93.Surat Wadh-Dhuhaa |
Imeshuka Makka | Ina aya 11 |
Utangulizi | Orodha ya Sura | Faharasa |
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0
1. Naapa kwa mchana! 1
2. Na kwa usiku unapo tanda! 2
3. Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. 3
4. Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. 4
5. Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. 5
6. Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? 6
7. Na akakukuta umepotea akakuongoa? 1
8. Akakukuta mhitaji akakutosheleza? 8
9. Basi yatima usimwonee! 9
10. Na anaye omba au kuuliza usimkaripie! 10
11. Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie. 11
Sura Nyingine | Faharasa |