Al A'sr maelezo
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul A'sr

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Naapa kwa Zama kwa sababu ya maajabu mengi na mazingatio yaliomo ndani yake.
Rudi kwenye sura

* 2. Hakika kila binaadamu bila ya shaka yumo katika namna fulani au fulani ya kukhasiri, kwa mujibu wa anavyo ghilibiwa na pumbao na matamanio.
Rudi kwenye sura

* 3. Isipo kuwa wale walio muamini Mwenyezi Mungu na wakatenda mema, na wakadumu juu ya ut'iifu, na wakasemezana na kuusiana kwa kushikamana na Haki, kwa itikadi, na maneno, na vitendo. Na wakausiana wasubiri na wavumilie mashaka yanayo wapata wenye kushikamana na Dini. Basi hao ndio wenye kusalimika na hiyo khasara, wenye kufanikiwa duniani na Akhera.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani