Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Insan

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Hakika kimempitia mwanaadamu kipindi cha zama kabla hajapuliziwa roho, naye hata bado hakuwa ni kitu cha kutajika kwa jina lake, wala hajuulikani nini atakuwa.
Rudi kwenye sura

* 2. Hakika Sisi tumemuumba mwanaadamu naye ana sifa namna mbali mbali, kwa ajili ya kumtia mtihanini, majaribioni, baadaye. Kwa hivyo tukamjaalia awe anasikia na anaona, ili apate kuzisikia Aya na azione Ishara.
Rudi kwenye sura

* 3. Hakika Sisi tumembainishia Njia ya Uwongofu, ama awe Muumini au awe kafiri.
Rudi kwenye sura

* 4. Hakika Sisi tumewawekea tayari makafiri minyororo kuwafungia miguu yao, pingu za kuwafungia mikono na shingo, na moto unao waka.
Rudi kwenye sura

* 5,6. Hakika walio kuwa wakweli katika Imani yao watakunywa mvinyo iliyo changanywa na maji ya kafuri. Hiyo ni chemchem wanayo inywa waja wa Mwenyezi Mungu, na wanaipitisha watakapo kwa sahala.

* 7. Wanatekeleza yaliyo wajibikia , na wanaikhofu Siku kubwa hiyo ambayo madhara yake yataenea kote kote,
Rudi kwenye sura

* 8. Na huwalisha chakula mafakiri wasio weza kazi, na watoto walio fiwa na wazee wao, na wafungwa wasio miliki kitu, ijapo kuwa wao wenyewe hao watoaji wanakipenda hicho wanacho kitoa, na wanakihitajia.
Rudi kwenye sura

* 9. Na hujiambia nafsi zao: Hakika sisi tunakulisheni kwa ajili ya kutaka thawa;bu za Mwenyezi Mungu. Sisi hatutaki kwenu malipo au zawadi, wala hatutaki kushukuriwa na kusifiwa.
Rudi kwenye sura

* 10. Hakika sisi tunakhofu kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku ya kumletea msiba atakaye kuwapo siku hiyo, na siku ya watu kukunja nyuso zao na vipaji vyao.
Rudi kwenye sura

* 11,12. Basi Mwenyezi Mungu akawalinda na shida za siku hiyo, na badala ya mkunjo wa wenye maasi, akawapa nyuso za kupendeza, na ukunjufu na furaha katika nyoyo zao, na akawajazi kwa ile subira yao Pepo imeenea furaha, na nguo zake ni hariri laini.

* 13. Wakiegemea huko Peponi juu ya makochi, hawaoni joto la jua, wala shida ya baridi.
Rudi kwenye sura

* 14. Na Pepo ambayo vivuli vya miti yake vimeenea kote kote, na matunda yake mepesi kuyachuma.
Rudi kwenye sura

* 15,16. Na wakiwazungukia watumishi wao kwa bilauri za kunywea zilio fanywa kwa fedha, lakini unaona kiliomo ndani kama kwamba ni kigae, na vinapimwa vinywaji kwa kadiri wanavyo penda wanywaji.

* 17,18. Na watu wema hupewa kunywa huko Peponi mvinyo inayo fanana na sharubati ya tangawizi kwa utamu. Hiyo ni kutokana na chemchem ya Peponi inayo itwa Salsabil, kwa sababu ya wepesi wa unywaji wake na uzuri wake.

* 19. Na watakuwa wanawazunguka vijana ambao hawabadiliki hali yao, kwa furaha na sururi. Ukiwaona wanapo zunguka kwa wepesi na uchangamfu, utawadhania kwa uzuri wao na usafi wa rangi zao, kama lulu zilizo tandazwa mbele yako zinang'ara.
Rudi kwenye sura

* 20. Na ukitazama popote katika hiyo Pepo utaona neema kubwa, na ufalme ulio tanda.
Rudi kwenye sura

* 21. Juu yao zipo nguo za hariri nyepesi za kijani, na nguo za hariri nzito. Na mapambo yao yaliomo mikononi mwao ni vikuku vya fedha. Na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji kingine kilio safi, hakina uchafu wala najisi.
Rudi kwenye sura

* 22. Hakika neema hizi ameziandaa kwa kukulipeni kwa vitendo vyenu. Na hizo juhudi zenu duniani ni zenye kusifika kwa Mwenyezi Mungu, na zinampendeza, na zimekubaliwa.
Rudi kwenye sura

* 23. Hakika Sisi, kwa rehema yetu na hikima yetu, tumekuteremshia wewe Qur'ani kwa njia ya kukutuza moyo wako, na uweze daima kuihifadhi, basi huto isahau kabisa.
Rudi kwenye sura

* 24. Basi subiri, uivumilie hikima ya Mola wako Mlezi kwa kuakhirisha kushinda kwako kuwashinda maadui zako, na wewe ukapata mitihani kwa maudhi yao. Wala usiwat'ii washirikina, wingi wa madhambi, walio zama katika ukafiri.
Rudi kwenye sura

* 25,26. Na dumisha kumkumbuka na kumtaja Mola wako Mlezi, na sali alfajiri mapema, na adhuhuri, na alasiri jioni, na usiku sali magharibi na isha. Na fanya ibada za usiku kwa muda mrefu.

* 27. Hakika hawa makafiri wanaipenda dunia, na wanaifadhilisha kuliko Akhera. Na wanaiacha migongoni mwao siku yenye misiba mikubwa, na vitisho vikali. Wala wao hawajui nini cha kuwaokoa wao na hayo!
Rudi kwenye sura

* 28. Sisi tumewaumba wao, na tumefanya kwa hikima kuumbwa kwao. Na tukitaka tutawateketeza wao na tutawaleta mfano ya wao badala yao, ambao hao watakuja kumt'ii Mwenyezi Mungu kinyume na wao.
Rudi kwenye sura

* 29. Hakika Sura hii ni mawaidha kwa walimwengu wote. Basi mwenye kutaka atafuata njia ya Imani na uchamngu kwendea kwa Mola wake Mlezi imfikishe kwenye maghfira yake na Pepo yake.
Rudi kwenye sura

* 30. Wala nyinyi hamwezi kutaka kitu chochote ila wakati anapo taka Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzijua hali zenu, Mwenye hikima kwa anayo yataka na akayakhiari.
Rudi kwenye sura

* 31. Humuingiza amtakaye katika Pepo yake. Basi kuingia Peponi ni kwa fadhila na rehema ya Mwenyezi Mungu. Naye amewadhalilisha wenye kudhulumu, amewatengenezea adhabu iliyo chungu.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani