Al Qaaria'h maelezo
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Qaaria'h

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. AL-QAARIA'H, Inayo gonga, ni Kiyama, ambacho kinaanza kwa mpulizo wa mwanzo wa barugumu, na kinaishia itapo katwa hukumu baina ya watu.
Rudi kwenye sura

* 2. Kitu gani kilicho cha ajabu zaidi katika ukuu wake, na khatari zake na kitisho chake!
Rudi kwenye sura

* 3. Na kitu gani kitacho kujuulisha hali ya AL-QAARIA'H katika kitisho chake juu ya nafsi za watu?
Rudi kwenye sura

* 4. Siku hiyo watu watakuwa kama vipepeo kwa wingi na kuhangaika kulia na kushoto, madhaifu na wanyonge!
Rudi kwenye sura

* 5. Na milima itakuwa kama sufi iliyo tiwa rangi na kuchambuliwa kwa kutapanyika vipande mbali mbali na kupeperuka katika anga huku na huku.
Rudi kwenye sura

* 6,7. Ama yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, mema yake yakapindukia kuliko maovu yake, basi huyo atakuwa na maisha yatayo mridhisha mwenyewe, na nafsi yake itue.
Rudi kwenye sura

* 6,7. Ama yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, mema yake yakapindukia kuliko maovu yake, basi huyo atakuwa na maisha yatayo mridhisha mwenyewe, na nafsi yake itue.
Rudi kwenye sura

* 8,9. Na ama ambaye mizani yake itakuwa nyepesi, na maovu yake yakazidi kuliko mema yake, basi makaazi yake yatakuwa Jahannamu.
Rudi kwenye sura

* 8,9. Na ama ambaye mizani yake itakuwa nyepesi, na maovu yake yakazidi kuliko mema yake, basi makaazi yake yatakuwa Jahannamu.
Rudi kwenye sura

* 10. Na nini cha kukujuulisha ni nini Hawiya?
Rudi kwenye sura

* 11. Moto ulio mkali, hapana moto unao fikilia ukali wake, hata ukichochewa vipi na kutiwa kuni gani!
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani