Maelezo: Suuratul Hud |
(1) Mwenyezi Mungu amemuamrisha Nabii s.a.w. asitie shaka, si kwa kuwa yawezekana kuwa yeye awe na shaka, lakini ni kuashiria kuwa walio kuwa duni yake Nabii wajilinde wasiache shaka ikaingia nyoyoni mwao. |
(1) Tazama Aya 27 Surat Al Muuminun (23). |
(1) Mlima huo uko Mosal (kaskazini mwa Iraq na kusini ya Turki) Ulikuwa maarufu hapo kale. |
(1) Hizi Aya mbili zinakataza kupunja kwa vipimo na mizani kwa kuwa ni ukhalifu unao stahiki kupewa adhabu na kuaziriwa. Makosa haya ya kupunja na udanganyifu pia yanahisabiwa ni ukhalifu hata katika kanuni za kutungwa za dikrii. Na katika Qur'ani tukufu ni moja katika njia ya kulinda mali. Nchi ya Madyana ipo baina ya kaskazi ya Hijazi na kusini ya Sham. Na hii ilikuwa imejaa miti. Ikiitwa Al-aykah,(yaani Machakani). Na Mwenyezi Mungu aliwapelekea adhabu kwa sababu ya uasi wao. |