Al A'laq maelezo
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul A'laq

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Ewe Muhammad! Soma unayo funuliwa kwa kufunguliwa kwa Jina la Mola wako Mlezi ambaye ni Yeye tu peke yake ndiye Mwenye uweza wa kuumba.
Rudi kwenye sura

* 2. Amemuumba mtu kwa ukamilifu wa mwili wake na ilimu kutokana na kipande cha damu ambacho hakina chochote cha kupelekea kujiona bora.
Rudi kwenye sura

* 3. Endelea na kusoma, na Mola wako Mlezi aliye Karimu kushinda wote, atakutukuza wala hatakudharau.
Rudi kwenye sura

* 4. Yeye ndiye ambaye aliye mfunza mtu kuandika kwa kalamu, na wala kwanza hakuwa anajua hayo.
Rudi kwenye sura

* 5. Amemfunza mtu yasiyo kuwa yanampitia katika mawazo yake.
Rudi kwenye sura

* 6,7. Ni hakika kweli mtu hupindukia mpaka na hupanda kiburi mbele ya Mola wake Mlezi anapo jiona si mhitaji, katajirika.
Rudi kwenye sura

* 6,7. Ni hakika kweli mtu hupindukia mpaka na hupanda kiburi mbele ya Mola wake Mlezi anapo jiona si mhitaji, katajirika.
Rudi kwenye sura

* 8. Ewe Muhammad! Hakika ni kwa Mola wako Mlezi peke yake ndiyo yako marejeo ya wote kwa kufufuliwa na kulipwa.
Rudi kwenye sura

* 9,10. Je! Umemwona huyu jeuri anaye mzuia mja asisali anapo taka kusali?
Rudi kwenye sura

* 9,10. Je! Umemwona huyu jeuri anaye mzuia mja asisali anapo taka kusali?
Rudi kwenye sura

* 11,12. Hebu niambie khabari za jeuri huyu kama yeye yumo katika uwongofu katika huku kuzuia kwake, au kwamba ndio anaamrisha uchamngu katika hayo anayo amrisha!
Rudi kwenye sura

* 11,12. Hebu niambie khabari za jeuri huyu kama yeye yumo katika uwongofu katika huku kuzuia kwake, au kwamba ndio anaamrisha uchamngu katika hayo anayo amrisha!
Rudi kwenye sura

* 13. Niambie khabari za huyu mwenye kukataza anapo yakadhibisha aliyo kuja nayo Mtume, na akapuuza Imani na vitendo vyema!
Rudi kwenye sura

* 14. Hivyo hajui kwamba Mwenyezi Mungu anazijua vyema hali zake, naye atamlipa kwazo?
Rudi kwenye sura

* 15. Kwa kumkemea huyu mwenye kuzuia, anaambiwa kama hakuacha hayo anayo yafanya, basi hapana shaka tutamkokota kwa nguvu tukimshika kwa shungi lake la nywele mpaka Motoni!
Rudi kwenye sura

* 16. Hilo shungi lilio juu ya uso wake mwenye kuropokwa uwongo na mwenye athari za ukosefu!
Rudi kwenye sura

* 17. Basi yeye awaite wenziwe na watu wa baraza lake wawe ndio wasaidizi duniani au Akhera.
Rudi kwenye sura

* 18. Sisi tutawaita askari wetu wamsaidie Muhammad na walio pamoja naye, na wapambane na huyo mwenye kukanya na wasaidizi wawasukume kwenye Jahannamu!
Rudi kwenye sura

*19. Kumnyamazisha huyu mwenye kuzuia, wewe usimkubalie kwa hayo anayo kukataza nayo, na dumu juu ya Sala zako, na endelea na sijida zako, na jijongeze kwa Mola wako Mlezi kwa hivyo.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani