Al Falaq maelezo
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Falaq

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Sema najikinga na Mola Mlezi wa asubuhi inapo pambazuka kutokana na usiku.
Rudi kwenye sura

* 2. Na shari ya kila chenye shari katika viumbe, ambavyo hapana wa kuzuia shari yao ila Mwenye kumiliki amri yao.
Rudi kwenye sura

* 3. Na shari ya usiku unapo kuwa totoro.
Rudi kwenye sura

* 4. Na shari ya anaye pita baina ya watu kwa sababu ya kuwafisidi.
Rudi kwenye sura

* 5. Na shari ya hasidi anaye tamani iondoke neema kwa wengine.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani