| 26.Suurat Shu'araa |
| Imeshuka Makka | Ina aya 227 |
| Utangulizi | Sura Nyingine | Faharasa |

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0

1. T'aa Siin Miim. (T'.S.M.)
1

2. Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha.
2

3. Huenda labda ukajikera nafsi yako kwa kuwa hawawi Waumini.
3

4. Tunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea
shingo zao.
4

5. Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman ila wao hujitenga
nao.
5

6. Kwa yakini wamekanusha; kwa hivyo zitakuja wafikia khabari za
yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha.
6

7. Je! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila
namna nzuri?
7

8. Hakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi wao hawakuwa wenye
kuamini.
8

9. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
9

10. Na Mola wako Mlezi, alipo mwita Musa, akamwambia: Fika kwa watu
madhaalimu,
10

11. Watu wa Firauni. Hawaogopi?
11

12. Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe.
12

13. Na kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu haukunjuki vyema.
Basi mtumie ujumbe Harun.
13

14. Na wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopa wasije kuniuwa.
14

15. Akasema: Siyo hivyo kabisa! Nendeni na miujiza yetu. Hakika Sisi
tu pamoja nanyi, tunasikiliza.
15

16. Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa
Mola Mlezi wa walimwengu wote.
16

17. Waachilie Wana wa Israili wende nasi.
17

18. (Firauni) akasema: Sisi hatukukulea wewe utotoni, na ukakaa kwetu
katika umri wako miaka mingi?
18

19. Na ukatenda kitendo chako ulicho tenda, nawe ukawa miongoni mwa
wasio na shukrani?
19

20. (Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa miongoni mwa
wale walio potea.
20

21. (Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa miongoni mwa
wale walio potea.
21

22. Na hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia, na wewe umewatia utumwani
Wana wa Israili?
22

23. Firauni akasema: Na nani huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote?
23

24. Akasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na viliomo baina
yao, ikiwa nyinyi ni wenye yakini.
24

25. (Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi?
25

26. (Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba
zenu wa kwanza.
26

27. (Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni
mwendawazimu.
27
1

28. (Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na
viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini.
28

29. (Firauni) akasema: Ukimfuata mungu mwengine asiye kuwa mimi,
basi bila ya shaka nitakufunga gerezani.
29

30. Akasema: Je! Ijapo kuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi?
30

31. Akasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wasemao kweli.
31

32. Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri.
32

33. Na akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwa watazamao.
33

34. (Firauni) akawaambia waheshimiwa walio mzunguka: Hakika huyu
ni mchawi mtaalamu.
34

35. Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna
shauri gani?
35

36. Wakasema: Mpe muda yeye na nduguye na uwatume mijini wapigao
mbiu ya mgambo.
36

37. Wakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu.
37

38. Basi wakakusanywa wachawi wakati na siku maalumu.
38

39. Na watu wakaambiwa: Je! Mtakusanyika?
39

40. Huenda tutawafuata wachawi wakiwa wao ndio watakao shinda.
40

41. Basi walipo kuja wachawi wakamwambia Firauni: Je! Tutapata ujira
tukiwa sisi ndio tulio shinda?
41

42. Naam! Na hakika mtakuwa katika watu wa mbele.
42

43. Musa akwaambia: Tupeni mnavyo taka kutupa.
43

44. Basi wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema: Kwa nguvu
za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenye kushinda.
44

45. Musa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua.
45

46. Hapo wachawi walipinduka wakasujudu.
46

47. Wakasema: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote.
47

48. Mola Mlezi wa Musa na Harun.
48

49. (Firauni) akasema: Je! Mmemuamini kabla sijakuruhusuni? Bila
ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliye kufunzeni uchawi. Basi mtakuja
jua! Nitakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakubandikeni
misalabani nyote.
49

50. Wakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu
Mlezi.
50

51. Hakika sisi tunatumai Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu,
kwa kuwa ndio wa kwanza wa kuamini.
51

52. Na tulimuamrisha Musa kwa wahyi: Nenda na waja wangu wakati wa
usiku. Kwa hakika mtafuatwa.
52

53. Basi Firauni akawatuma mijini wapiga mbiu za mgambo.
53

54. (Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo.
54

55. Nao wanatuudhi.
55

56. Na sisi ni wengi, wenye kuchukua hadhari.
56

57. Basi tukawatoa katika mabustani na chemchem,
57

58. Na makhazina, na vyeo vya hishima,
58

59. Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili.
59

60. Basi wakawafuata lilipo chomoza jua.
60

61. Na yalipo onana majeshi mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika
sisi bila ya shaka tumepatikana!
61

62. (Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi.
Yeye ataniongoa!
62

63. Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako.
Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa.
63

64. Na tukawajongeza hapo wale wengine.
64

65. Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote.
65

66. Kisha tukawazamisha hao wengine.
66

67. Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao
si katika wenye kuamini.
67

68. Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
68

69. Na wasomee khabari za Ibrahim.
69

70. Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini?
70

71. Wakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea.
71

72. Akasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita?
72

73. Au yanakufaeni, au yanakudhuruni?
73

74. Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo.
74

75. Je! Mmewaona hawa mnao waabudu-
75

76. Nyinyi na baba zenu wa zamani?
76

77. Kwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu
wote.
77

78. Ambaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiye ananiongoa,
78

79. Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha.
79

80. Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha.
80

81. Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha.
81

82. Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya
Malipo.
82

83. Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao
mema.
83

84. Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadaye.
84

85. Na unijaalie katika warithi wa Bustani za neema.
85

86. Na umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu.
86

87. Wala usinihizi Siku watapo fufuliwa.
87

88. Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana.
88

89. Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi.
89

90. Na Pepo itasogezwa kwa wachamngu.
90

91. Na Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu.
91

92. Na wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwaabudu
92

93. Badala ya Mwenyezi Mungu? Je! Wanakusaidieni, au wanajisaidia
wenyewe?
93

94. Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu,
94

95. Na majeshi ya Ibilisi yote.
95

96. Watasema, na hali ya kuwa wanazozana humo:
96

97. Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri,
97

98. Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote.
98

99. Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote.
99

100. Basi hatuna waombezi.
100

101. Wala rafiki wa dhati.
101

102. Laiti tungeli pata kurejea tena tungeli kuwa katika Waumini.
102

103. Hakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye
kuamini.
103

104. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
104

105. Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume.
105

106. Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu?
106

107. Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
107

108. Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
108

109. Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa
Mola Mlezi wa walimwengu wote.
109

110. Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
110

111. Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa
chini?
111

112. Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya?
112

126. Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua!
113

114. Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini.
114

115. Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri.
115

116. Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe.
116

117. Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha.
117

118. Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi
na walio pamoja nami, Waumini.
118

119. Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu
iliyo sheheni.
119

120. Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia.
120

121. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
121

122. Kina A'd waliwakanusha Mitume.
122

123. Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu?
123

124. Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
124

125. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
125

126. Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila
kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
126

127. Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi?
127

128. Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele!
128

129. Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari.
129

130. Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari.
130

131. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
131

132. Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua.
132

133. Amekupeni wanyama wa kufuga na wana.
133

134. Na mabustani na chemchem.
134

135. Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa.
135

136. Wakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni
mwa watoao mawaidha.
136

137. Haya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokea zamani.
137

138. Wala sisi hatutaadhibiwa.
138

139. Wakamkanusha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika
haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
139

140. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
140

141. Kina Thamud waliwakanusha Mitume.
141

142. Alipo waambia ndugu yao Saleh: Je! Hamumchimngu?
142

143. Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
143

144. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
144

145. Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola
Mlezi wa walimwengu wote.
145

146. Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa?
146

147. Katika mabustani, na chemchem?
147

148. Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva.
148

149. Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi.
149

150. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
150

151. Wala msit'ii amri za walio pindukia mipaka,
151

152. Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi.
152

153. Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa.
153

154. Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa
wewe ni miongoni mwa wasemao kweli.
154

155. Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi
muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu.
155

156. Wala msimguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa.
156

157. Lakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta.
157

158. Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini
hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
158

159. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
159

160. Watu wa Lut'i waliwakanusha Mitume.
160

161. Alipo waambia ndugu yao, Lut'i: Je! Hamumchimngu?
161

162. Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu.
162

163. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi.
163

164. Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa
Mola Mlezi wa walimwengu wote.
164

165. Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?
165

166. Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu?
Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!
166

167. Wakasema: Ewe Lut'i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni
mwa wanao tolewa mji!
167

168. Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo
chenu.
168

169. Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo.
169

170. Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote,
170

171. Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma.
171

172. Kisha tukawaangamiza wale wengine.
172

173. Na tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa.
173

174. Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
174

175. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu,
Mwenye kurehemu.
175

176. Watu wa Machakani waliwakanusha Mitume.
176

177. Shuaibu alipo waambia: Je! Hamfanyi mkamchamngu?
177

178. Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
178

179. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
179

180. Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola
Mlezi wa walimwengu wote.
180

181. Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja.
181

182. Na pimeni kwa haki iliyo nyooka;
182

183. Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi.
183

184. Na mcheni aliye kuumbeni nyinyi na vizazi vilivyo tangulia.
184

185. Wakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa.
185

186. Na wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona
wewe ni katika waongo.
186

187. Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni
mwa wasemao kweli.
187

188. Akasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayo yatenda.
188

189. Basi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika
hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa.
189

190. Hakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwa wengi wao wenye
kuamini.
190

191. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu
Mwenye kurehemu.
191

192. Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu
wote.
192

193. Ameuteremsha Roho muaminifu,
193

194. Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji,
194

195. Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi.
195

196. Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale.
196

197. Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa
Wana wa Israili?
197

198. Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu,
198

199. Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini.
1990

200. Namna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu.
200

201. Hawataiamini mpaka waione adhabu chungu.
201

202. Basi itawafikia kwa ghafla, na hali hawana khabari.
202

203. Na watasema: Je, tutapewa muhula?
203

204. Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu?
204

205. Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka,
205

206. Kisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa,
206

207. Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa?
207

208. Wala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa na waonyaji
208

209. Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu.
209

210. Wala Mashet'ani hawakuteremka nayo,
10

211. Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi.
11

212. Hakika hao wametengwa na kusikia.
12

213. Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa
miongoni mwa watakao adhibiwa.
13

214. Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.
14

215. Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini.
15

216. Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo
yatenda.
16

217. Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
17

218. Ambaye anakuona unapo simama,
18

219. Na mageuko yako kati ya wanao sujudu.
19

220. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.
20

221. Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani?
21

222. Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi.
22

223. Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo.
23

224. Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata.
24

225. Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde?
25

226. Na kwamba wao husema wasiyo yatenda?
26

227. Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka
Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu
watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.
27
| Sura Nyingine | Faharasa |