Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Mut'affifiin

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1,2,3. Wataangamia wanao punja, ambao wakijipimia wenyewe kwa watu hujitwalia ya kutosha na kuzidi, na wakiwapimia watu kwa vipimo au mizani huwapunguzia haki yao wanayo stahiki, kwa dhulma!

* 4,5. Hivyo haiwapitikii katika akili zao hawa wanao punja wenzao kwamba watakuja fufuliwa katika siku ya vitisho vikuu?
Rudi kwenye sura

* 4,5. Hivyo haiwapitikii katika akili zao hawa wanao punja wenzao kwamba watakuja fufuliwa katika siku ya vitisho vikuu?
Rudi kwenye sura

* 6. Siku watapo simama watu kwa amri ya Mola Mlezi wa walimwengu wote na hukumu yake?
Rudi kwenye sura

* 7. Wacheni kupunja, na kughafilika na kufufuliwa! Kwani hakika waliyo andikiwa wakosefu katika a'mali zao mbovu, bila ya shaka yamo katika Sijjin.
Rudi kwenye sura

* 8. Na nini kitakujuvya nini hiyo Sijjin?
Rudi kwenye sura

* 9. Hicho ni Kitabu kilicho pigwa mistari baina ya maandishi yake.
Rudi kwenye sura

* 10. Wataangamia wanao kadhibisha siku itapo kuwa kufufuliwa na kuhisabiwa.
Rudi kwenye sura

* 11. Ambao wanaikanusha Siku ya Malipo.
Rudi kwenye sura

* 12. Na wala haikanushi Siku ya Malipo ila kila mwenye kupindukia mipaka mwingi wa madhambi.
Rudi kwenye sura

* 13. Na akisomewa Aya za Mwenyezi Mungu zenye kutaja kuwepo malipo husema: Huo ni uwongo wa walio tangulia!
Rudi kwenye sura

* 14. Ewe uliye kiuka mipaka! Wacha kauli hiyo potovu. Bali nyoyo za wenye kupindukia mipaka imegubikwa na ukafiri na maasi waliyo yatenda.
Rudi kwenye sura

* 15. Hakika ni kweli kuwa hao wanao kadhibisha watazuiliwa siku hiyo rehema ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ya maasi waliyo yachuma.
Rudi kwenye sura

* 16. Kisha hakika hao bila ya shaka wataingia Motoni.
Rudi kwenye sura

* 17. Kisha wataambiwa kwa kuwakebehi: Hii basi ndiyo adhabu inayo kuteremkieni ambayo mlikuwa mkiikanusha duniani!
Rudi kwenye sura

* 18. Ni hakika kuwa vitendo vya watu wema bila ya shaka vimeandikwa katika I'liyyin.
Rudi kwenye sura

* 19. Na nini cha kukujuvya nini I'liyyin?
Rudi kwenye sura

* 20,21. Hicho ni Kitabu kilicho andikwa wazi maandishi yake, wanakihudhurisha na kukihifadhi Malaika walio kurubishwa.
Rudi kwenye sura

* 20,21. Hicho ni Kitabu kilicho andikwa wazi maandishi yake, wanakihudhurisha na kukihifadhi Malaika walio kurubishwa.
Rudi kwenye sura

* 22,23. Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema za Peponi, juu ya viti vya enzi, wakiziangalia neema na ukarimu alio wakirimu Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura

* 22,23. Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema za Peponi, juu ya viti vya enzi, wakiziangalia neema na ukarimu alio wakirimu Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura

* 24. Utaona katika nyuso zao uchangamfu na mng'aro wa neema.
Rudi kwenye sura

* 25,26. Wakinyweshwa kinywaji safi kilicho hifadhiwa; kuhifadhiwa huko hakukuzidisha ila uzuri wake. Na kupata neema hizo, basi, na washindanie wanao shindana.
Rudi kwenye sura

* 25,26. Wakinyweshwa kinywaji safi kilicho hifadhiwa; kuhifadhiwa huko hakukuzidisha ila uzuri wake. Na kupata neema hizo, basi, na washindanie wanao shindana.
Rudi kwenye sura

* 27,28. Cha kuchanganyia kinywaji hicho ni maji ya Tasniim ya Peponi, nayo ni chemchem wanao inywa walio kurubishwa si wengineo, katika watu wa Peponi.
Rudi kwenye sura

* 27,28. Cha kuchanganyia kinywaji hicho ni maji ya Tasniim ya Peponi, nayo ni chemchem wanao inywa walio kurubishwa si wengineo, katika watu wa Peponi.
Rudi kwenye sura

* 29. Wale walio kuwa wakibeba madhambi kuipingia Dini walikuwa wakiwacheka kuwakejeli Waumini duniani.
Rudi kwenye sura

* 30. Na wakipita Waumini mbele yao basi wao hukonyezana kwa kuwabeza.
Rudi kwenye sura

* 31. Na hao wakosefu wakirejea kwa ahali zao hurejea kwa furaha na kuona ladha kwa vile kuwakejeli Waumini.
Rudi kwenye sura

* 32,33. Na wakiwaona Waumini husema: Ama hakika hawa wamepotea kweli kwa kumuamini Muhammad. Wala hao wakosefu hawakutumwa wawe wa kuwahukumu Waumini kwa kuwaongoza au kuwapoteza, wala kuwa ni walinzi wa vitendo vyao.

* 34. Basi Siku ya Malipo walio amini watakuwa ndio wa kuwacheka hao makafiri kwa kuwalipizia kile kicheko chao na kejeli yao ya duniani.
Rudi kwenye sura

* 35. Ilhali wako juu ya vitanda na matakia watakuwa Waumini wakiziangalia neema za Mwenyezi Mungu alizo wapa.
Rudi kwenye sura

* 36. Je! Makafiri watalipwa huko Akhera kwa waliyo yatenda duniani?
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani