Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Aa'laq......

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Litakase jina la Mola wako Mlezi lilio tukufu na kila kitu kisicho kuwa kinaelekeana nalo.
Rudi kwenye sura

* 2. Aliye umba kila kitu, na akajaalia uumbaji wote sawa sawa katika hukumu na kupangana.
Rudi kwenye sura

* 3. Na akakadiria kwa kila kitu kwa mujibu wa maslaha yake, na akakiongoza.
Rudi kwenye sura

* 4. Na ambaye akatoa kwenye ardhi mimea namna mbali mbali ya kuwalisha wanyama.
Rudi kwenye sura

* 5. Na akaifanya mimea hiyo baada ya kuwa kijani imestawi, ikakauka na imekuwa myeusi!
Rudi kwenye sura

* 6. Ewe Muhammad! Sisi tutakujaalia uwe ni mwenye kuisoma Qur'ani kwa ufunuo kutoka kwetu, na wala hutosahau utacho kihifadhi.
Rudi kwenye sura

* 7. Isipo kuwa anacho taka Mwenyezi Mungu ukisahau, kwani hakika Yeye Mtukufu anayajua wanayo yadhihirisha waja wake na wanayo yaficha, ikiwa maneno au vitendo.
Rudi kwenye sura

* 8. Na tutakuwezesha kupita njia ya kufikilia kwa wepesi mambo yako yote.
Rudi kwenye sura

* 9. Basi wakumbushe watu ikiwa kukumbusha kutaleta manufaa, kwani inavyo faa ndio kuwanafiisha.
Rudi kwenye sura

* 10. Watanafiika kwa ukumbusho wako wanao mwogopa Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura

* 11. Na atajitenga na ukumbusho mpotovu anaye shikilia kufanya inda na ukafiri.
Rudi kwenye sura

* 12. Ambaye ataingia kwenye Moto mkubwa ulio andaliwa kuwa ndio malipo yake.
Rudi kwenye sura

* 13. Tena hatokufa huko Motoni akapumzika kwa kifo, wala hawi hai kwa uhai wa kustarehe nao.
Rudi kwenye sura

* 14. Hakika amefuzu mwenye kujisafisha na ukafiri na maasi.
Rudi kwenye sura

* 15. Na akalikumbuka jina la Muumba wake kwa moyo wake na ulimi wake, na akasali kwa unyenyekevu kama itakikanavyo.
Rudi kwenye sura

* 16. Bali nyinyi hamfanyi hayo yanayo pelekea kufanikiwa, lakini katika hima zenu mnatanguliza maisha ya duniani kuliko ya Akhera.
Rudi kwenye sura

* 17. Na Akhera ni bora kuliko dunia, kwa usafi wa neema zake, na ni yenye kubaki na kudumu zaidi.
Rudi kwenye sura

* 18,19. Hakika haya yote yaliyo tajwa katika Sura hii bila ya shaka yamethibitishwa katika Vitabu vya zamani, Vitabu vya Ibrahimu na Musa; kwani haya yamewafikiana na mafunzo ya dini zote na yamesajiliwa katika Vitabu vya mbinguni.
Rudi kwenye sura

* 18,19. Hakika haya yote yaliyo tajwa katika Sura hii bila ya shaka yamethibitishwa katika Vitabu vya zamani, Vitabu vya Ibrahimu na Musa; kwani haya yamewafikiana na mafunzo ya dini zote na yamesajiliwa katika Vitabu vya mbinguni.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani