Adh-dhaariyaat maelezo
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Adh-dhaariyaat

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1,2,3,4. Ninaapa kwa pepo zinazo timua mawingu, zikayasukuma kwa nguvu, huku zikibeba mizigo mizito ya maji, zikawa zinakwenda kwa wepesi kwa amri ya Mwenyezi Mungu, zikawa zinagawanya riziki kwa ampendaye Mwenyezi Mungu.

* 5,6. Hakika hayo mnayo ahidiwa, nayo ya kufufuliwa na mengineyo, ni hakika ya kweli itakayo tokea, na kwamba kwa yakini malipo kwa vitendo vyenu yatakuwa tu hapana hivi wala hivi.

* 7,8. Ninaapa kwa mbingu zenye njia zilizo wekwa baraabara, kwamba nyinyi msemapo mnayo yasema ni maneno ya kugongana.

* 9. Huacha kuamini hiyo ahadi ya kweli na malipo yatakayo kuwa huyo anaye acha, kwa sababu amekhiari kufuata pumbao la nafsi yake kuliko akili yake.
Rudi kwenye sura

* 10,11. Wameteketea waongo wanao sema katika khabari za Kiyama kuwa ni mambo ya dhana na kukisia tu, ambao kwamba wamezamishwa katika ujinga, wameghafilika na dalili za yakini.

* 12. Wanauliza kwa kejeli, kwa kuwa wanaona hayawi hayo: Lini itakuwa hiyo siku ya malipo?
Rudi kwenye sura

* 13. Siku watapo simamishwa Motoni wakichomwa!
Rudi kwenye sura

* 14. Wataambiwa: Onjeni adhabu yenu hii ambayo duniani mlikuwa mkiihimiza iwe.
Rudi kwenye sura

* 15. Hakika walio mt'ii Mwenyezi Mungu na wakamkhofu watakuwa wananeemeka katika Mabustani na chemchem za Peponi ambazo haziwezi kusifika hakika yake.
Rudi kwenye sura

* 16. Wakipokea thawabu na takrima wanazo pewa na Mola wao Mlezi. Hakika hao kabla ya hapo walikuwa duniani ni wenye kufanya mambo mazuri kwa kutimiza waliyo takiwa wayafanye.
Rudi kwenye sura

* 17,18. Walikuwa kulala kwao usiku ni kuchache, na wakikesha sana kwa ibada, na mwishoni mwa usiku walikuwa wakiomba maghfira.

* 19. Na katika mali yao wakiweka fungu maalumu lilio thibiti kwa ajili ya wenye haja, wanao omba na wanao jizuilia kuomba kwa kujiteta.
Rudi kwenye sura

* 20. Na katika ardhi zipo dalili nyingi zilizo wazi zinazo pelekea yakini, kwa mwenye kuitafuta njia.
Rudi kwenye sura

* 21. Na hali kadhaalika katika nafsi zenu zipo Ishara zilizo wazi. Je! Mmeghafilika nazo, hamzioni?
Rudi kwenye sura

* 22. Na katika mbingu ipo amri ya riziki zenu na kukadiriwa mnayo ahidiwa.
Rudi kwenye sura

* 23. Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi kwamba hakika yote hayo mnayo yakanya kuwa, yaani kufufuliwa, kulipwa, kuadhibiwa wanao kadhibisha, na kuwalipa thawabu wachamngu, yote hayo bila ya shaka ni ya kweli thaabiti kama hivyo kusema kwenu ambako hamna shaka nako kuwa mnasema.
Rudi kwenye sura

* 24,25. Unakijua kisa cha Malaika, wageni wa hishima wa Ibrahim? Pale walipo ingia kwake na wakamtolea Salamu, na yeye akawajibu kwa Salamu, na kuwambia kuwa ni watu asio wajua.

* 26,27. Akenda kwa mkewe naye ana khofu, akaja na ndama aliye nona. Akawakaribisha, nao hawakula. Akasema kwa kuto wajua hakika yao: Mbona hamli?

* 28. Akahisi katika nafsi yake khofu kuwaogopa. Wakasema: Usiogope. Na wakampa bishara kuwa atapata mwana mwenye ilimu nzuri.
Rudi kwenye sura

* 29. Akatokea mkewe akipiga kelele alipo isikia ile bishara, akijipiga uso wake kwa mkono wake, kwa kuona muhali hayo na kustaajabu, na akasema: Mimi ni kizee, na tasa. Itakuwaje nizae?
Rudi kwenye sura

* 30. Wakasema: Hivyo ndivyo alivyo kwisha hukumu Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima katika kila anayo hukumu, ni Mwenye ujuzi ambaye hapana linalo fichikana kwake lolote.
Rudi kwenye sura

* 31. Ibrahim akasema: Mna kazi gani tena baada ya khabari hii nzuri, enyi wajumbe?
Rudi kwenye sura

* 32,33,34. Wakasema: Kwa hakika sisi tumetumwa kwa kaumu iliyo pita kiasi katika uasi, tuwatupie mawe ya udongo, ambayo hapana anaye yajua yalivyo ila Mwenyezi Mungu. Mawe hayo ni makhsusi na maalumu kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka katika mambo machafu.

* 35,36. Basi tukahukumu tuwatoea kwenye mji huo walio amini. Lakini hatukukuta ila nyumba moja tu ndiyo ya Waislamu.

* 37. Na katika mji huo tumeacha alama ya maangamizo ya watu wake, ili wapate kuzingatia wanayo ikhofu adhabu chungu.
Rudi kwenye sura

* 38. Na katika kisa cha Musa yapo mawaidha. Tulipo mtuma kwa Firauni, na tukatilia nguvu kwa kumpa ushahidi ulio wazi.
Rudi kwenye sura

* 39. Firauni akapuuza kumuamini Musa kwa kutegemea ati nguvu zake. Akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu!
Rudi kwenye sura

* 40. Tukamchukua yeye na hao anao jitapia kwao, tukawatumbukiza baharini, naye ni mwenye kuyatenda hayo ya ukafiri na inda anayo laumiwa kwayo.
Rudi kwenye sura

* 41. Na katika kisa cha A'di yamo mawaidha pia. Tulipo wapelekea upepo usio kuwa na kheri yoyote.
Rudi kwenye sura

* 42. Upepo huo haupiti kwa kitu chochote ila hukiacha kama fupa lilio nyambuka.
Rudi kwenye sura

* 43,44. Na katika kisa cha Thamudi ipo Ishara. Walipo ambiwa: Stareheni katika majumba yenu kwa muda maalumu. Wakajivuna na wakatakabari wasifuate amri ya Mola wao Mlezi. Basi radi ikawaangamiza nao wanaiona kwa macho yao inavyo tokea.

* 45. Basi hawakuweza kuinuka. Wala hawakuweza kujipigania kuijikinga na adhabu.
Rudi kwenye sura

* 46. Na kaumu ya Nuhu tuliihiliki kabla ya hawa. Hakika hao walikuwa watu walio toka nje ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura

* 47,48. Na mbingu tumeipanga kwa nguvu, na bila ya shaka Sisi ni waweza zaidi ya hayo. (1) Na ardhi tumeikunjua, na Sisi ni wenye kuitengeneza vizuri kama kitanda.
(1) Aya hii tukufu inaashiria maana za kitaalamu nyingi; miongoni mwazo ni kwamba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ameumba ulimwengu huu mkunjufu kwa nguvu. Na Yeye ni Muweza kwa atakayo. Na maana ya mbingu katika Aya hii ni kila kilicho juu ya kitu na kikakifunika. Basi kila kilicho zunguka sayari na nyota na mkusanyiko wa jua katika sehemu hii inayo onekana ya ulimwengu kimetanda kupita inavyo kadirika na akili, wala haiwezi kupimika. Kwani masafa yao hukisiwa kwa mamilioni ya miaka ya mwangaza. Na mwaka mmoja wa mwangaza kwa ilivyo thibiti kwa ilimu za kisasa katika karne hii ya ishirini ni masafa yanayo kwenda mwangaza kwa mbio za kilomita 300,000 kwa nukta moja ya dakika. Na ibara ya Aya tukufu (Na hakika Sisi ndio twenye kuutanua) inaashiria hayo, yaani kutanda huko kwa ulimwengu kunako staajabisha tangu kuumbwa kwake. Kama vile vile kuwa kukunjuka huko kungali kunaendelea, na hayo sayansi ya sasa imethibitisha vile vile. Na imejuulikana kwa nadhariya ya kutanda ambayo katika mwanzo mwanzo wa karne hii imethibiti kuwa ni kweli kiilimu, na ufupi wake ni kuwa ulimwengu unaendelea kukua na kupanuka, na kila sayari za mbinguni zinajitenga wenyewe kwa wenyewe.

* 49. Na kila kitu tumekiumba namna mbili, yaani kwa jozi, ili mpate kukumbuka muuamini uwezo wetu.
Rudi kwenye sura

* 50,51. Basi fanyeni haraka kuendea kwenye ut'iifu wa Mwenyezi Mungu. Wala msimfanye mungu mwengine kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi nimekujieni kwa amri ya Mwenyezi Mungu kukuonyeni kwa uwazi matokeo ya ushirikina.

* 52. Hivyo ndivyo ilivyo kuwa hali ya mataifa yote kwa Mitume wao. Hakuja Mtume kwa watu wa kabla ya kaumu yako ila walimwita: Mchawi au mwendawazimu.
Rudi kwenye sura

* 53. Je! Mmeusiana, mmeambizana, nyinyi kwa nyinyi kusema hivyo ndio maana mnalirejea hilo kwa hilo? Bali hao ni watu walio pindukia mipaka, ndio wakawafikiana katika kuwashutumu Mitume!
Rudi kwenye sura

* 54. Basi wapuuzilie mbali hawa wenye inda! Wewe hulaumiki usipo wajibu kitu.
Rudi kwenye sura

* 55. Wewe dumisha kukumbusha, kwani ukumbusho huwazidisha Waumini kufumbua macho na kuwa na nguvu za yakini.
Rudi kwenye sura

* 56. Wala sikuwaumba majini na watu kwa jambo la kuniletea Mimi manufaa, bali ili waniabudu, na kuniabudu Mimi ni manufaa kwao.
Rudi kwenye sura

* 57. Sitaki kwao riziki, kwani Mimi si mhitaji kwa walimwengu wote; wala sitaki wanilishe, kwani Mimi ndiye ninaye lisha, wala silishwi.
Rudi kwenye sura

* 58. Hakika Mwenyezi Mungu peke yake, ndiye mdhamini wa kuwapa riziki waja wake, na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Aliye imara, hashindiki.
Rudi kwenye sura

* 59. Hakika hao walio jidhulumu nafsi zao kwa ukafiri na kukanusha wana fungu lao la adhabu mfano wa fungu la wenzao katika kaumu zilizo kwisha pita. Basi wasifanye haraka kuhimiza adhabu ishuke kabla ya wakati wake.
Rudi kwenye sura

* 60. Basi maangamio yatawapata wenye kuikataa siku yao waliyo ahidiwa, kwa sababu ya shida na vitisho viliomo katika siku hiyo.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani