Al Bayyinah maelezo
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Bayyinah

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Hawakuwa walio mkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake miongoni mwa Mayahudi na Wakristo, na miongoni mwa washirikina, waache kughafilika kwao na ujinga wao kuto ijua Haki mpaka iwajie hoja ya kukata.
Rudi kwenye sura

* 2,3. Na hoja hiyo ni Mtume aliye tumwa kutokana na Mwenyezi Mungu awasomee kurasa zilizo takasika na upotovu, ndani yake zimo hukumu zilizo sawa zenye kutamka kwa haki na kwa yaliyo ndiyo.
Rudi kwenye sura

* 2,3. Na hoja hiyo ni Mtume aliye tumwa kutokana na Mwenyezi Mungu awasomee kurasa zilizo takasika na upotovu, ndani yake zimo hukumu zilizo sawa zenye kutamka kwa haki na kwa yaliyo ndiyo.
Rudi kwenye sura

* 4. Wala hawakufarikiana walio pewa Kitabu katika Mayahudi na Wakristo, ila baada ya kuwajia hiyo hoja iliyo wazi yenye kuonyesha ya kwamba Muhammad ndiye huyo Mtume wa Mwenyezi Mungu aliye ahidiwa katika Vitabu vyao.
Rudi kwenye sura

* 5. Na hawakulazimishwa jambo katika walio lazimishwa ila iwe ibada yao kwa Mwenyezi Mungu ni kumsafia Yeye Dini, waache upotovu wasimame sawa kwenye Haki, na wazihifadhi Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Mila Iliyo Nyooka.
Rudi kwenye sura

* 6. Hakika wale walio kufuru katika Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu, wala hawatatoka humo. Hao ndio waovu wa viumbe kwa itikadi na vitendo.
Rudi kwenye sura

* 7. Hakika wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakatenda vitendo vyema, hao ndio bora ya viumbe kwa itikadi na vitendo.
Rudi kwenye sura

* 8. Malipo yao Akhera kwa Imani na vitendo vyema walivyo vitanguliza, ni Mabustani ya kudumu yenye kupitiwa na mito kati yake, watakaa humo milele. Mwenyezi Mungu amepokea a'mali zao, na wao watamshukuru kwa hisani yake aliyo wafanyia. Hiyo ndiyo jaza ya mwenye kuiogopa adhabu ya Mola wake Mlezi, akaamini na akatenda mema.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani