Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul H'aaqqah

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1,2. Kiyama ni Tukio litakalo tukia kwa haki, yaani kwa kweli. Ni nini hicho Kiyama kitacho tokea kweli?

* 3. Na kitu gani kitacho kujuvya ukweli wake, na kitacho kupa sura ya kitisho chake na shida zake?
Rudi kwenye sura

* 4. Kina Thamudi na kina A'di walikanusha Kiyama kinacho wagutua walimwengu wote kwa kitisho chake na shida zake.
Rudi kwenye sura

* 5. Ama Thamudi basi walihilikiwa kwa tukio lilio pindukia mipaka yote kwa ukali wake.
Rudi kwenye sura

* 6. Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo ubaridi na mkali,
Rudi kwenye sura

* 7. Mwenyezi Mungu aliwasalitisha nao muda wa masiku saba, na siku nane zilizo fuatana mfululizo, utaona walio patikana na upepo huo wamekuwa maiti kama magogo ya mitende yaliyo kuwa matupu ndani yake. ("Masiku" ni wingi wa "Usiku"; "Siku" wingi wake ni "Siku" vile vile.)
Rudi kwenye sura

* 8. Je! Unamwona yeyote aliye bakia katika hao?
Rudi kwenye sura

* 9. Akaja Firauni, na mataifa mengine yaliyo kufuru kabla yake, na wale jamaa walio acha mwendo wa haki na vitendo vya maumbile wakafanya vitendo vichafu kabisa hata miji yao ikapinduliwa juu chini.
Rudi kwenye sura

* 10. Kila umma katika hawa walimuasi Mtume wa Mola wao Mlezi. Naye Mwenyezi Mungu akawashika kwa kuwaadhibu kwa mshiko ulio zidi ukali.
Rudi kwenye sura

* 11. Maji yalipo zidi ukomo wake, na yakapanda juu ya milima katika tukio la tofani ya Nuhu, Sisi tulikupandisheni, yaani kwa kuwapandisha wazee wenu wa asli, katika safina inayo kwenda baharini.
Rudi kwenye sura

* 12. Ili kulifanya tukio hilo la kuwaokoa Waumini na kuwazamisha makafiri liwe zingatio na mawaidha kwenu, na lihifadhiwe na kila sikio lenye kuhifadhi linalo sikia.
Rudi kwenye sura

* 13,14. Litakapo pulizwa barugumu kwa mpulizo mmoja, na ardhi na milima ikaondolewa pahala ilipo, na ikavunjwa mara moja,

* 15,16. Siku hiyo ndiyo kitashuka cha kushuka, na mbingu zitapasuka kwa kuondoka hukumu zake na sharia zake, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu baada ya kuwa madhubuti zenye nguvu.

* 17. Na Malaika pembezoni mwake, na wapo Malaika wanane siku hiyo watakao beba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi, juu ya Malaika hawa wengine.
Rudi kwenye sura

* 18. Siku hiyo ndio mtaletwa kwa ajili ya kuhisabiwa. Wala haifichikani siri yenu yoyote mliyo kuwa mkiificha.
Rudi kwenye sura

* 19. Ama mwenye kupewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema akiwatangazia furaha yake walio karibu naye: Chukueni msome kitabu changu!
Rudi kwenye sura

* 20. Mimi nilikuwa na yakini tangu duniani kuwa nitapata hisabu yangu, basi nikajitayarisha nafsi yangu kwa mkutano huu.
Rudi kwenye sura

* 21. Basi huyo atakuwa katika maisha yaliyo enea kupendeza.
Rudi kwenye sura

* 22. Katika Bustani ya pahali na daraja ya juu.
Rudi kwenye sura

* 23. Matunda yake yakaribu kwa kuyachuma. (kuyatunda).
Rudi kwenye sura

* 24. Kuleni na mnywe kwa kula na kunywa kusio na karaha, wala maudhi, kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo kwisha vitanguliza katika siku za duniani zilizo pita.
Rudi kwenye sura

* 25,26. Ama mwenye kupewa kitabu chake kwa mkono wake wa kushoto atasema kwa majuto na huzuni: Laiti kuwa sikupewa kitabu changu, wala sikuijua hisabu yangu!

* 27. Laiti kuwa kule kufa niliko kwisha kufa kungeli kuwa ndio kumalizika kwangu kwa mwisho, wala nisingeli fufuliwa tena!
Rudi kwenye sura

* 28,29. Hapana chochote nilicho kimiliki duniani kilicho nifaa. Uzima wangu umenipotea, na nguvu zangu zimenitoka.

* 30,31,32. Wataambiwa walinzi wa Jahannamu: Mshikeni, na mfungeni mikono yake kwenye shingo yake. Kisha msimtie popote ila ndani ya Moto wa Jahannamu, kisha mfungeni kwenye mnyororo mrefu kabisa.

* 33,34. Hakika huyo alikuwa hamsadiki Mwenyezi Mungu Mtukufu, wala hamhimizi yoyote kuwalisha masikini.

* 35,36,37. Basi hii leo huyu kafiri hana jamaa wa kumtetea, wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni, ambao kwa hakika ni mchanganyiko wa damu na usaha. Hawakili chakula hicho ila wakosefu walio kusudia kufanya maasi yao, na wakakamia kuendelea nayo.

* 38,39,40. Basi naapa kwa mnavyo viona katika vinavyo onekana, na msivyo viona katika ulimwengu wa ghaibu, kwamba hakika Qur'ani bila ya shaka inatoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ulimi wa Mjumbe mwenye cheo cha juu.

* 41. Wala Qur'ani si maneno ya mtunga mashairi kama mnavyo dai. Ama nyinyi ni chache mno imani yenu ya kuwa Qur'ani inatoka kwa Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura

* 42. Wala Qur'ani haisemi kwa maneno ya kumunyia munyia kama wanenavyo makuhani mlio wazoea. Ni uchache mno kukumbuka kwenu na kuzingatia khitilafu zilioko baina ya Qur'ani na maneno ya makuhani.
Rudi kwenye sura

* 43. Hii ni uteremsho unao toka kwa Mwenye kuwaangalia walimwengu wote kwa kuwaumba na kuwalea.
Rudi kwenye sura

* 44,45,46. Na lau kuwa angeli dai kitu chochote ambacho tusicho kisema basi bila ya shaka tungeli mshika akitoe kama mtu anavyo mkamata mtu kwa mkono wa kulia akammaliza hapo hapo. Kisha bila ya shaka tungeli mkata mshipa wake wa moyo, afe saa ile ile. (Biblia inasema katika Kumbukumbu la Torati 18.20 "Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.")

* 47. Na hapana yeyote katika nyinyi, hata ange kuwa na nguvu namna gani, angeli weza kuzuia adhabu yetu isimfikilie.
Rudi kwenye sura

* 48. Na hakika Qur'ani ni mawaidha kwa wanao fuata amri za Mwenyezi Mungu, na wanaepuka makatazo yake.
Rudi kwenye sura

* 49. Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba kati yenu wapo wanao ikanusha Qur'ani.
Rudi kwenye sura

* 50. Na kwamba hakika hiyo bila ya shaka ni sababu ya majuto ya wanao ikataa, wakati watapo iona adhabu yao, na neema za wenye kusadiki.
Rudi kwenye sura

* 51. Na hakika Qur'ani bila ya shaka ni Haki iliyo thibiti, isiyo na shaka yoyote.
Rudi kwenye sura

* 52. Basi mtakase Mola wako Mlezi, na dumisha kudhukuru jina lake.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani