Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Annabaa

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Wanaulizana nini hao makafiri?
Rudi kwenye sura

* 2,3. Wanaulizana khabari kubwa, khabari ya kufufuliwa, ambayo wao wamezama ndani yake kukhitalifiana baina ya wenye kuikataa na wenye kuitilia shaka.
Rudi kwenye sura

* 2,3. Wanaulizana khabari kubwa, khabari ya kufufuliwa, ambayo wao wamezama ndani yake kukhitalifiana baina ya wenye kuikataa na wenye kuitilia shaka.
Rudi kwenye sura

* 4. Kuwazuia kuulizana huko wanaambiwa kuwa watakuja ujua ukweli wa mambo hapo watapo ona kufufuliwa kumetokea khasa.
Rudi kwenye sura

* 5. Tena kuwazuia, watakuja jua itapo wateremkia adhabu.
Rudi kwenye sura

* 6. Kwani wao hawaoni Ishara za uweza wetu kwamba Sisi tumeifanya ardhi imetandikwa upatikane utulivu juu yake na iwezekane kutembea juu yake?
Rudi kwenye sura

* 7. Na tukaifanya milima ni vigingi vya ardhi vya kuituliza? Sehemu ya gamba gumu lilio juu ya ardhi linfikilia kiasi ya kilomita 60 unene wake, na inazidi mikunjo, mifimbi, inapanda juu kuwa milima, na huteremka chini kuwa ni vina vya bahari; na hiyo hulingana kwa sababu ya uzito unao patikana kutokana na milima. Na kulingana huko hakuharibiki ila kwa kubugunyika, kwani gamba kavu la ardhi linazuiliwa na milima, kama vigingi vinavyo zuilia khema. (Rejea Maoni ya Wataalamu juu ya Aya 7 ya Surat Qaf).
Rudi kwenye sura

* 8. Na tukakuumbeni kwa jozi, wanaume na wanawake?
Rudi kwenye sura

* 9. Na tukafanya kulala kwenu ni mapumziko ya machofu ya kazi? Kulala usingizi ni kusita nishat'i ya sehemu ya ubongo yenye kutambua na kuwa macho. Yaani gamba la ubongo, au kupunguka nishat'i yake kwa wingi, ukilinganisha na daraja za nishat'i ya sehemu za viungo vilio baki. Na kwa hivyo kunapunguka nguvu na joto la mwili, tena mwili hapo wakati wa usingizi hupata kutua na kupumzika baada ya kuhangaika viungo au akili au vyote viwili. Basi kazi za kimwili zote hupunguka isipo kuwa kazi za kusaga chakula, na kupitisha mkojo katika mafigo, na kutoka majasho katika ngozi, kwani yakisita hayo hupatikana madhara juu ya maisha ya mtu. Ama kuvuta pumzi huko nako hupunguka, na huwa ni kwa ndani zaidi, na huwa kwa kifua zaidi kuliko kwa tumbo. Na mpigo wa mishipa hupungua kasi kwa kunavyo tokana na moyo, na hudhoofika mkazano wa musulo (muscular tension), na kwa hivyo huwa taabu kupata harakati za kinyume. Na yote haya ni ili binaadamu apate kupumzika wakati wa kulala.
Rudi kwenye sura

* 10. Na tumeufanya usiku ni sitara kwenu kwa kiza kinacho kufunikeni.
Rudi kwenye sura

* 11. Na tumeufanya mchana ni wakati wa kuhangaika kwenu kutafuta cha kukusaidieni katika maisha yenu.
Rudi kwenye sura

* 12. Na tumesimamisha juu yenu mbingu saba zenye nguvu madhubuti.
Rudi kwenye sura

* 13. Na Sisi tumeliumba jua lenye mwangaza na linalo waka. Makusudio ya Assiraj Alwahhaaj, Taa yenye mwanga na joto, ni Jua. Na hayo kama ilivyo thibiti katika sayansi kuwa daraja ya joto la uso wake inafika daraja 6000. Ama kati yake daraja yake inazidi daraja 30 milioni kwa sababu ya mdidimizo mkubwa unao patikana juu ya madda ziliomo ndani yake. Na jua linatoa nishat'i hizi zifuatazo: 9 katika 100 ya miale ya Ultraviolet rays, 46 katika 100 ya miale ya mwangaza, 45 katika 100 miale ya joto, au Infra red rays. Na kwa hivyo hii Aya tukufu imeliita kuwa ni Taa yenye mwangaza na joto.
Rudi kwenye sura

* 14. Na tumeteremsha kutokana na mawingu yaliyo karibia kunyesha maji yenye kumiminika kwa nguvu. Mvua ndio kitu pekee kinacho toka asli yake maji matamu katika ardhi. Na asli ya mvua ni kukusanyika vijisehemu vya maji yanayo panda kutoka baharini, na maziwa na mito, yakakusanyika kama mawingu na yakageuka chembe za mvua au vipande vya barafu, na khatimaye yakaanguka kwa sura ya mvua au theluji.
Rudi kwenye sura

* 15. Ili tutoe kwa maji haya nafaka na mimea kuwa ni chakula kwa ajili ya watu na wanyama.
Rudi kwenye sura

* 16. Na mabustani yenye miti iliyo fungamana na matawi yake yameingiliana.
Rudi kwenye sura

* 17. Hakika siku ya uamuzi baina ya viumbe imewekewa miadi ilio kwisha kadiriwa kwa ajili ya kufufuliwa.
Rudi kwenye sura

* 18. Siku litakapo pulizwa barugumu na kufufuliwa watu, mtakuja kwenye mkutano makundi kwa makundi.
Rudi kwenye sura

* 19. Na mbingu zitapasuliwa kila upande hata zitakuwa ni milango milango.
Rudi kwenye sura

* 20. Na milima itaondolewa baada ya kung'olewa mwahala mwake, na kuvurugwa, ikawa unaiona kama sura ya milima na hali hiyo ni kifusi tu kilicho rindikwa, kama uonavyo mangati, sarabi, unaona kama sura ya maji nayo si maji.
Rudi kwenye sura

* 21. Hakika Jahannamu imekuwa kama ni kitu kinacho ngojea, walinzi wake wanawangojea watu watakao kuja kuingia.
Rudi kwenye sura

* 22. Yawe ni marejeo na mafikio kwa wenye kupindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura

* 23. Watakaa humo dahari baada ya dahari.
Rudi kwenye sura

* 24. Hawataonja humo hata chembe ya upepo wa kuburudisha joto lake, wala kinywaji cha kupoza kiu chao.
Rudi kwenye sura

* 25. Lakini watakunywa maji yalio pita ukomo kwa umoto wake, na usaha unao miminika kutokana na ngozi za watu wa Motoni.
Rudi kwenye sura

* 26. Malipo ya kuwafikiana na vitendo vyao viovu.
Rudi kwenye sura

* 27. Kwani hao hawakutaraji kuwa itakuwapo kuhisabiwa, hata watende ya kuwaokoa humo.
Rudi kwenye sura

* 28. Wakazikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu zenye kuthibitisha kufufuliwa kwa mkadhibisho mkali.
Rudi kwenye sura

* 29. Na kila kitu tumekidhibiti kwa kukiandika.
Rudi kwenye sura

* 30. Basi onjeni, wala hampati kwetu ila kuzidishiwa adhabu tu.
Rudi kwenye sura

* 31. Hakika wenye kumcha Mola wao Mlezi watapata kuokoka na adhabu, na wataipata Pepo,
Rudi kwenye sura

* 32. Na mabustani yenye matunda, na mizabibu mizuri,
Rudi kwenye sura

* 33. Na wanawari walio watipwatipwa wa hirimu yao,
Rudi kwenye sura

* 34. Na bilauri safi zilizo jaa pomoni,
Rudi kwenye sura

* 35. Hawasikii huko Peponi upuuzi wala uwongo.
Rudi kwenye sura

* 36. Ni malipo kutokana na Mola wako Mlezi, kwa fadhila yake na ihsani ya kutosha.
Rudi kwenye sura

* 37. Mola Mlezi wa mbinguni na duniani na vilio baina yao, ambaye rehema yake imeenea juu ya kila kitu. Hapana yeyote mwenye madaraka ya kusema mbele yake.
Rudi kwenye sura

* 38. Siku atakapo simama Jibrili na Malaika walio teuliwa nao wamenyenyekea, hasemi mmoja wao ila akipewa idhini na Arrahman, Mwingi wa rehema, kuwa aseme, naye atasema lilio sawa tu.
Rudi kwenye sura

* 39. Hiyo ndiyo siku isiyo na shaka. Basi atakaye na ashike njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi arejee kwa Imani, na a'mali njema.
Rudi kwenye sura

* 40. Hakika Sisi tumekuhadharisheni na adhabu itakayo tokea karibu, siku atakapo angalia mtu vitendo vyake vilivyo tangulizwa na mikono yake, na atakapo sema kafiri kwa kutamani kuokoka: Laiti ningeli bakia udongo baada ya kufa, nisifufuliwe wala nisihisabiwe!
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani