Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Ghaashiyah

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Je! Ewe Muhammad! Imepata kukujia hadithi ya Kiyama ambacho kwa vitisho vyake kitawafanya watu wazimie?
Rudi kwenye sura

* 2,3. Siku hiyo ya Kiyama zitakuwepo nyuso zimedhalilika, zimechoka, taabani kwa shughuli na mashaka ya Motoni,
Rudi kwenye sura

* 2,3. Siku hiyo ya Kiyama zitakuwepo nyuso zimedhalilika, zimechoka, taabani kwa shughuli na mashaka ya Motoni,
Rudi kwenye sura

* 4. Zinaingia kwenye Moto unao waka kwa nguvu!
Rudi kwenye sura

* 5. Wananywesha maji yanayo toka kwenye chemchem inayo tokota.
Rudi kwenye sura

* 6. Hawana chakula ila chakula kiovu kabisa, anaadhibika mwenye kukila.
Rudi kwenye sura

* 7. Hakileti nafuu yoyote katika mwili, wala hakiondoi njaa.
Rudi kwenye sura

* 8,9,10. Na pia zitakuwapo nyuso zenye kutoa nuru Siku ya Kiyama, kwa malipo ya vitendo vyao walivyo fanya duniani. Hao watakuwa wameridhia kwa watayo yapata katika Pepo iliyo juu kwa pahala na cheo.
Rudi kwenye sura

* 8,9,10. Na pia zitakuwapo nyuso zenye kutoa nuru Siku ya Kiyama, kwa malipo ya vitendo vyao walivyo fanya duniani. Hao watakuwa wameridhia kwa watayo yapata katika Pepo iliyo juu kwa pahala na cheo.
Rudi kwenye sura

* 8,9,10. Na pia zitakuwapo nyuso zenye kutoa nuru Siku ya Kiyama, kwa malipo ya vitendo vyao walivyo fanya duniani. Hao watakuwa wameridhia kwa watayo yapata katika Pepo iliyo juu kwa pahala na cheo.
Rudi kwenye sura

* 11,12. Humo halisikilizani neno la upuuzi. Humo mna chemchem isiyo katika.
Rudi kwenye sura

* 11,12. Humo halisikilizani neno la upuuzi. Humo mna chemchem isiyo katika.
Rudi kwenye sura

* 13. Humo vitakuwamo viti vilivyo nyanyuliwa kwa cheo na kwa hakika, kama ni ziada ya neema.
Rudi kwenye sura

* 14. Na bilauri (gilasi) zilio wekwa mbele yao,
Rudi kwenye sura

* 15. Na mito na matakia yalio pangwa kwa safu.
Rudi kwenye sura

* 16. Na mazulia mengi yaliyo tandazwa hapo barazani.
Rudi kwenye sura

* 17. Je! Wanapuuza kuzingatia Ishara, basi hebu na wamuangalie ngamia, vipi alivyo umbwa kwa namna ya peke yake kwa uweza wa Mwenyezi Mungu? Katika kuumbwa ngamia zipo Ishara na miujiza yenye kuthibitisha uweza wa Mwenyezi Mungu ambao yafaa wenye kuzingatia wauzingatie. Katika sifa zake zinazo onekana ni hizo zinazo mfanya kweli awe ni jahazi ya jangwani. Macho yake yamenyanyuka yako juu ya kichwa, na yanaelekea nyuma, na tena yana kope za kuyakinga na mchanga na vumbi. Kadhaalika pua na masikio yamefunikwa na nywele kwa sababu hiyo hiyo. Ukivuma mdharuba wa mchanga pua hufunga na masikio hupinda, juu ya kuwa tokea hapo ni madogo na si yenye kudhihiri mno, ukilinganisha na mwili wake. Ama miguu ni mirefu kwa kusaidia wepesi wa kwenda, pamoja na kunasibiana na urefu wa shingo yake. Ama nyayo ni pana zimetanda kwa ukhafifu ili kumwezesha ngamia kwenda juu ya mchanga laini. Na ngamia kwa jumla chini ya kifua chake na chini ya viungo vyake vya miguu pana kama mito inayo msaidia ngamia kupiga magoti na kulala juu ya ardhi ngumu na imoto, kama vile vile pande zote mbili za mkia wake yapo manyoya marefu ya kumlinda sehemu zake za nyuma na vitu vya kumuudhi. Ama vipawa alivyo pewa ngamia kwa ajili ya kazi yake ni vya ajabu zaidi. Siku za baridi hahitajii maji, bali anaweza asinywe maji muda wa miezi miwili mfululizo, ikiwa chakula kimajimaji na laini, au wiki mbili ikiwa kikavu. Pia anaweza kustahamili kiu hata siku za joto muda wa wiki au wiki mbili, na hupungua muda huo zaidi ya thuluthi mbili ya uzito wake. Na anapo yapata maji huyagugumia maji kwa wingi mno arejeshe uzito wake wa zamani kwa dakika chache tu. Na ngamia hayarimbiki maji katika tumbo lake kama ilivyo kuwa ikidhaniwa, bali katika mfumo wa mwili wake, na huyatumia kwa uangalifu mkubwa mno. Kwa hivyo kabisa hapumui kama anavyo pumua mbwa, mathalan, wala hatoi pumzi kwa mdomo wake, wala hatoki majasho kwenye ngozi yake ila kwa uchache kabisa. Na hayo ni kuwa daraja ya joto ya mwili wake inakuwa chini sana asubuhi mapema. Kisha hupanda kidogo kidogo zaidi ya daraja sita kabla ya kuhitajia kuipoza kwa jasho na kutoa mvuke. Na juu ya maji mengi mno yanayo toka katika mwili baada ya kiu kirefu kwa hakika uzito wa damu hauathiriki ila kwa kiasi tu, na kwa hivyo kiu hakina athari kitu juu yake. Na imethibiti mafuta ya nunudu yaliyo khaziniwa kwa ajili ya nishat'i yanamkifu kumkinga na machungu ya njaa, lakini hayamfaidishi sana kwa haja ya maji ambayo ni lazima kwa mwili wake. Na bado wataalamu wangali wanagundua mapya katika ngamia kila wakichungua ya kuhakikisha hadhi aliyo mpa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa atazamwe katika uumbaji wake wa muujiza.
Rudi kwenye sura

* 18. Na waizingatie mbingu wanayo iona daima, vipi ilivyo nyanyuliwa huko mbali bila ya nguzo!
Rudi kwenye sura

* 19. Na milima wanayo ikwea mpaka wakafika vileleni kwake, vipi ilivyo simamishwa kwa urefu, imeshikamana na ardhi, haiyumbi wala haitikisiki! Mara nyingi katika Qur'ani tukufu inatajwa kuwa ardhi "imekunjuliwa". Na makusudio ya hayo ni kuwa ardhi ijapo kuwa ni duara kama mpira kwa sura yake, lakini inavyo onekana kwa watazamao ni kuwa imekunjuliwa. Na haya hayagongani na yaliyo thibitishwa na sayansi katika jambo lolote.
Rudi kwenye sura

* 20. Na ardhi wanayo ikalia na kuyendea juu yake, vipi ilivyo kunjuliwa na kutandazwa!
Rudi kwenye sura

* 21,22 Basi kumbusha kwa wito wako, kwani kazi yako muhimu ni kufikisha wito tu. Hukuwa mtawala juu yao.
Rudi kwenye sura

* 21,22 Basi kumbusha kwa wito wako, kwani kazi yako muhimu ni kufikisha wito tu. Hukuwa mtawala juu yao.
Rudi kwenye sura

* 23,24 Lakini miongoni mwao ataye puuza na akakataa, basi Mwenyezi Mungu atampa adhabu iliyo kubwa kabisa, isiyo kuwa na ya kuipita.
Rudi kwenye sura

* 23,24 Lakini miongoni mwao ataye puuza na akakataa, basi Mwenyezi Mungu atampa adhabu iliyo kubwa kabisa, isiyo kuwa na ya kuipita.
Rudi kwenye sura

* 25. Hakika ni kwetu Sisi marejeo yao kwa kifo na kufufuliwa, wala hapana penginepo isipo kuwa kwetu.
Rudi kwenye sura

* 26. Tena ni juu yetu Sisi tu peke yetu kuwahisabia na kuwalipa.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani