Al Layl maelezo
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Layl

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Naapa kwa usiku kinapo enea kiza chake!
Rudi kwenye sura

* 2. Na naapa kwa mchana unapo zagaa mwangaza wake!
Rudi kwenye sura

* 3. Na naapa kwa Mjuzi aliye umba viwili viwili, dume na jike, katika kila vinavyo zaliwa!
Rudi kwenye sura

* 4. Hakika juhudi zenu bila ya shaka zimekhitalifiana; kwani wapo wenye kubahatika katika juhudi zao, na wako wasio bahatika.
Rudi kwenye sura

* 5,6,7. Ama mwenye kutoa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na akamkhofu Mola wake Mlezi, na kwa hivyo akaepuka anayo yakataza, na akayakinika kufuata fadhila njema, nayo ni Imani kumuamini Mwenyezi Mungu kwa kumjua, basi Sisi tutamtengenezea awe katika khulka ya wepesi na raha kwa kumwongoza kwenye njia ya kheri.
Rudi kwenye sura

">* 5,6,7. Ama mwenye kutoa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na akamkhofu Mola wake Mlezi, na kwa hivyo akaepuka anayo yakataza, na akayakinika kufuata fadhila njema, nayo ni Imani kumuamini Mwenyezi Mungu kwa kumjua, basi Sisi tutamtengenezea awe katika khulka ya wepesi na raha kwa kumwongoza kwenye njia ya kheri.

* 8,9,10. Ama mwenye kufanya ubakhili kwa mali yake asitoe haki ya Mwenyezi Mungu iliomo humo, na akawa hana haja na yatokayo kwa Mwenyezi Mungu, na akakadhibisha khulka nzuri, basi huyo tutamtengenezea khulka ambayo inapelekea uzito na mashaka ya milele.
Rudi kwenye sura

">* 8,9,10. Ama mwenye kufanya ubakhili kwa mali yake asitoe haki ya Mwenyezi Mungu iliomo humo, na akawa hana haja na yatokayo kwa Mwenyezi Mungu, na akakadhibisha khulka nzuri, basi huyo tutamtengenezea khulka ambayo inapelekea uzito na mashaka ya milele.

* 11. Na kitu gani katika adhabu ambacho hayo mali yake yataweza kumkinga nacho, atapo teketea yeye mwenyewe mzima?
Rudi kwenye sura

* 12. Hakika ni juu yetu, Sisi, kwa kufuatana na hikima yetu, ndio tuwabainishie viumbe njia ya uwongofu.
Rudi kwenye sura

* 13. Na juu yetu Sisi peke yetu, bila ya shaka, hili jambo la kuendesha yaliomo duniani na Akhera.
Rudi kwenye sura

* 14. Ndio maana tukakutieni khofu ya Moto unao waka na kuripuka!
Rudi kwenye sura

* 15,16. Hawauingii kwa kudumu ila kafiri aliye ikadhibisha Haki na akazipuuza Ishara za Mola wake Mlezi.
Rudi kwenye sura

* 15,16. Hawauingii kwa kudumu ila kafiri aliye ikadhibisha Haki na akazipuuza Ishara za Mola wake Mlezi.
Rudi kwenye sura

* 17,18. Na atakuwa mbali na huo Moto aliye mwingi wa kujikinga na ukafiri na maasi, amabye hutoa mali yake wakati wa nafasi ili kujisafisha na uchafu wa ubakhili, na najsi ya uchoyo.

* 19. Na mtoaji huyu si kama anaye mtu yeyote ambaye ndio anamlipa kwa neema aliyo mfanyia zamani,
Rudi kwenye sura

* 20. Bali anatoa hicho kwa kutafuta radhi ya Mola wake Mlezi Mtukufu tu.
Rudi kwenye sura

* 21. Na bila ya shaka atakuja pata kutoka kwa Mola wake Mlezi anacho kitaka kwa njia za ukamilifu kabisa, hata itimie radhi kwake.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani