Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo ya Sura: Suuratun Najm

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

*1. Ninaapa kwa nyota inapo tua kwa kuchwa, ya kwamba Muhammad hakuiacha Njia iliyo sawa ya kufuata Haki, na wala hakupata kuitakidi upotovu.
Rudi kwenye sura

*2. Ninaapa kwa nyota inapo tua kwa kuchwa, ya kwamba Muhammad hakuiacha Njia iliyo sawa ya kufuata Haki, na wala hakupata kuitakidi upotovu.
Rudi kwenye sura

*3. Wala halitoki katika anayo yatamka ya Qur'ani kwa mapendo ya nafsi yake.
Rudi kwenye sura

*4. Hii Qur'ani anayo itamka si chochote ila ni Wahyi (Ufunuo) ulio toka kwa Mwenyezi Mungu anamfunulia yeye.
Rudi kwenye sura

*5. Aliye mfundisha ufunuo huu ni mwenye nguvu nyingi.
Rudi kwenye sura

*6. Ambaye ametua akili zake na maoni yake, akasimama sawa sawa katika sura yake; naye yuko upande wa juu katika mbingu upeo wa macho wa mwenye kuangalia.
Rudi kwenye sura

*7. Ambaye ametua akili zake na maoni yake, akasimama sawa sawa katika sura yake; naye yuko upande wa juu katika mbingu upeo wa macho wa mwenye kuangalia.
Rudi kwenye sura

*8. Kisha Jibrili alimkaribia, na akazidi kukaribia, hata akawa ukaribu wake ni kiasi ya mipinde miwili, bali karibu kuliko hivyo.
Rudi kwenye sura

*9. Kisha Jibrili alimkaribia, na akazidi kukaribia, hata akawa ukaribu wake ni kiasi ya mipinde miwili, bali karibu kuliko hivyo.
Rudi kwenye sura

*10. Jibrili akamfunulia mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, alicho mfunulia, nao ufunuo huo ni jambo lenye shani kubwa na athari ya mbali kabisa.
Rudi kwenye sura

*11. Moyo wa Muhammad haukukanya yale macho yake yaliyo yaona.
Rudi kwenye sura

*12. Hivyo nyinyi mnamkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu na mnabishana naye kwa aliyo yaona kwa macho yake?
Rudi kwenye sura

*13. Na bila ya shaka Muhammad alimwona Jibrili kwa sura yake mara nyengine, katika pahala pasipo juulikana ila na Mwenyezi Mungu tu, ambapo amepaita Sidratul muntahaa, "Mkunazi wa Mwisho". Na akasimulia kuwa hapo ndio ipo Jannatul Ma-awa, Bustani inayo kaliwa. Vikafunikwa na kuzibwa, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, visio weza kuelezwa. Jicho la Muhammad halikubabaika kwa aliyo yaona, na wala hakukiuka mpaka ya aliyo amrishwa kwa kuona kwake huko.
Rudi kwenye sura

*14. Na bila ya shaka Muhammad alimwona Jibrili kwa sura yake mara nyengine, katika pahala pasipo juulikana ila na Mwenyezi Mungu tu, ambapo amepaita Sidratul muntahaa, "Mkunazi wa Mwisho". Na akasimulia kuwa hapo ndio ipo Jannatul Ma-awa, Bustani inayo kaliwa. Vikafunikwa na kuzibwa, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, visio weza kuelezwa. Jicho la Muhammad halikubabaika kwa aliyo yaona, na wala hakukiuka mpaka ya aliyo amrishwa kwa kuona kwake huko.
Rudi kwenye sura

*15. Na bila ya shaka Muhammad alimwona Jibrili kwa sura yake mara nyengine, katika pahala pasipo juulikana ila na Mwenyezi Mungu tu, ambapo amepaita Sidratul muntahaa, "Mkunazi wa Mwisho". Na akasimulia kuwa hapo ndio ipo Jannatul Ma-awa, Bustani inayo kaliwa. Vikafunikwa na kuzibwa, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, visio weza kuelezwa. Jicho la Muhammad halikubabaika kwa aliyo yaona, na wala hakukiuka mpaka ya aliyo amrishwa kwa kuona kwake huko.
Rudi kwenye sura

*16. Na bila ya shaka Muhammad alimwona Jibrili kwa sura yake mara nyengine, katika pahala pasipo juulikana ila na Mwenyezi Mungu tu, ambapo amepaita Sidratul muntahaa, "Mkunazi wa Mwisho". Na akasimulia kuwa hapo ndio ipo Jannatul Ma-awa, Bustani inayo kaliwa. Vikafunikwa na kuzibwa, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, visio weza kuelezwa. Jicho la Muhammad halikubabaika kwa aliyo yaona, na wala hakukiuka mpaka ya aliyo amrishwa kwa kuona kwake huko.
Rudi kwenye sura

*17. Na bila ya shaka Muhammad alimwona Jibrili kwa sura yake mara nyengine, katika pahala pasipo juulikana ila na Mwenyezi Mungu tu, ambapo amepaita Sidratul muntahaa, "Mkunazi wa Mwisho". Na akasimulia kuwa hapo ndio ipo Jannatul Ma-awa, Bustani inayo kaliwa. Vikafunikwa na kuzibwa, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, visio weza kuelezwa. Jicho la Muhammad halikubabaika kwa aliyo yaona, na wala hakukiuka mpaka ya aliyo amrishwa kwa kuona kwake huko.
Rudi kwenye sura

*18. Hakika ameona mengi katika Ishara za Mwenyezi Mungu na maajabu yake makubwa makubwa.
Rudi kwenye sura

*19. Je! Mmeyajua hayo, na mkayafikiri ya kina Lata na Uzza na Manata, huyo mwengine wa tatu, mlio wafanya kuwa ni miungu wa kuwaabudu?
Rudi kwenye sura

*20. Je! Mmeyajua hayo, na mkayafikiri ya kina Lata na Uzza na Manata, huyo mwengine wa tatu, mlio wafanya kuwa ni miungu wa kuwaabudu?
Rudi kwenye sura

*21. Mkagawa, nyinyi muwe na watoto wa kiume, na mkamfanyia Mwenyezi Mungu awe na watoto wa kike!
Rudi kwenye sura

*22. Huo basi ni ugawaji wa dhulma, mnamgawia Mwenyezi Mungu kile mnacho kichukia nyinyi wenyewe!
Rudi kwenye sura

*23. Hayo masanamu yenu si chochote ila ni majina tu yasiyo na maana yoyote ya kiungu. Mmeyatunga nyinyi na baba zenu kwa kufuata pumbao lenu la upotovu. Mwenyezi Mungu hakuteremsha nayo hoja yoyote ya kusadikisha huo uzushi wenu mnao wadaia. Na hawa hawafuati ila ni dhana tu, na kipendacho nyoyo zao zilio potoka na kuacha maumbile yaliyo sawa. Na hakika yalikwisha wajia kutoka kwa Mola wao Mlezi yenye uwongofu, laiti wangeli ufuata huo!
Rudi kwenye sura

*24. Mwanaadamu hapati kila anacho kitamani, ya kupata uombezi wa haya masanamu au mengineyo anayo yatamani kwa nafsi yake. Kwani mambo yote, ya duniani na Akhera, ni ya Mwenyezi Mungu peke yake.
Rudi kwenye sura

*25. Mwanaadamu hapati kila anacho kitamani, ya kupata uombezi wa haya masanamu au mengineyo anayo yatamani kwa nafsi yake. Kwani mambo yote, ya duniani na Akhera, ni ya Mwenyezi Mungu peke yake.
Rudi kwenye sura

*26. Na malaika wengi wa mbinguni, juu ya ubora wa vyeo vyao, haufai kitu uombezi wao isipo kuwa baada ya kupewa idhini huyo mwombezi na Mwenyewe Mtukufu, na kumridhia huyo mwenye kuombewa.
Rudi kwenye sura

*27. Hakika hao wasio iamini Akhera ndio bila ya shaka wanao sema kuwa Malaika ni wanawake. Wanasema: Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu!
Rudi kwenye sura

*28. Na kwa kauli hii hawana ujuzi wowote. Hawafuati kitu ila dhana zao tu zilio potoka, na dhana haifai kitu mbele ya haki.
Rudi kwenye sura

*29. Basi jitenge nao hao makafiri walio ipuuza Qur'ani na ikawa hamu yao si chochote ila uhai wa duniani tu, wakiyakataa yenye maslaha nao.
Rudi kwenye sura

*30. Hayo wanayo yafuata katika itikadi zao, na vitendo vyao ndio ukomo walio yafikilia katika ilimu. Hakika Mola wako Mlezi anamjua vyema anaye shikilia upotovu, na anamjua vyema aliye elekea kupokea uwongofu.
Rudi kwenye sura

*31. Na ni vya Mwenyezi Mungu pekee vyote viliomo katika mbingu na ardhi, kwa kuviumba na kuvidabiri, ili awalipe walio potea wenye kufanya viovu vitendo vyao, na awalipe walio hidika watu wema kwa malipo yaliyo mema.
Rudi kwenye sura

*32. Wema hao ndio wale wanao jitenga na madhambi yenye adhabu kubwa kubwa, na yanayo chukiza mno. Lakini Mwenyezi Mungu husamehe dhambi ndogo ndogo. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkuu wa kughufiria, naye anajua vyema hali zenu. Kwani Yeye ndiye aliye kuumbeni kutokana na ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu katika hali zenu mbali mbali za kukua na kugeuka. Basi msikae mkijisifu nafsi zenu kuwa mmesafika kwa kujigamba na kujifakhari. Na Yeye ndiye Mjuzi mkubwa kabisa wa kila mwenye kumcha na akajisafisha nafsi yake kweli kweli kwa uchamngu wake.
Rudi kwenye sura

*33. Je! Umezingatia ukamwona anaye puuza kuifuata Haki, na akatoa kidogo katika mali, na khalafu akakata kabisa kutoa? Je! Huyo anayo ilimu ya kujua mambo ya ghaibu, basi kwa hivyo ndio anayajua yanayo mpelekea kuiacha kuifuata Haki, na akafanya ubakhili wa mali?
Rudi kwenye sura

*34. Je! Umezingatia ukamwona anaye puuza kuifuata Haki, na akatoa kidogo katika mali, na khalafu akakata kabisa kutoa? Je! Huyo anayo ilimu ya kujua mambo ya ghaibu, basi kwa hivyo ndio anayajua yanayo mpelekea kuiacha kuifuata Haki, na akafanya ubakhili wa mali?
Rudi kwenye sura

*35. Je! Umezingatia ukamwona anaye puuza kuifuata Haki, na akatoa kidogo katika mali, na khalafu akakata kabisa kutoa? Je! Huyo anayo ilimu ya kujua mambo ya ghaibu, basi kwa hivyo ndio anayajua yanayo mpelekea kuiacha kuifuata Haki, na akafanya ubakhili wa mali?
Rudi kwenye sura

*36. Kwani huyo hakuambiwa yaliomo katika Vitabu vya Musa na Ibrahim, aliye fika ukomo wa kutimiza aliyo agana na Mwenyezi Mungu, ya kwamba hapana mtu ataye mbebea dhambi mwenginewe?
Rudi kwenye sura

*37. Kwani huyo hakuambiwa yaliomo katika Vitabu vya Musa na Ibrahim, aliye fika ukomo wa kutimiza aliyo agana na Mwenyezi Mungu, ya kwamba hapana mtu ataye mbebea dhambi mwenginewe?
Rudi kwenye sura

*38. Kwani huyo hakuambiwa yaliomo katika Vitabu vya Musa na Ibrahim, aliye fika ukomo wa kutimiza aliyo agana na Mwenyezi Mungu, ya kwamba hapana mtu ataye mbebea dhambi mwenginewe?
Rudi kwenye sura

*39. Na kwamba mtu hapati ila malipo ya vitendo vyake mwenyewe.
Rudi kwenye sura

*40. Na kwamba vitendo vyake vitakuja tangazwa, na ataviona Siku ya Kiyama, iwe ni kumtukuza mtenda mema, na kumkebehi mtenda maovu.
Rudi kwenye sura

*41. Kisha kila mtu atalipwa malipo anayo stahiki.
Rudi kwenye sura

*42. Na kwamba kwa hakika ni kwa Mola wako Mlezi, wala si kwa mwenginewe, ndio miadi ya kurejea.
Rudi kwenye sura

*43. Na Yeye peke yake ni Mwenye uweza wa kuufanya uso uonyeshe furaha au maudhiko, na pia ni Mwenye kuziumba sababu za starehe na dhiki.
Rudi kwenye sura

*44. Na hakika ni Yeye, ndiye Mwenye kuondoa uhai, na kuuleta.
Rudi kwenye sura

*45. Na Yeye ndiye aliye umba vitu kwa jozi, yaani dume na jike, binaadamu na wanyama, kutokana na manii yanayo miminwa. Makusudio ya Aya hii tukufu ni kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba Yeye ameumba waume na wake katika wanaadamu na wanyama wote kutokana na tone ya manii ambayo humo humo mna ume na uke. Na juu ya udogo wake na udhaifu wake ndio chemchem ya uhai. Umuujiza wa Qur'ani unadhihirika katika Aya hii tukufu ukikumbuka kuwa ulimwengu ulikuwa haujui mpaka hivi karibu kuwa katika maji ya mwanamume ndio zimo mbegu "sperms" na katika maji ya mwanamke mna vijiyai "ova", ndio vikikutana vijidudu vya manii ya mwanamume na vijiyai vya mwanamke vikawa kitu kimoja ndio hiyo huwa mimba. Ukweli huu ulitajwa na Qur'ani kabla ya kuvumbuliwa na ilimu za Sayansi.
Rudi kwenye sura

*46. Na Yeye ndiye aliye umba vitu kwa jozi, yaani dume na jike, binaadamu na wanyama, kutokana na manii yanayo miminwa. Makusudio ya Aya hii tukufu ni kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba Yeye ameumba waume na wake katika wanaadamu na wanyama wote kutokana na tone ya manii ambayo humo humo mna ume na uke. Na juu ya udogo wake na udhaifu wake ndio chemchem ya uhai. Umuujiza wa Qur'ani unadhihirika katika Aya hii tukufu ukikumbuka kuwa ulimwengu ulikuwa haujui mpaka hivi karibu kuwa katika maji ya mwanamume ndio zimo mbegu "sperms" na katika maji ya mwanamke mna vijiyai "ova", ndio vikikutana vijidudu vya manii ya mwanamume na vijiyai vya mwanamke vikawa kitu kimoja ndio hiyo huwa mimba. Ukweli huu ulitajwa na Qur'ani kabla ya kuvumbuliwa na ilimu za Sayansi.
Rudi kwenye sura

*47. Na juu yake Yeye ndio kufufua baada ya kifo.
Rudi kwenye sura

*48. Na Yeye ndiye anaye toa kinacho tosheleza, na akaridhisha kwa kinacho kinaisha na cha kuweka akiba.
Rudi kwenye sura

*49. Na hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa hii nyota kubwa inayo itwa Shii'ra (Sirius, Dog Star). Makusudio hapa ni Nyota hiyo inayo itwa Ash-shi'ra Alyamaaniya, au wanavyo ita Wazungu Sirius au Dog Star. Nyota hii inang'ara kwa nguvu zaidi kuliko nyota zote ziliomo katika kikundi cha nyota kinacho itwa Alkalbu l-akbar, kwa Kizungu Canis Major au Greater Dog. Nyota hiyo ndiyo inayo zagaa sana mbinguni, na huonekana kusini ya mstari wa kati wa mbinguni kiasi ya daraja 18. Na kwa jina hilo la Nyota ya Mbwa ikijuulikana hata miaka elfu tatu ilio pita. Katika mabaki ya michoro ya Mafirauni wa Misri imeashiriwa pia. Mwenyezi Mungu ameitaja khasa kwa kuwa Waarabu walikuwa wakiiabudu hapo kale, na pia Wamisri wa zamani, kwani kutokea kwake upande wa mashariki katikati ya mwezi wa Julai kabla ya kuchomoza jua kulikuwa kunawafikiana na wakati wa mafuriko ya Misri ya kati, yaani katika tukio muhimu kabisa katika ulimwengu huo wa kale. Na tukio hili huenda ndilo lilio fanya kuanzisha kuwekea kiwango urefu wa mwaka katika dunia nzima. Kwani kudhihiri Nyota ya Shiira kabla ya kuchomoza jua hakutokei ila mara moja tu katika mwaka. Basi huu ndio mwanzo wa mwaka mpya.
Rudi kwenye sura

*50. Na Yeye ndiye aliye wateketeza kina A'di wa mwanzo, kaumu ya Nabii Hudi. Na akawateketeza Thamudi, kaumu ya Nabii Saleh. Hakuwabakisha.
Rudi kwenye sura

*51. Na Yeye ndiye aliye wateketeza kina A'di wa mwanzo, kaumu ya Nabii Hudi. Na akawateketeza Thamudi, kaumu ya Nabii Saleh. Hakuwabakisha.
Rudi kwenye sura

*52. Na aliwaangamiza kaumu ya Nuhu kabla ya kuwaangamiza A'di na Thamudi. Hakika hao walikuwa wamekithiri kudhulumu, na wamezidi kwa uasi kuliko A'di na Thamudi.
Rudi kwenye sura

*53. Na miji ya kaumu Lut'i iliyo pinduliwa juu chini, ni Yeye Mwenyezi Mungu ndiye aliye ipindua.
Rudi kwenye sura

*54. Akaizunguka kwa kuiadhibu kama alivyo izunguka. Basi katika neema za Mola wako Mlezi una shaka nayo ipi?
Rudi kwenye sura

*55. Akaizunguka kwa kuiadhibu kama alivyo izunguka. Basi katika neema za Mola wako Mlezi una shaka nayo ipi?
Rudi kwenye sura

*56. Hii Qur'ani ni onyo katika jinsi ya yale yale maonyo ya kale waliyo onywa kwayo watu walio tangulia.
Rudi kwenye sura

*57. Kiyama kimekaribia; na wala hapana wa kuujuulisha wakati kitapo tokea ila mwenyewe Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura

*58. Kiyama kimekaribia; na wala hapana wa kuujuulisha wakati kitapo tokea ila mwenyewe Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura

*59. Hivyo nyinyi mnapinga kila la kweli? Na mnaistaajabia kwa kuikaataa hii Qur'ani? Na mnacheka kwa kejeli na maskhaara, wala hamlii kama wafanyavyo wenye yakini, nanyi mmo katika pumbao na kutakabari?
Rudi kwenye sura

*60. Hivyo nyinyi mnapinga kila la kweli? Na mnaistaajabia kwa kuikaataa hii Qur'ani? Na mnacheka kwa kejeli na maskhaara, wala hamlii kama wafanyavyo wenye yakini, nanyi mmo katika pumbao na kutakabari?
Rudi kwenye sura

*61. Hivyo nyinyi mnapinga kila la kweli? Na mnaistaajabia kwa kuikaataa hii Qur'ani? Na mnacheka kwa kejeli na maskhaara, wala hamlii kama wafanyavyo wenye yakini, nanyi mmo katika pumbao na kutakabari?
Rudi kwenye sura

*62. Basi msujudieni Mwenyezi Mungu aliye iteremsha Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu wote, na muabuduni Yeye tu peke yake Mwenye kutukuka kwa utukufu wake.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani