Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Fajr

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Naapa kwa mwangaza wa asubuhi unapo ufukuza usiku.
Rudi kwenye sura

* 2. Na kwa masiku kumi yaliyo tukuzwa na Mwenyezi Mungu. (Na hayo ni masiku kumi ya mwanzo wa Mwezi wa Alhaj, Mfungo Tatu).
Rudi kwenye sura

* 3. Na shafi' yaani hisabu inayo gawika kwa mbili, kama 4, 6, 8 n.k. na witri, yaani isiyo gawika kwa mbili, kama 1, 3, 5 n.k. katika kila kitu.
Rudi kwenye sura

* 4. Na kwa usiku unapo pita kwa kwenda ulimwengu kwa namna ya ajabu.
Rudi kwenye sura

* 5. Je! Katika vitu vilivyo tajwa vinavyo onekana kwa akili hapana kiapo cha kukinaisha?
Rudi kwenye sura

* 6,7. Kwani hujui jinsi Mola wako Mlezi alivyo wateremshia adhabu yake kaumu ya Hud, watu wa Iram wenye majengo marefu?
Rudi kwenye sura

* 6,7. Kwani hujui jinsi Mola wako Mlezi alivyo wateremshia adhabu yake kaumu ya Hud, watu wa Iram wenye majengo marefu?
Rudi kwenye sura

* 8. Ambayo haikupata kujengwa mfano wake kwa umadhubuti na ujenzi katika nchi.
Rudi kwenye sura

* 9. Kwani hukujua jinsi Mola wako Mlezi alivyo teremsha adhabu yake kwa Thamudi, kaumu ya Saleh, walio chonga majabali kujengea nyumba zao huko bondeni?
Rudi kwenye sura

* 10. Au kwani hukujua vipi Mola wako Mlezi alivyo wateremshia adhabu yake Firauni mwenye majeshi yaliyo upa nguvu ufalme wake kama vigingi vinavyo simamisha makhema?
Rudi kwenye sura

* 11. Ambao walipita mipaka katika nchi?
Rudi kwenye sura

* 12. Na wakazidisha kufanya uharibifu kwa ukafiri na udhalimu?
Rudi kwenye sura

* 13. Basi Mola wako Mlezi aliwateremshia adhabu kali ya kuwaunguza.
Rudi kwenye sura

* 14. Hakika Mola wako Mlezi anaviangalia vitendo vya watu, na anawahisabia, na atakuja kuwalipa kwavyo.
Rudi kwenye sura

* 15. Ama mtu akijaribiwa na Mola wake Mlezi na akamkirimu, na akamneemesha kwa mali na cheo na nguvu, basi husema kwa kughurika na hayo: Mola wangu Mlezi amenitukuza kwa kuwa ninastahiki haya!
Rudi kwenye sura

* 16. Na pindi Mola wake Mlezi akimjaribu mtu kwa kumdhikisha riziki, basi hughafilika na hikima ya hayo na husema: Mola wangu Mlezi kanidhalilisha!
Rudi kwenye sura

* 17. Wacheni mtindo huo! Mambo siyo hayo kama msemavyo; bali nyinyi hamumkirimu yatima;
Rudi kwenye sura

* 18. Wala hamhimizani kuwalisha masikini;
Rudi kwenye sura

* 19. Na mnakula mali ya urithi kwa pupa, hamchagui linalo faa na lisilo faa.
Rudi kwenye sura

* 20. Na mnayapenda mali mno, yanayo kupelekeeni kupapatika katika kuyakusanya na ubakhili wa kuyatumia.
Rudi kwenye sura

* 21. Wacheni vitendo hivyo! Kwani inakungojeeni siku itapo lazwa ardhi iwe sawa sawa,
Rudi kwenye sura

* 22. Na aje Mola wako Mlezi kama anavyo stahiki kuja kwake Subhanahu na Malaika waje kwa safu safu;
Rudi kwenye sura

* 23. Na siku hiyo iletwe Jahannamu, nyumba ya adhabu, siku hiyo yatapo tokea hayo mwanaadamu atakumbuka aliyo yaharibu - lakini wapi! Kukumbuka huko kumfae nini, na wakati umekwisha pita?
Rudi kwenye sura

* 24. Atasema kwa majuto: Laiti ningeli jitangulizia katika dunia vitendo vyema vya kunifaa katika maisha ya Akhera!
Rudi kwenye sura

* 25,26. Siku hiyo zitakuwa hali hizi, haadhibu mtu kama adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala hafungi mtu kama afungavyo Yeye.
Rudi kwenye sura

* 25,26. Siku hiyo zitakuwa hali hizi, haadhibu mtu kama adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala hafungi mtu kama afungavyo Yeye.
Rudi kwenye sura

* 27. Ewe nafsi uliye tulia juu ya Haki!
Rudi kwenye sura

* 28. Rejea kwenye radhi ya Mola wako Mlezi nawe uradhi kwa neema ulio pewa, nawe umemridhisha kwa a'mali uliyo ikadimisha.
Rudi kwenye sura

* 29. Basi ingia katika kundi la waja wangu walio wema!
Rudi kwenye sura

* 30. Na ingia katika Pepo yangu, nyumba ya neema ya milele!
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani