Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Addukhan

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. H'a Mim. Imeanzia Sura hii kwa baadhi ya harufi za kutamkwa kama ilivyo ada ya Qur'ani katika kufungulia Sura nyingi kwa harufi kama hizi.
Rudi kwenye sura

* 2. Mwenyezi Mungu anaapa kwa Qur'ani yenye kuweka wazi Dini ya Haki, yenye kuwabainishia watu yaliyo na maslaha ya dunia yao na Akhera yao, ili kujuulisha utukufu wa cheo chake.
Rudi kwenye sura

* 3. Hakika Sisi tumeanza kuiteremsha Qur'ani katika usiku ulio jaa kheri, wenye baraka nyingi, kwani ni mwendo wetu kuonya kwa kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu.
Rudi kwenye sura

* 4. Katika usiku huu wenye baraka hupambanuliwa baina ya mambo yote yenye hikima, na Qur'ani ndio kilele cha hikima, na ndio pambanuo baina ya kweli na uwongo. Na kwa hivyo ndio ikateremshwa katika usiku huo.
Rudi kwenye sura

* 5. Nakusudia kwa jambo hili, yaani jambo kuu lenye kutoka kwetu kama ilivyo kwisha pita hukumu ya mpango wetu. Kwani ni shani yetu kutuma Mitume kwa Vitabu ili kuwafikishia waja wetu.
Rudi kwenye sura

* 6. Kwa ajili ya rehema ya Mola wako Mlezi kwa waja wake, amewatuma Mitume kwa watu wawafikishie uwongofu wake, kwani hakika Yeye peke yake, ndiye Mwenye kusikia kila cha kusikiwa, Mwenye kujua kila cha kujuulikana.
Rudi kwenye sura

* 7. Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini na haki, na mnaifuata, na mnaamini kuwa hakika ndio Yeye Mwenye kuteremsha Qur'ani kuwa ni rehema na uwongofu.
Rudi kwenye sura

* 8. Hapana Mungu isipo kuwa Yeye anaye stahiki kuabudiwa, Yeye peke yake, Mwenye kuhuisha na kufisha. Na Yeye peke yake, ndiye aliye kuumbeni nyinyi na kawaumba baba zenu wa mwanzo.
Rudi kwenye sura

* 9. Lakini makafiri wana shaka na ukweli huu, wamo wakifuata pumbao lao. Na huo ndio mtindo wa watu wa pumbao na michezo, sio mwendo wa watu wa ilimu na yakini.
Rudi kwenye sura

* 10. Basi ewe Mtume! Ngojea ukame utapo wateremkia, wakasibiwa na kukonda na udhaifu wa kuona, ikawa mtu huwa anaona baina ya mbingu na ardhi moshi dhaahiri shaahiri, akawa anasikia mvumo wake wala hauoni.
Rudi kwenye sura

* 11. Moshi huu utawazunguka wale wanao kadhibisha walio sibiwa na ukame, watasema kwa wingi wa kitisho: Hii ni adhabu kali na chungu!
Rudi kwenye sura

* 12. Kama pia watavyo sema kwa kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu: Hakika sisi tutaamini ukituondolea adhabu ya njaa na dhiki.
Rudi kwenye sura

* 13. Watu hawa watawaidhika vipi, hata watimize hiyo Imani wanayo iahidi wakiondolewa adhabu, na hali Mtume mwenye ujumbe ulio wazi kesha wajia na miujiza yenye kuonyesha ukweli wake, na hayo ndiyo mawaidha makubwa kabisa?
Rudi kwenye sura

* 14. Kisha wakaacha kumsadiki Mtume aliye tiliwa nguvu na miujiza iliyo wazi, na wakamwambia: Huo uwongo na uzushi! Mara nyengine wakimsingizia kuwa amefunzwa hayo na mtu, na mara nyengine kuwa akili yake imekorogeka.
Rudi kwenye sura

* 15. Mwenyezi Mungu anawarudi: Sisi hakika tutakuondoleeni adhabu wakati wa duniani, nao ni wakati mchache, lakini nyinyi mtarejea tu, bila ya shaka, yale yale mliyo kuwa mkiyatenda.
Rudi kwenye sura

* 16. Ewe Mtume! Watajie ile siku tutapo washika kwa mshiko mkubwa, wa nguvu. Nasi kwa mshiko huu ndio tunawatesa.
Rudi kwenye sura

* 17. Na bila ya shaka tulikwisha wafanyia mtihani, kabla ya makafiri wa Makka, kaumu ya Firauni kwa kuwaitia kwenye Imani, na akawajia Musa, Mtume Mtukufu kwa Mwenyezi Mungu. Wakamkataa kwa inda tu. Na huo ndio mtindo wa hawa washirikina.
Rudi kwenye sura

* 18. Mtume Mtukufu aliwaambia: Nipeni enyi waja wa Mwenyezi Mungu lilio waajibu juu yenu, nalo ni kuitikia wito wangu, kwani mimi ni Mtume nimetumwa makhsusi kwenu, na ni muaminifu katika ujumbe wangu.
Rudi kwenye sura

* 19. Wala msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu kwa kumkadhibisha Mtume wake, kwani mimi nakuleteeni muujiza ulio wazi wa kubainisha ukweli wa Unabii wangu na Utume wangu.
Rudi kwenye sura

* 20. Na mimi najilinda na Mwenye kuniumba msiweze kuniuwa kwa kunipiga mawe.
Rudi kwenye sura

* 21. Na ikiwa hamnisadiki basi jitengeni nami, wala msiniudhi.
Rudi kwenye sura

* 22. Musa akamwambia Mola wake Mlezi kwa kumshitakia watu wake alipo kata tamaa nao kuwa hawaamini: Hakika watu hawa shauri yao imekwisha fika ukomo katika ukafiri; basi Wewe wafanyie wanalo stahiki.
Rudi kwenye sura

* 23. (Naye Musa akaambiwa:) Toka na Waumini usiku usiku kwa kificho, wasije kukupateni, kwani Firauni na askari wake watakufuateni pindi wakijua, wakukamateni.
Rudi kwenye sura

* 24. Na iache bahari imetulia kama ilivyo baada ya kwisha pigwa kwa fimbo, wapate kuingia hao wanao kanya; kwani wao watazama tu, hapana hivi wala hivi.
Rudi kwenye sura

* 25. Hao watu wa Firauni baada ya kuzama kwao waliacha mabustani mengi yenye kunawiri, na chemchem zinazo tiririka maji yake,
Rudi kwenye sura

* 26. Na makulima ya namna kwa namna, na makaazi mazuri mazuri,
Rudi kwenye sura

* 27. Na maisha ya raha na starehe, waliyo kuwa wakiyaonea utamu.
Rudi kwenye sura

* 28. Mfano wa adhabu hiyo Mwenyezi Mungu humuadhibu mwenye kwenda kinyume na amri yake, na akatoka katika ut'iifu wake, na humwondolea neema yule mwenye nayo akawapa watu wenginewe wasio kuwa na makhusiano nao yoyote, la ya ujamaa wala dini.
Rudi kwenye sura

* 29. Basi la mbingu wala ardhi hazikuwahuzunukia ilipo wanyakua adhabu, jinsi ilivyo haribika hali yao; wala hawakungojewa watubu, wala hawakupewa muhula wapate kudiriki taksiri yao, kwa jinsi walivyo dharauliwa!
Rudi kwenye sura

* 30. Na kwa hakika Mwenyezi Mungu aliwaokoa Wana wa Israili na adhabu ya kuwadhalilisha.
Rudi kwenye sura

* 31. Aliwaokoa kwa Firauni. Hakika Firauni alikuwa jeuri kwa watu wake, amepita mipaka kwa shari na uasi.
Rudi kwenye sura

* 32. Ninaapa: Tuliwakhiari Wana wa Israili kwa kuwa tuliwajua kwamba wao wana stahiki kuteuliwa kuliko watu wengine wote wa zama zao. Kwa hivyo tukawatuma miongoni mwao Manabii wengi kwa kuwa tulijua hali zao.
Rudi kwenye sura

* 33. Na Mwenyezi Mungu akawaletea katika mkono wa Musa dalili kadhaa wa kadhaa za kuwatia wao katika mitihani iliyo wazi.
Rudi kwenye sura

* 34,35. Hakika hawa wanao kadhibisha kufufuliwa bila ya shaka wanasema: Hapana kufa ila kwa haya haya mauti yetu ya kwanza ya duniani, wala sisi hatutafufuliwa tena.
Rudi kwenye sura

* 34,35. Hakika hawa wanao kadhibisha kufufuliwa bila ya shaka wanasema: Hapana kufa ila kwa haya haya mauti yetu ya kwanza ya duniani, wala sisi hatutafufuliwa tena.
Rudi kwenye sura

* 36. Na wao humwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu na Waumini: Ikiwa nyinyi mnasema kweli katika madai yenu kwamba Mola wenu Mlezi anahuisha wafu kwa ajili ya hisabu katika Akhera, basi upesi upesi tufufulieni baba zetu walio kwisha kufa, kwa kumwomba huyo Mola wenu Mlezi!
Rudi kwenye sura

* 37. Je! Makafiri wa Makka wanawashinda kaumu ya Tubbaa' na walio watangulia kwa nguvu, na ulinzi, na utawala, na mambo yote ya kidunia? Ewe Muhammad! Hao washirikina wa kaumu yako hawawashindi hao kwa nguvu, na hao Sisi tuliwateketeza katika dunia kwa ukafiri wao na madhambi yao. Basi nawawazingatie!
Rudi kwenye sura

* 38. Na Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na viliomo baina yao bila ya hikima.
Rudi kwenye sura

* 39. Hatukuziumba hizo ila kwa umbo lilio ambatana na hikima, kwa nidhamu iliyo thibiti yenye kuonyesha ushahidi wa kuwepo Mwenyezi Mungu wa pekee, Mwenye uwezo. Lakini wengi wa hawa wameghafilika, wamo katika upofu, hawazioni dalili hizi.
Rudi kwenye sura

* 40. Hakika siku ya hukumu kupambanua baina ya mwenye haki na asiye na haki, ni wakati walio ahidiwa wote.
Rudi kwenye sura

* 41. Siku ambayo jamaa hawezi kumtetea jamaa yake, wala rafiki kumtetea rafiki yake kwa lolote, hata kwa uchache wa adhabu. Wala wao hawatanusuriwa nafsi zao mbele ya Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura

* 42. Lakini wale ambao Mwenyezi Mungu amewarehemu, miongoni mwa Waumini, Mwenyezi Mungu atawasamehe, na atawapa ruhusa ya uombezi waweze kuwaombea wenginewe. Hakika Yeye ndiye Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye kuwarehemu waja wake Waumini.
Rudi kwenye sura

* 43,44. Hakika mti wa Zaqqumu unao juulikana kwa ubaya wa sura yake, na ukarihi kuula kwake, na harufu yake, ni chakula cha wakosefu wenye madhambi mengi.
Rudi kwenye sura

* 43,44. Hakika mti wa Zaqqumu unao juulikana kwa ubaya wa sura yake, na ukarihi kuula kwake, na harufu yake, ni chakula cha wakosefu wenye madhambi mengi.
Rudi kwenye sura

* 45,46. Utamu wake kama maadeni iliyo yayushwa kwa moto, inatokota matumboni kama yanavyo tokota maji yanayo chemshwa.
Rudi kwenye sura

* 45,46. Utamu wake kama maadeni iliyo yayushwa kwa moto, inatokota matumboni kama yanavyo tokota maji yanayo chemshwa.
Rudi kwenye sura

* 47. Enyi Mazabania wa Jahannamu (Walinzi wa Motoni)! Mkamateni huyu mkosefu, mwenye dhambi, mumtokomeze kwa nguvu na ukali mpaka katikati ya Jahannamu!
Rudi kwenye sura

* 48. Kisha mmiminieni juu ya kichwa chake maji ya moto makali kuzidi kumuadhibu na kumtesa.
Rudi kwenye sura

* 49. Ataambiwa kwa kejeli na maskhara: Onja hii adhabu kali, kwani ati wewe si ndiye mtukufu mwenye nguvu katika kaumu yako, ndiye mheshimiwa unavyo jiona mwenyewe!
Rudi kwenye sura

* 50. Hapana shaka hii adhabu mnayo ipata ni kweli yenye kuwa, na ndiyo mliyo kuwa mkiibisha duniani, na mkiitilia shaka kuwa haiwi.
Rudi kwenye sura

* 51. Hakika hao ambao wamejikinga nafsi zao na maasi kwa kufuata ut'iifu wa Mwenyezi Mungu wapo pahala patukufu ambapo ndani yake wao wanajipatia amani kwa nafsi zao.
Rudi kwenye sura

* 52. Katika mabustani watapo kuwa ndani yake wanastarehe, na chemchem za maji yanayo pita chini yao, kwa sababu ya kuwakirimu wao kwa kutukuza hizo neema zao.
Rudi kwenye sura

* 53. Wakivaa humo hariri nyepesi na nzito kuzidi kuongeza mapambo yao, nao wakielekeana katika majlisi zao, ili kutimiza starehe.
Rudi kwenye sura

* 54. Na pamoja na malipo haya tutawaoza huko Peponi mahurulaini, ambao huwezi kuwachanganyia jicho kwa hadi ya uzuri wao na ukubwa wa macho yao.
Rudi kwenye sura

* 55. Nao huko Peponi watataka kila tunda wanalo litamani, kwa kujua kuwa hayatawaletea vimbizi, wala hayatakwisha, wala hayataadimika.
Rudi kwenye sura

* 56. Huko Peponi hawataonja mauti baada ya mauti ya kwanza waliyo kwisha yaonja duniani ulipo kwisha muda wao wa kuishi, na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni.
Rudi kwenye sura

* 57. Kuhifadhiwa kwao na adhabu ni fadhila na hisani ya Muumba wako. Kuhifadhiwa huko na adhabu na kuingizwa kwao Peponi ndio hadi ya mwisho ya kufuzu kulio kukubwa.
Rudi kwenye sura

* 58. Basi hakika Sisi tumekufanyia wepesi kuisoma Qur'ani na kuifikisha kama ilivyo teremka kwa lugha yako, na lugha yao, ili wapate kuwaidhika, na waiamini, na watende kwa mujibu yaliomo ndani yake.
Rudi kwenye sura

* 59. Basi wewe yangojee hayo yatakayo wafika, na wao pia wanangojea yatakayo kufika wewe na huo wito wako, mambo yakibadilika.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani