46. Na haiwajii hoja katika hoja za Mola wao Mlezi, yenye kuonyesha Upweke wa Mwenyezi Mungu na uweza wake, ila wao huipa nyongo, hawaijali.
Rudi kwenye sura

* 47. Na wakiambiwa: Wapeni mafakiri kutokana na hicho alicho kuruzukuni Mwenyezi Mungu, makafiri huwaambia Waumini: Je! Tuwalishe watu ambao Mwenyezi Mungu Mwenyewe angeli taka angeli walisha? Hivyo inakuwa tunamfanyia inda Mwenyezi Mungu kwenda kinyume na mapenzi yake! Nyinyi mnao taka tutoe, si chochote ila mmo katika upofu ulio wazi, hamuioni Haki.
Rudi kwenye sura

* 48. Na huwaambia Waumini kwa kuwafanyia kejeli: Lini yatatokea hayo mlio tuahidi, kama nyinyi mnasema kweli katika mnayo ahidi?
Rudi kwenye sura

* 49. Hawangojei ila sauti moja tu, iwamalize kwa ghafla, nao wakizozana katika mambo ya kidunia, wameghafilika na Akhera.
Rudi kwenye sura

* 50. Kwa upesi wa hayo yatakayo wateremkia, hawatowahi kuusia chochote, wala kurejea kwa ahali zao.
Rudi kwenye sura

* 51. Na barugumu litapulizwa kwa mpulizo wa kufufua watu. Mara watu watatoka makaburini mwao wakikimbilia kwenda kukutana na Mwenyezi Mungu. Na hilo barugumu, na kupulizwa kwake, ni katika anayo yajua Mwenyezi Mungu Yeye peke yake.
Rudi kwenye sura

* 52. Watasema watakao fufuliwa kutoka makaburini: Balaa gani lilio tushukia! Nani aliye tuamsha tukauwacha usingizi wetu? Jawabu ya suala lao itawajia: Hii ndiyo siku ya kufufuliwa aliyo waahidia Arrahaman, Mwingi wa Rehema, waja wake, na Mitume wakaisemea kweli kwa waliyo yasimulia.
Rudi kwenye sura

* 53. Wito wao wa kuwatoa hautakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote watakusanywa mbele yetu wahudhurishwe ili tuwahisabie.
Rudi kwenye sura

* 54. Basi katika hii siku ya leo haipungukiwi nafsi na chochote katika ujira wake kwa kazi iliyo tenda. Na wala hamtopata isipo kuwa jaza ya mliyo kuwa mkiyatenda, ikiwa ni kheri au shari.
Rudi kwenye sura

* 55. Hakika watu wa Peponi hii leo watakuwa wameshughulika kwa neema walizo nazo, wakistaajabia na kufurahia.
Rudi kwenye sura

* 56. Wao na wake zao wamo katika vivuli vilivyo enea, wameegemea juu ya viti vilivyo pambwa.
Rudi kwenye sura

* 56. Wao na wake zao wamo katika vivuli vilivyo enea, wameegemea juu ya viti vilivyo pambwa.
Rudi kwenye sura

* 58. Wataambiwa: "Salama", kuwa ni kauli iliyo toka kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu.
Rudi kwenye sura

* 59. Na wataambiwa wakosefu siku hii ya leo: Jitengeni mbali na Waumini.
Rudi kwenye sura

* 60. Enyi wanaadamu! Sikukuusieni kuwa msimfuate Shetani kwa ut'iifu kama kwamba ni mungu wa kuabudiwa. Hakika yeye ni adui yenu, aliye dhihirisha uadui wake.
Rudi kwenye sura

* 61. Na nyinyi mniabudu Mimi peke yangu, kwani kuniabudu Mimi tu ndiyo Njia kuu katika kusimamisha Dini sawa.
Rudi kwenye sura

* 62. Na Shetani amewapotoa viumbe wengi kati yenu. Nyinyi mmeghafilika na hayo. Basi hamkuwa mkifikiri mlipo mt'ii yeye?
Rudi kwenye sura

* 63. Wataambiwa: Hii ndiyo Jahannamu mliyo kuwa mkiahidiwa mlipo kuwa duniani. Ndiyo jaza ya ukafiri wenu.
Rudi kwenye sura

* 64. Ingieni! Na hilikini kwa joto lake hii leo kwa ukafiri wenu!
Rudi kwenye sura

* 65. Leo vitazibwa vinywa vyao, basi havito tamka kitu. Mikono yao ndiyo itakayo sema nasi, na miguu yao itatamka kwa kutoa ushahidi juu yao kwa waliyo kuwa wakiyafanya.
Rudi kwenye sura

* 66. Na tungeli taka kuwatia upofu duniani tungeli watia upofu, wakawa wanaipapasa njia ya kupita wasiweze kuiona. Wataionaje nasi tumewapofoa!
Rudi kwenye sura

* 67. Na lau tungeli taka kuzigeuza sura zao tungeli zigeuza zikawa mbaya, juu ya kuwa wana nguvu na vyeo. Hata wasinge weza kwenda mbele wala kurudi nyuma, kwa kuwa inge kuwa tumevunja nguvu zao.
Rudi kwenye sura

* 68. Na tunaye mfanyia umri wake ukawa mrefu, tunamrudisha, kutoka nguvu akawa dhaifu. Basi je hawayazingatii haya wakayatia akilini ya uweza wetu kuyafanya haya, na wao wakajua kuwa dunia ni nyumba ya kupita ina mwisho wake, na kuwa Akhera ndiyo nyumba ya kubaki na kudumu? Na tunaye mfanyia umri wake uwe mrefu tunamrejesha awe kinyume na alivyo kuwa. Yaani baada ya kuwa na nguvu anakuwa dhaifu. Hayo ni kwa kuwa maisha ya mwanaadamu yanapitia vipindi vitatu, kukua, kutimia kukua; na ukongwe unaanza kwa kunywea kwa mafigo, ini, Ghudda Ddarqiya au Thyroid gland, na Pancreas, yaani Dongoronya. Na haya huleta athari katika kudhoofika mwili wote. Mishipa ya damu nayo huanza kukacha na kunywea, na kwa hivyo hupunguka damu inayo kwenda katika viungo vyote vya mwili, basi ndio huzidi udhaifu juu ya udhaifu. Na katika sababu za kukonga ni kuzidi nguvu za kubomoka kuliko kujengeka katika mwili, yaani Metabolism. Na hayo ni kwa kuwa Khalaya au Cells, za mwili zote zimo katika hali ya kugeuka, na pia Khalaya za damu, isipo kuwa Khalaya za ubongo wa kichwani na wa katika mifupa. Hizo hazigeuki muda wote wa uhai. Ikiwa kiasi ya kuundika upya ni sawa ya kiasi cha kuharibika, basi hapana madhara yanayo tokea. Lakini ikiwa kuharibika ni kukubwa kuliko kujengeka katika kiungo chochote basi hapo hudhihiri madhara kwenye kiungo hicho. Na kwa hivyo kila umri ukiwa mkubwa kiasi cha kujengeka kinapungua na kinazidi kiasi cha kubomoka kwa Khalaya, na kunadhihiri kunywea, na kupungua nguvu kote. Na hukhitalifiana kiasi cha kujengeka kwa mnasaba wa kubomoka kwa kukhitalifiana namna ya mfumo (Nasiij, Texture). Katika hayo yanayo dhihiri kama ngozi iliyo funika mwili, na zilio funika paipu za kusaga chakula, na paipu za Ghudad, Glands, zinachakaa kwa upesi zaidi kila miaka ya binaadamu ikipita. Na hii ni sababu ya kuonekana upesi alama za kuzeeka.
Rudi kwenye sura

* 69. Na Sisi hatukumfunza Mtume kutunga mashairi. Wala haifai hivyo, kwa kuzingatia pahala pake na cheo chake awe mtungaji mashairi! Hii Qur'ani iliyo teremka juu yake si chochote ila ni mawaidha, na Kitabu cha mbinguni kilio wazi. Hakikhusiani kabisa na mashairi.
Rudi kwenye sura

* 70. Hii Qur'ani ni kumtia khofu mwenye moyo ulio hai ulio nawirika kwa akili. Na ipite hukumu ya adhabu kuwashukia wanao ipinga Qur'ani, wenye kukataa uwongofu wake.
Rudi kwenye sura

* 71. Je! Makafiri wameingiwa na upofu hata hawaoni kwamba Sisi tumewaumbia kutokana na iliyo fanya kudra yetu nyama hoa, wanyama wa mifugo, (1) na wao wamekuwa wanawamiliki, wanawatumilia kama wapendavyo? (1) Ngamia, kondoo, mbuzi na ng'ombe.
Rudi kwenye sura

* 72. Na hao wanyama tumewafanya wawatumikie. Wengine basi wanawapanda, na wengine wanawala.
Rudi kwenye sura

* 73. Na wanapata kwa hao vitu vya kuwapa manufaa, kama sufi, na manyoya, na nywele, na ngozi, na mafupa, na vinywaji kutokana na maziwa yao. Je! Wanasahau neema hizi hata wamekuwa hawamshukuru aliye waneemesha?
Rudi kwenye sura

* 74. Na washirikina wamefanya miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu wakiwaabudu kwa kutaraji kuwa ati watawasaidia.
Rudi kwenye sura

* 75. Hiyo miungu ya uwongo haiwezi kuwasaidia kwa lolote Mwenyezi Mungu akiwatakia madhara. Kwani miungu hiyo haiwezi kunafiisha wala kudhuru. Bali wao kwa hiyo miungu isiyo weza kitu, ni kama askari walio tayarishwa kwa ajili ya kuwakhudumia na wa kuwalinda na madhara.
Rudi kwenye sura

* 76. Basi yasikuhuzunishe maneno yao kumkhusu Mwenyezi Mungu kwa kumkufuru, na kukukhusu wewe kwa kukwambia mwongo. Hakika Sisi tunayajua wanayo yaficha na wanayo yatangaza. Nasi tutawalipa kwa hayo.
Rudi kwenye sura

* 77. Je! Binaadamu anakataa kuwepo Mwenyezi Mungu na uweza wake, na haoni yeye kwamba Sisi, baada ya kuwa hata hayupo, tulimuumba kutokana na tone la manii dhalili? Na sasa amekuwa mkali wa kutukhasimu kwa uwazi kabisa?
Rudi kwenye sura

* 78. Tena huyu mpingaji aliye dhaahiri ametupigia mfano ambao kwao anakanya uweza wetu kufufua mafupa baada ya kuoza na kusagika. Na amesahau kuwa Sisi tulimuumba yeye, naye hata hakuwepo aslani. Akasema kwa kukanya na kuona haliwezi kuwa hilo: Ni nani huyo atakaye yafufua mafupa nayo yamekwisha mung'unyika?
Rudi kwenye sura

* 79. Ewe Muhammad! Sema: Atayafufua yule yule aliye yaumba hapo mara ya kwanza. Kwani aliye anza anao uweza wa kufanya tena. Naye ni Mkubwa wa kujua kila alicho kiumba. Basi haemewi Yeye na kukusanya vipande vipande baada ya kutawanyika.
Rudi kwenye sura

* 80. Aliye kuumbieni moto kutoka mti mbichi, baada ya kwisha kauka. Nguvu za jua zinaingia ndani ya mimea kwa wasita wa mwangaza. Khalaya zenye madda ya kijani katika mimea Chlorophyl ndizo zinafyonza Carbon dioxide kutokana na hewa, na hii huchanganyika na maji yanayo fonzwa na mimea, na kufanyika Carbohydrates kwa kuathiriwa na nguvu zinazo tokana na mwangaza wa jua. Tena hufanyika mbao, kuni, ambazo sehemu kubwa ni muundo wa kimyaa wa Carbon na Hydrogen na Oxygen. Na kutokana na kuni hizi hufanyika makaa haya ya miti tuyatumiayo. Ukiyachoma makaa hutoka nguvu zilizo kuwamo ndani yake kwa ajili ya kupikia, na kwa kazi nyingi nyenginezo. Na makaa ya mawe si chochote ila ni hiyo hiyo mimea na miti iliyo kuwa na kufanyika kama ilivyo elezwa, na kisha ikazikika kwa njia fulani na kugeuka baada ya kupita mamilioni ya miaka kuwa makaa ya mawe, kwa kuathirika na hali za geology kama joto au mdidimizo au menginewe. Na yapasa kuzingatia kuwa kutajwa katika Aya hii "mti wa kijani" si bure, bali ni ishara ya hiyo Chlorophyll ya kijani ambayo ni lazima kwa ajili ya kuimeza Carbon dioxide katika mimea.
Rudi kwenye sura

* 81. Kwani hao wamepotelewa na akili zao hata hawajui kwamba aliye ziumba mbingu na ardhi, juu ya ukubwa wao, ni Muweza vile vile kurejesha kuwaumba wanaadamu ambao ni wadogo na hali yao ni dhaifu? Kwani? Yeye ni Muweza sana, na Yeye ni Mwingi wa kuumba, ambaye ujuzi wake umeenea kila kitu.
Rudi kwenye sura

* 82. Hakika shani yake katika kuumba anapo taka kiwe kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Kikawa, na hutokea hapo hapo!
Rudi kwenye sura

* 83. Basi Mtukufu ametakasika na kila kisicho laiki na dhati yake, yule ambaye katika kudra yake upo Ufalme wa kila kitu, kwa kuumba, na kupanga, na kuendesha - Kwake Yeye peke yake mtarejeshwa, akuhisabuni kwa a'mali zenu.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani