Al Aa' Laa Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
87.Surat Al Aa'laa

Imeshuka Makka Ina aya 19
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa, 1


2. Aliye umba, na akaweka sawa, 2


3. Na ambaye amekadiria na akaongoa,3


4. Na aliye otesha malisho, 4


5. Kisha akayafanya makavu, meusi. 5


6. Tutakusomesha wala hutasahau, 6


7. Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana. 7


8. Na tutakusahilishia yawe mepesi. 8


9. Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. 9


10. Atakumbuka mwenye kuogopa. 10


11. Na atajitenga mbali nayo mpotovu, 11


12. Ambaye atauingia Moto mkubwa. 12


13. Tena humo hatakufa wala hawi hai. 13


14. Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa. 14


15. Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali. 15


16. Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia! 16


17. Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. 17


18. Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo, 18


19. Vitabu vya Ibrahimu na Musa. 19


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani