Ash shams maelezo
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratush Shams

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Naapa kwa jua na mwangaza wake na kuchomoza kwake na kwa joto lake!
Rudi kwenye sura

* 2. Na kwa mwezi unapo lifuata na likawa nyuma yake kwa kutoa mwangaza baada ya kuchwa jua,
Rudi kwenye sura

* 3. Na kwa mchana unapo lidhihirisha jua, likaonekana wazi halikufichikana.
Rudi kwenye sura

* 4. Na kwa usiku unapo lifunika jua, ukawa mwangaza wake hauonekani.
Rudi kwenye sura

* 5. Na kwa mbingu na kwa Mweza Mtukufu aliye inyanyua na akaijenga kwa hikima yake.
Rudi kwenye sura

* 6. Na kwa ardhi na kwa Mweza Mtukufu aliye ikunjua kwa kila upande, na akaitengeneza kwa ajili ya utulivu, na akaifanya kama tandiko.
Rudi kwenye sura

* 7. Na kwa nafsi, na aliye iumba na akaiweka sawa, kwa kuipa nguvu,
Rudi kwenye sura

* 8. Akaifunza jema na baya, na akaipa uweza wa kutenda itakayo katika hayo,
Rudi kwenye sura

* 9. Hakika amefuzu mwenye kuisafisha nafsi yake kwa ut'iifu na vitendo vya kheri.
Rudi kwenye sura

* 10. Na hakika amekhasiri mwenye kuzificha fadhila zake, na akayaua matayarisho aliyo umbwa nayo ya kutenda kheri.
Rudi kwenye sura

* 11,12. Kina Thamudi walimkanusha Nabii wao kwa upotovu wao na jeuri zao, alipo gutuka mwovu wao mkubwa kabisa kutaka kumchinja ngamia.
Rudi kwenye sura

* 11,12. Kina Thamudi walimkanusha Nabii wao kwa upotovu wao na jeuri zao, alipo gutuka mwovu wao mkubwa kabisa kutaka kumchinja ngamia.
Rudi kwenye sura

* 13. Saleh, Mtume wa Mwenyezi Mungu, akawaambia: Mwachilieni huyu ngamia wa Mwenyezi Mungu ale maridhawa katika ardhi ya Mwenyezi Mungu, na tahadharini msimzuie maji katika siku yake aliyo wekewa.
Rudi kwenye sura

* 14. Wakamkadhibisha Mtume wao katika hilo onyo lake, wakamchinja. Mola wao Mlezi akazibomoa nyumba zao kwa sababu ya dhambi zao; akazisawazisha na ardhi!
Rudi kwenye sura

* 15. Wala Yeye Mwenyezi Mungu hakhofu matokeo ya adhabu hiyo, kwani hiyo ni malipo ya haki kwa yale waliyo yatenda.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani