At tahriim maelezo
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul At tahriim

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Ewe Nabii! Kwa nini unajikhini nafsi yako alicho kuhalalishia Mwenyezi Mungu? Unataka kuwaridhi wakezo, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mkunjufu wa kurehemu.
Rudi kwenye sura

* 2. Amekuwekeeni Sharia ya kuondoa viapo vyenu kwa kafara. Na Mwenyezi Mungu ni Bwana wenu, Mwenye kutawala mambo yenu, na Yeye ni Mtimilivu wa ujuzi, basi anakuwekeeni Sharia zenye kheri yenu, naye ni Mwenye hikima katika kuweka Sharia zake.
Rudi kwenye sura

* 3. Na taja pale Nabii alipo msimulia jambo kwa siri mmoja katika wake zake, na alipo ifichua. Na Mwenyezi Mungu akamjuvya Nabii wake kuwa imefichuliwa. Akamjuvya baadhi, na akamzuilia - kwa staha - baadhi nyengine. Alipo mjuvya, akasema yule mke: Nani aliye kwambia haya? Akasema Nabii: Ameniambia Mwenye kujua kila kitu, asiye fichika kitu.
Rudi kwenye sura

* 4. Mkirejea nyinyi wawili kwa Mwenyezi Mungu nanyi mmejuta basi itakuwa mmefanya waajibu wenu wa kutubu, kwa sababu nyoyo zenu zilikuwa zimeacha jambo analo lipenda Mtume wa Mwenyezi Mungu, nalo ni kuweka siri. Na ikiwa mtasaidiana kinyume chake kwa mambo ya kumuudhi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msaidizi wake, na Jibrili, na Waumini wanao sifika kwa wema, na Malaika baada ya msaada wa Mwenyezi Mungu nao ni wenye kumsaidia.
Rudi kwenye sura

* 5. Asaa Mola wake Mlezi akikuacheni, enyi wakeze, atamwoza badala yenu wake wengine walio wanyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu kwa ut'iifu, wenye kusadiki kwa nyoyo zao, wanyonge mbele ya Mwenyezi Mungu, wenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa toba, wenye kumuabudu kwa kujidhalilisha kwake, wendao kila njia za ut'iifu kwa Mwenyezi Mungu, wajane na bikra.
Rudi kwenye sura

* 6. Enyi mlio amini! Jihifadhini nafsi zenu na ahali zenu na Moto, ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanao simamia kazi yake na kuwaadhibu waliomo humo ni Malaika wakali, na wana nguvu katika muamala wao. Na wao hutekeleza lile wanalo amrishwa, wala hawakawilishi.
Rudi kwenye sura

* 7. Wataambiwa makafiri Siku ya Kiyama: Msitafute udhuru leo! Hapana shaka mnalipwa mliyo kuwa mkiyatenda.
Rudi kwenye sura

* 8. Enyi mlio amini! Rejeeni kwa Mwenyezi Mungu, muache madhambi yenu, mrejee kweli kweli kwa ikhlasi. Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu, na akakutieni Peponi kwenye kupita mito chini ya majumba yake na miti yake, Siku atakayo inyanyua Mwenyezi Mungu hadhi ya Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao hao itakuwa inakwenda mbele yao, nayo itakuwa kuliani mwao, nao watakuwa wakisema kwa kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu: Ewe Bwana wetu, Mwenye kumiliki mambo yetu! Tutimizie nuru yetu, mpaka tuongoke kufikia Peponi. Na tusamehe dhambi zetu. Hakika Wewe ni Mtimilivu wa uweza juu ya kila kitu.
Rudi kwenye sura

* 9. Ewe Nabii! Pambana kwa Jihadi na hao walio tangaza ukafiri wao, na wanaafiki walio uficha ukafiri wao, kwa kila unacho kimiliki, nguvu na hoja. Na kuwa mkali juu ya makundi yote mawili hayo katika Jihadi yako. Na makaazi ya hao ni Jahannamu. Na marejeo maovu ni hayo marejeo yao!
Rudi kwenye sura

* 10. Mwenyezi Mungu ametaja hali ya ajabu inayo juulikana kuwa ni hali zinazo fanana kwa wanao kufuru. Nayo ni hali ya mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Hao walikuwa chini ya ulinzi wa waja wawili katika waja wema. Nao wakawakhuni kwa kupanga njama dhidi yao, na kufichua siri zao kwenda wambia kaumu zao. Na waja wema wawili hawakuweza kuwakinga wake zao kwa lolote katika adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na wakaambiwa hao wake wawili walipo angamizwa: Ingieni Motoni pamoja na wanao ingia!
Rudi kwenye sura

* 11. Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano kwa Waumini kisa cha mke wa Firauni alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba karibu na rehema yako Peponi, na uniokoe na utawala wa Firauni na vitendo vyake vilivyo pita mipaka katika dhulma, na uniokoe na kaumu ya wanao fanya uadui!
Rudi kwenye sura

* 12. Na Mwenyezi Mungu amewapigia Waumini mfano wa Mariamu binti wa Imrani, ambaye amehifadhi utupu wake, tukampulizia humo katika roho yetu, akashika mimba ya Isa. Naye akayasadiki maneno ya Mwenyezi Mungu, nayo ni amri zake, na makatazo yake, na Vitabu vilivyo teremshwa juu ya Mitume wake. Na yeye alikuwa miongoni mwa idadi walio dumu juu ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu. (Huku kupuliziwa Mariamu roho ya Mwenyezi Mungu si kiroja, kwani wanaadamu wote wamepuliziwa kadhaalika. Soma Surat Al-H'ijr Aya 28-29 inapo simuliwa alipo umbwa mtu na akapuliziwa kutokana na roho ya Mwenyezi Mungu.)
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani