Al A'adiyaat Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
100.Surat Al-A'adiyaat

Imeshuka Makka Ina aya 11
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua, 1


2. Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini, 2


3. Wakishambulia wakati wa asubuhi, 3


4. Huku wakitimua vumbi, 4


5. Na wakijitoma kati ya kundi, 5


6. Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi! 6


7. Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo! 7


8. Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali! 8


9. Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini? 9


10. Na yakakusanywa yaliomo vifuani? 10


11. Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote! 11


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani