Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Balad

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Naapa kiapo cha mkazo kwa mji wa Makka, mji mtakatifu;
Rudi kwenye sura

* 2. Na wewe unaishi katika mji huu, unauzidisha utukufu wake na cheo chake.
Rudi kwenye sura

* 3. Na naapa kwa mzazi na anacho kizaa, na kwa hao wawili ndio jinsi inahifadhika na maendeleo yanabakia.
Rudi kwenye sura

* 4. Hakika Sisi tumemuumba mtu katika mashaka na taabu tangu mwanzo wake mpaka kumalizika mambo yake.
Rudi kwenye sura

* 5. Je! Anadhani mtu aliye umbwa katika mashaka haya kuwa hapana awezae kumdhalilisha?
Rudi kwenye sura

* 6. Anasema: Nimetumia katika kupambana na Muhammad s.a.w. na kuupinga wito wake mali mengi ukiyakusanya pamoja.
Rudi kwenye sura

* 7. Ati anadhani kwamba mambo yake hayo yamefichikana, hayajui yeyote hata huyo aliye muumba?
Rudi kwenye sura

* 8,9. Kwani Sisi hatukumuumba na macho mawili ya kutazamia, na ulimi na midomo miwili ili aweze kutamka na kusema sawa?
Rudi kwenye sura

* 8,9. Kwani Sisi hatukumuumba na macho mawili ya kutazamia, na ulimi na midomo miwili ili aweze kutamka na kusema sawa?
Rudi kwenye sura

* 10. Na tukamwonyesha njia ya kheri na ya shari, na tukamtengenezea aweze kuchagua mojawapo?
Rudi kwenye sura

* 11. Basi huyo hakunafiika kwa tuliyo mtengenezea, wala hakuivuka njia ya milimani inayo mzuia asifikie uwokovu, nayo ni choyo wa nafsi yake.
Rudi kwenye sura

* 12. Na kitu gani kitakufunza nini huko kujitoma kwenye njia ya milimani?
Rudi kwenye sura

* 13. Kumkomboa mtu kutokana na utumwa,
Rudi kwenye sura

* 14. Au kumlisha siku ya njaa
Rudi kwenye sura

* 15. Yatima aliye jamaa wa kumliwaza kwa ujamaa na ufakiri.
Rudi kwenye sura

* 16. Au masikini mwingi wa haja na kufakirika.
Rudi kwenye sura

* 17. Tena awe pamoja na hayo miongoni mwa wenye Imani wanao usiana na wenzao kwa subira na kuoneana huruma.
Rudi kwenye sura

* 18. Hao wanao sifika kwa sifa hizi, ndio watu wa kheri, wa mkono wa kulia.
Rudi kwenye sura

* 19. Na walio zikataa dalili tulizo zisimamisha kuthibitisha Haki kutoka na Kitabu na hoja zake, hao ndio wapotovu watu waovu walio kosa kheri na watapata adhabu.
Rudi kwenye sura

* 20. Juu yao utakuwa Moto ulio bebeana na milango yake ikafungwa.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani