An Nas Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
114.Surat AnNas

Imeshuka Makka Ina aya 6
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu, 1


2. Mfalme wa wanaadamu, 2


3. Mungu wa wanaadamu, 3


4. Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas, 4


5. Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu, 5


6. Kutokana na majini na wanaadamu. 6


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani