Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul A'basa

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Uso wake ulitaghayari kwa kuchukia na akageuka,
Rudi kwenye sura

* 2. Kwa sababu kamjia kipofu anamuuliza khabari ya Dini yake.
Rudi kwenye sura

* 3. Na wewe unajuaje, pengine huyo kipofu atatakasika kwa atayo yapata kwako,
Rudi kwenye sura

* 4. Au atawaidhika na mawaidha yamfae.
Rudi kwenye sura

* 5,6. Ama yule anaye jiona ametosheka kwa mali yake na nguvu zake, wewe ndio unamkabili na unamshughulikia kumfikishia wito wako.
Rudi kwenye sura

* 5,6. Ama yule anaye jiona ametosheka kwa mali yake na nguvu zake, wewe ndio unamkabili na unamshughulikia kumfikishia wito wako.
Rudi kwenye sura

* 7. Na wewe una lawama gani ikiwa yeye hakutakasika kwa Imani?
Rudi kwenye sura

* 8,9,10. Ama anaye kukimbilia kutafuta ilimu na uwongofu, naye anamkhofu Mwenyezi Mungu wewe unampuuza.

* 11. Hakika Aya hizi ni mawaidha.
Rudi kwenye sura

* 12. Mwenye kutaka atawaidhika kwa Qur'ani.
Rudi kwenye sura

* 13. Nayo Qur'ani imo katika kurasa zilizo tukuzwa kwa Mwenyezi Mungu,
Rudi kwenye sura

* 14. Zina cheo cha juu, na pahala palipo tukuka, zimetakasika na kila upungufu.
Rudi kwenye sura

* 15. Katika mikono ya Malaika ambao Mwenyezi Mungu amewafanya ndio mabalozi baina yake na Mitume wake;
Rudi kwenye sura

* 16. Walio bora, wema.
Rudi kwenye sura

* 17. Ameangamia mwanaadamu! Nini kilicho mfanya akufuru na hali Mwenyezi Mungu amemfanyia hisani zote hizi?
Rudi kwenye sura

* 18. Hakumbuki yeye kaumbwa kutokana na nini?
Rudi kwenye sura

*19. Kutokana na maji ya kudharauliwa Yeye Mwenyezi Mungu alimwanzisha kumuumba akamjaalia apitie daraja mbali mbali za kukua.
Rudi kwenye sura

* 20. Kisha akamfanyia nyepesi njia ya kufikia Imani, na akamfunza njia hiyo.
Rudi kwenye sura

* 21. Kisha akamfisha na akamtukuza kwa kumtia kaburini.
Rudi kwenye sura

* 22. Na tena akipenda atamhuisha baada ya kufa kwake.
Rudi kwenye sura

* 23. Ni kweli mwanaadamu, juu ya kuwa umri wake mrefu duniani, hakutimiza aliyo amrishwa na Mwenyezi Mungu katika mambo ya Imani na ut'iifu.
Rudi kwenye sura

* 24. Hebu mtu na aangalie shani ya chakula chake - vipi tulivyo kipanga na kumsahilishia!
Rudi kwenye sura

* 25. Ni Sisi tumeiteremsha mvua kutoka mbinguni, ikateremka.
Rudi kwenye sura

* 26. Tena tukaipasua pasua ardhi kwa ajili ya mimea.
Rudi kwenye sura

* 27. Tukaotesha humo nafaka ambazo watu huzila na huweka akiba.
Rudi kwenye sura

* 28. Na mizabibu na mimea ya majani inayo liwa mibichi.
Rudi kwenye sura

* 29. Na mizaituni mizuri, na mitende yenye kuzaa,
Rudi kwenye sura

* 30. Na mabustani yaliyo songamana matawi ya miti yake,
Rudi kwenye sura

* 31. Na matunda ya kustaladhi nayo, na malisha ya kula nyama hoa (mifugo).
Rudi kwenye sura

* 32. Tumeotesha yote hayo kwa ajili ya faida yenu na wanyama wenu wa kufuga.
Rudi kwenye sura

* 33. Basi utakapo kuja ukelele wa Kiyama utakao tia uziwi masikio,
Rudi kwenye sura

* 34,35,36. Siku mtu atakapo mkimbia ndugu yake, na mama yake, na baba yake, na mkewe, na wanawe!

* 37. Kila mmojapo katika hawa atakuwa na jambo lake la kumshughulisha!
Rudi kwenye sura

* 38,39. Zipo nyuso siku hii zenye mwangaza, zenye kung'ara na kufurahi kwa neema za Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura

* 38,39. Zipo nyuso siku hii zenye mwangaza, zenye kung'ara na kufurahi kwa neema za Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura

* 40. Na nyuso nyengine siku hii zina vumbi zimesawijika.
Rudi kwenye sura

* 41. Zimegubikwa na kiza na weusi.
Rudi kwenye sura

* 42. Wenye nyuso hizi ni makafiri wapotovu, ambao walio kuwa hawabali maasi waliyo kuwa wakiyatenda.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani