| 1.Suurat al-Faatih'a |
| Imeshuka Makka | Ina aya 7 |
| Utangulizi | Orodha ya Sura | Faharasa |

1. KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
1

2. Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;
2

3. Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;
3

4. Mwenye kumiliki siku ya malipo.
4

5. Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada.
5

6. Tuongoe njia iliyonyooka.
6

7. Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.
7
| Sura Nyingine | Faharasa |