At Tin maelezo
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratut Tin

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Naapa kwa tini na zaituni, kwa baraka zao na ubora wa manufaa yao.
Rudi kwenye sura

* 2. Na kwa mlima ambao juu yake ndio Mwenyezi Mungu alimsemeza Musa.
Rudi kwenye sura

* 3. Na kwa huu mji mtukufu wa Makka, ambao anaushuhudia utukufu wake mwenye kwenda uzuru, na anapata amani mwenye kuuingia.
Rudi kwenye sura

* 4. Kwa hakika bila ya shaka yoyote Sisi tumemuumba mtu amesimama sawa kwa umbo bora kabisa lilio nyooka, na akasifika kwa sifa nzuri kabisa.
Rudi kwenye sura

* 5. Kisha tukamteremsha cheo mpaka akawa ni wa chini kabisa katika hao walioko chini, kwa kuacha kufanya waajibu wa hayo tuliyo muumbia.
Rudi kwenye sura

* 6. Lakini walio amini na wakatenda vitendo vyema, hao basi watapata ujira usio wakatikia wala kuwapungukia.
Rudi kwenye sura

* 7. Basi kitu gani kinacho kupelekea kukadhibisha kufufuliwa na kulipwa baada ya kuwekwa wazi uweza wetu wa hayo?
Rudi kwenye sura

* 8. Kwani Mwenyezi Mungu aliye yatenda hayo tuliyo kueleza si muadilifu kuliko mahakimu wote kwa kufanya na kupanga?
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani