Al Buruuj maelezo
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Buruuj

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Naapa kwa mbingu yenye Buruj au Manaazil, njia au vituo ambavyo nyota hupitia katika nyendo zake, Buruuj au Manaazil ndio huu mkusanyiko wa nyota unao onekana kwa sura namna mbali mbali mbinguni. Hizo Buruuj zimegawika sehemu kumi na mbili ambazo ardhi inazipitia inapo lizunguka jua.
Rudi kwenye sura

* 2. Na kwa Siku iliyo ahidiwa kuwa ndiyo Siku ya Hisabu na Malipo,
Rudi kwenye sura

* 3. Na kwa viumbe watao hudhuria Siku hiyo wakaona vitisho na ajabu zitakazo kuwepo,
Rudi kwenye sura

* 4. Hakika Mwenyezi Mungu amewalaani watu walio chimba khandaki katika ardhi,
Rudi kwenye sura

* 5. Wakawasha moto kuwatumbukiza ndani yake Waumini ili kuwatesa,
Rudi kwenye sura

* 6. Na wao wamekaa ukingoni mwake wakishuhudia mateso yanayo wapata Waumini.
Rudi kwenye sura

* 7. Na wao wapo hapo wamehudhuria kwenye mateso wanayo watendea Waumini.
Rudi kwenye sura

* 8. Na hapana walilo lichukia kwa hao Waumini ila ni kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu ambaye adhabu yake huogopwa, Msifiwa anaye tarajiwa thawabu zake.
Rudi kwenye sura

* 9. Ambaye, peke yake, ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi anashuhudia yote wayatendayo Waumini na makafiri na atawalipa kwayo.
Rudi kwenye sura

* 10. Hakika walio watia matatani Waumini wanaume na Waumini wanawake kwa maudhi na kuwaadhibu kwa moto, kisha wasitubu na kurejea nyuma watapata Akhera adhabu ya Jahannamu kwa ukafiri wao, na watapata adhabu ya kuunguzwa kwa kule kuwaunguza moto Waumini.
Rudi kwenye sura

* 11. Hakika hao walio kusanya kwenye Imani ya Mwenyezi Mungu vitendo vyema watapata Mabustani yapitayo mito kati yake. Neema hiyo waliyo lipwa ni kufuzu kukubwa.
Rudi kwenye sura

* 12. Hakika mshiko wa Mola wako Mlezi kuwashika majabari umefika ukomo kwa ukali wake
Rudi kwenye sura

* 13. Ni Yeye peke yake ndiye Mwenye kuanza kuumba, na kisha ni Yeye anaye rejeza tena,
Rudi kwenye sura

* 14. Na Yeye ni Mwingi wa msamaha kwa mwenye kutubu na akarejea, na Mwingi wa mapenzi kwa mwenye kumpenda na akamt'ii.
Rudi kwenye sura

* 15. Yeye ndiye Mwenye Kiti cha Enzi na Mwenye kukimiliki, na Mkuu kwa dhati yake na sifa zake.
Rudi kwenye sura

* 16. Ni Mtendaji kwa alitakalo, na hendi kinyume na uweza wake yeyote anaye taka.
Rudi kwenye sura

* 17. Je! Imekujia, ewe Muhammad, hadithi ya kile kikundi kilicho a'si katika mataifa yaliyo kwisha pita?
Rudi kwenye sura

* 18. Kaumu ya Firauni na Thamudi na yaliyo washukia katika malipo ya kushikilia kwao upotovu?
Rudi kwenye sura

* 19. Bali hao makafiri katika kaumu yako ni shadidi zaidi katika kukukadhibisha kuliko hawa walivyo wakadhibisha Mitume wao.
Rudi kwenye sura

* 20. Na Mwenyezi Mungu anawaweza hao, na anawajua vilivyo.
Rudi kwenye sura

* 21. Bali hii ulio waletea ni Qur'ani tukufu inadhihirisha hoja za ukweli wako.
Rudi kwenye sura

* 22. Imo katika Ubao Ulio Hifadhiwa, hapana uwezo unao weza kuipotoa au kuigeuza
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani