3.Suurat Al 'Imran |
Imeshuka Madina | Ina aya 200 |
Utangulizi | Orodha ya Sura | Faharasa |
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0
1. Alif Laam Miim.
1
2. Mwenyezi Mungu, hakuna mungu ila Yeye Aliye Hai, Msimamizi wa
yote milele.
2
3. Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa
kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili
3
4. Kabla yake, ziwe uwongofu kwa watu. Na akateremsha Furqani (Upambanuo).
Hakika walio zikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu watakuwa na adhabu kali.
Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye kulipa.
4
5. Hakika Mwenyezi Mungu hakifichiki chochote kwake, duniani wala
mbinguni.
5
6. Yeye ndiye anaye kuundeni ndani ya matumbo ya wazazi kwa namna
apendayo. Hapana mungu ila Yeye, Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
6
7. Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya
muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine
za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano
kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana
yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema:
Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki
hayo isipo kuwa wenye akili.
7
8. (Na hao husema): Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada
ya kwisha tuongoa, na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye Mpaji.
8
9. Mola wetu Mlezi! Wewe ndiye Mkusanyaji wa watu kwa Siku isiyo
na shaka ndani yake. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.
9
10. Kwa hakika wale walio kufuru hazitowafaa kitu kwa Mwenyezi Mungu
mali zao, wala watoto wao; nao hao ndio kuni za Motoni.
10
11. Kama yaliyo wapata watu wa Firauni na wale walio kuwa kabla
yao. Walikanusha Ishara zetu, basi Mwenyezi Mungu aliwashika kwa madhambi
yao; na Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
11
12. Waambie walio kufuru: Karibuni mtashindwa na mtakusanywa, mtiwe
kwenye Jahannam; nako huko ni makao mabaya kabisa.
12
13. Hakika ilikuwa ni Ishara kwenu katika yale majeshi mawili yalipo
pambana. Jeshi moja likipigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na jingine
kafiri likiwaona zaidi kuliko wao mara mbili, kwa kuona kwa macho. Na Mwenyezi
Mungu humuunga mkono amtakaye kwa nusura yake. Hakika katika hayo yapo
mazingatio kwa wenye macho.
13
14. Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na wana, na mirundi
ya dhahabu na fedha, na farasi asili, na mifugo, na mashamba. Hayo ni starehe
ya maisha ya duniani; na kwa Mwenyezi Mungu ndio kwenye marejeo mema.
14
15. Sema: Nikwambieni yaliyo bora kuliko hayo? Kwa wachamngu ziko
Bustani kwa Mola wao zipitazo mito kati yake. Watadumu humo, na wake walio
takaswa, na wanazo radhi za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye
kuwaona waja wake.
15
16. Ambao husema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumeamini, basi tufutie
madhambi yetu, na tuepushe na adhabu ya Moto,
16
17. Wanao subiri, wanao sema kweli, na wat'iifu, na wanao toa sadaka,
na wanao omba maghafira kabla ya alfajiri.
17
18. Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa
hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana
mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
18
19. Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio
pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya
uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu
basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
19
20. Na pindi wakikuhoji, basi sema: Mimi nimeusalimisha uso wangu
kumwelekea Mwenyezi Mungu, na kadhaalika walio nifuata. Na waambie walio
pewa Kitabu na wasio na kisomo: Je! Mmesilimu? Wakisilimu basi wameongoka.
Na wakikengeuka basi juu yako ni kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu
ni Mwenye kuwaona waja wake.
20
21. Hakika wanao zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawauwa Manabii
pasipo haki, na wakawauwa watu waamrishao Haki wabashirie adhabu kali.
21
22. Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika duniani na Akhera. Nao
hawatapata wa kuwanusuru.
22
23. Huwaoni wale walio pewa sehemu ya Kitabu? Wanaitwa kukiendea
Kitabu cha Mwenyezi Mungu ili kiwahukumu baina yao; kisha baadhi yao wanageuka
wanakikataa.
23
24. Hayo ni kwa sababu walisema: Hautatugusa Moto isipo kuwa kwa
siku chache tu. Na yakawadanganya katika dini yao yale ambayo wenyewe waliyo
kuwa wakiyazua.
24
25. Basi itakuwaje tutakapo wakusanya Siku ambayo haina shaka kuja
kwake? Na kila nafsi italipwa kama ilivyo chuma, bila ya kudhulumiwa.
25
26. Sema: Ewe Mwenyezi Mungu uliye miliki ufalme wote! Wewe humpa
ufalme umtakaye, na humwondolea ufalme umtakaye, na humtukuza umtakaye,
na humuangusha umtakaye. Kheri yote iko mikononi mwako. Hakika Wewe ni
Muweza wa kila kitu.
26
27. Wewe huingiza usiku katika mchana, na huuingiza mchana katika
usiku. Na humtoa hai kutokana na maiti, na humtoa maiti kutokana na aliye
hai. Na unamruzuku umtakaye bila ya hisabu.
27
28. Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini.
Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ila
ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni
naye. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.
28
29. Sema: Mkificha yaliyomo vifuani mwenu au mkiyafichua Mwenyezi
Mungu anayajua; na anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo duniani. Na Mwenyezi
Mungu ni Muweza wa kila kitu.
29
30. Siku ambayo kila nafsi itakuta mema iliyo yafanya yamehudhurishwa,
na pia ubaya ilio ufanya. Itapenda nafsi lau kungekuwako masafa marefu
baina ya ubaya huo na yeye. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye. Na
Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake.
30
31. Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi,
Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi
Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu.
31
32. Sema: Mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na wakigeuka basi Mwenyezi
Mungu hawapendi makafiri.
32
33. Hakika Mwenyezi Mungu alimteuwa Adam na Nuhu na ukoo wa Ibrahim
na ukoo wa Imran juu ya walimwengu wote.
33
34. Ni wazao wao kwa wao; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na
Mwenye kujua.
34
35. Alipo sema mke wa Imran: Mola wangu Mlezi! Nimekuwekea nadhiri
kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu; basi nikubalie. Hakika Wewe ndiye
Mwenye kusikia na Mwenye kujua.
35
36. Basi alipo mzaa alisema: Mola wangu Mlezi! Nimemzaa mwanamke
- na Mwenyezi Mungu anajua sana aliye mzaa - Na mwanamume si sawa na mwanamke.
Na mimi nimemwita Maryamu. Nami namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde
na Shet'ani aliye laaniwa.
36
37. Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo
mema, na akamfanya Zakariya awe mlezi wake. Kila mara Zakariya alipo ingia
chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata
wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi
Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.
37
38. Pale pale Zakariya akamwomba Mola wake Mlezi, akasema: Mola wangu
Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unaye sikia maombi.
38
39. Alipo kuwa kasimama chumbani akisali, Malaika kamnadia: Hakika
Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya, ataye kuwa mwenye kusadikisha neno
litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni bwana na mt'awa na Nabii kwa watu wema.
39
40. Akasema Zakariya: Mola wangu Mlezi! Vipi nitapata mwana na hali
ukongwe umenifikia, na mke wangu ni tasa? Akasema: Ndivyo vivyo hivyo,
Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo.
40
41. Akasema: Mola wangu Mlezi! Niwekee alama. Akasema: Alama yako
ni kuwa hutasema na watu kwa siku tatu, isipo kuwa kwa kuashiria tu. Na
mdhukuru Mola Mlezi wako kwa wingi na mtakase jioni na asubuhi.
41
42. Na angalia pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Kwa hakika
Mwenyezi Mungu amekuteuwa, na akakutakasa, na akakutukuza kuliko wanawake
wote.
42
43. Ewe Maryamu! Mnyenyekee Mola Mlezi wako na usujudu na uiname
pamoja na wainamao.
43
44. Hizi ni khabari za ghaibu tunazo kufunulia; nawe hukuwa nao walipo
kuwa wakitupa kalamu zao nani wao atamlea Maryamu, na hukuwa nao walipo
kuwa wakishindana.
44
45. Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu
anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa
mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa
walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu).
45
46. Naye atazungumza na watu katika utoto wake na katika utuuzima
wake, na atakuwa katika watu wema.
46
47. Maryamu akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitampata mwana na hali
hajanigusa mwanaadamu? Mwenyezi Mungu akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi
Mungu huumba apendacho. Anapo hukumu jambo, huliambia: Kuwa! Likawa.
47
48. Na atamfunza kuandika na Hikima na Taurati na Injili.
48
49. Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na
Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama
sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti
kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka
akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi
ni wenye kuamini.
49
50. Na ninasadikisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati,
na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale mlio harimishiwa, na nimekujieni
na Ishara kutokana na Mola Mlezi wenu. Kwa hivyo mcheni Mwenyezi Mungu na
nit'iini mimi.
50
51. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi na ni Mola wenu Mlezi.
Basi muabudni Yeye. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.
51
52. Isa alipo hisi kuwa kati yao pana ukafiri alisema: Nani wasaidizi
wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wake wakasema: Sisi ni wasaidizi wa
Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika
ni Waislamu.
52
53. Mola wetu Mlezi! Tumeyaamini uliyo yateremsha, na tumemfuata
huyu Mtume, basi tuandike pamoja na wanao shuhudia.
53
54. Na Makafiri walipanga mipango na Mwenyezi Mungu akapanga mipango,
na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wenye kupanga.
54
55. Pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na
nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka
wale walio kufuata juu ya wale walio kufuru, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha
marejeo yenu yatakuwa kwangu, nikuhukumuni katika yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.
55
56. Ama wale walio kufuru, nitawaadhibu adhabu kali katika dunia
na Akhera, wala hawatapata wa kuwanusuru.
56
57. Na ama wale walio amini na wakatenda mema basi Mwenyezi Mungu
atawalipa ujira wao kaamili. Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhaalimu.
57
58. Haya tunayo kusomea ni katika Aya na Ukumbusho wenye hikima.
58
59. Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam;
alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa.
59
60. Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni
mwa wanao fanya shaka.
60
61. Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikilia ilimu hii waambie:
Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wake zetu na wake zenu, na
sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana
ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.
61
62. Hakika haya ndiyo maelezo ya kweli. Na hakuna mungu ila Mwenyezi
Mungu tu, na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
62
63. Na kama wakigeuka basi Mwenyezi Mungu anawajua waharibifu.
63
64. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina
yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe
na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya
Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni
Waislamu.
64
65. Enyi Watu wa Kitabu! Mbona mnabishana juu ya Ibrahim, na hali
Taurati na Injili hazikuteremshwa ila baada yake? Basi hamzingatii?
65
66. Angalieni! Nyinyi mlibishana katika yale mliyo yajua. Mbona sasa
mnabishana katika yale msiyo yajua? Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye, na
nyinyi hamjui.
66
67. Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu,
wala hakuwa katika washirikina.
67
68. Watu wanao mkaribia zaidi Ibrahim ni wale walio mfuata yeye na
Nabii huyu na walio amini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa Waumini.
68
69. Kipo kikundi katika Watu wa Kitabu wanao penda kukupotezeni;
lakini hawapotezi ila nafsi zao, nao wenyewe hawatambui.
69
70. Enyi Watu wa Kitabu! Mbona mnazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu
ilhali nyinyi mnashuhudia?
70
71. Enyi Watu wa Kitabu! Mbona kweli mnaivisha uwongo, na kweli
mnaificha na hali mnajua?
71
72. Na kikundi katika Watu wa Kitabu walisema: Yaaminini yale waliyo
teremshiwa wenye kuamini mwanzo wa mchana, na yakataeni mwisho wake; huenda
wakarejea.
72
73. Wala msimuamini ila anaye fuata dini yenu. Sema: Hakika uwongofu
ni uwongofu wa Mwenyezi Mungu, kuwa apewe mtu mfano wa mlio pewa nyinyi
au wakuhojini mbele ya Mola wenu Mlezi. Sema: Hakika fadhila zimo mikononi
mwa Mwenyezi Mungu. Humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na
Mjuzi.73
74. Yeye humchagua kumpa rehema zake amtakaye; na Mwenyezi Mungu
ndiye Mwenye fadhila kubwa.
74
75. Na miongoni mwa Watu wa Kitabu yupo ambaye ukimpa amana ya mrundi
wa mali atakurudishia, na miongoni mwao yupo ambaye ukimpa amana ya dinari
moja hakurudishii isipo kuwa ukimsimamia kumdai. Haya ni kwa kuwa wakisema:
Hatuna lawama kwa ajili ya hawa wasio jua kusoma. Na wanamzulia uwongo
Mwenyezi Mungu, hali nao wanajua.
75
76. Sivyo hivyo, bali anaye timiza ahadi yake na akamchamngu basi
Mwenyezi Mungu huwapenda wachamngu.
76
77. Hakika wanao uza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao thamani
ndogo, hao hawatakuwa na sehemu ya kheri yoyote katika Akhera, wala Mwenyezi
Mungu hatasema nao wala hatawatazama Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa,
nao watapata adhabu chungu.
77
78. Na wapo baadhi yao wanao pindua ndimi zao katika kusoma Kitabu
ili mdhanie kuwa hayo yanatoka Kitabuni, na wala hayatoki Kitabuni. Na
husema: Haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu. Na wala hayatoki kwa Mwenyezi
Mungu. Na wanamsingizia Mwenyezi Mungu uwongo na wao wanajua.
78
79. Haiwezi kuwa mtu aliye pewa na Mwenyezi Mungu Kitabu na hikima
na Unabii kisha awaambie watu: Kuweni wa kuniabudu mimi badala ya Mwenyezi
Mungu. Bali atawaambia: Kuweni wenye kumuabudu Mola Mlezi wa viumbe vyote,
kwa kuwa nyinyi mnafundisha Kitabu na kwa kuwa mnakisoma.
79
80.Wala hatakuamrisheni kuwafanya Malaika na Manabii kuwa ni miungu.
Je, atakuamrisheni ukafiri baada ya kuwa nyinyi Waislamu?
80
81. Na pale Mwenyezi Mungu alipo chukua ahadi kwa Manabii: Nikisha
kupeni Kitabu na hikima, kisha akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mliyo
nayo, ni juu yenu mumuamini na mumsaidie. Akasema: Je, mmekiri na mmekubali
kushika agizo langu juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni,
na Mimi ni pamoja nanyi katika kushuhudia.
81
82. Watakao geuka baada ya haya basi hao ndio wapotovu.
82
83. Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila
kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu kwa kumt'ii Yeye kikipenda
kisipende, na kwake Yeye watarejeshwa?
83
84. Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyo teremshiwa sisi,
na aliyo teremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na Yaakub na wajukuu
zao, na aliyo pewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi.
Hatubagui baina yao hata mmoja, na sisi ni wenye kusilimu kwake.
84
85. Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake.
Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.
85
86. Mwenyezi Mungu atawaongoaje watu walio kufuru baada ya kuamini
kwao, na wakashuhudia ya kuwa Mtume huyu ni wa haki, na zikawafikia hoja
zilizo wazi? Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.
86
87. Hao malipo yao ni kuwa ipo juu yao laana ya Mwenyezi Mungu na
ya Malaika na ya watu wote.
87
88. Humo watadumu. Hawatapunguziwa adhabu wala hawatapewa nafasi.
88
89. Isipo kuwa wale walio tubu baada ya hayo na wakatengenea; kwani
Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.
89
90. Hakika wale walio kufuru baada ya kuamini kwao, kisha wakazidi
kukufuru, toba yao haitakubaliwa, na hao ndio walio potea.
90
91. Hakika wale walio kufuru, na wakafa hali ni makafiri haitakubaliwa
kutoka kwa yeyote wao fidia ya dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wangeli
itoa. Hao watapata adhabu chungu, wala hawatakuwa na wa kuwanusuru.
91
92. KABISA HAMTAFIKIA wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda.
Na kitu chochote mnacho kitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua.
92
93. Kila chakula kilikuwa halali kwa Wana wa Israili isipo kuwa alicho
jizuilia Israili mwenyewe kabla haijateremshwa Taurati. Sema: Leteni Taurati
muisome ikiwa nyinyi ni wasema kweli.
93
94. Na wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu baada ya hayo, basi hao
ndio madhaalimu.
94
95. Sema: Mwenyezi Mungu amesema kweli. Basi fuateni mila ya Ibrahim
mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.
95
96. Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko
Bakka, iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote.
96
97. Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim, na
mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu
imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea.
Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu.
97
98. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnakanusha ishara za Mwenyezi
Mungu, na ilhali kuwa Mwenyezi Mungu ni Shahidi kwa yote mnayo yatenda?
98
99. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnamzuilia aliye amini Njia
ya Mwenyezi Mungu mkiitafutia kosa, na hali nyinyi mnashuhudia? Na Mwenyezi
Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yatenda.
99
100. Enyi mlio amini! Mkiwat'ii baadhi ya walio pewa Kitabu watakurudisheni
kuwa makafiri baada ya Imani yenu.
100
101. Na vipi mkufuru hali nyinyi mnasomewa Aya za Mwenyezi Mungu
na Mtume yuko kati yenu? Na mwenye kushikamana na Mwenyezi Mungu basi huyo
ameongozwa kwenye Njia Iliyo Nyooka.
101
102. Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha;
wala msife ila nanyi ni Waislamu.
102
103. Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala
msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile
mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa
neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni
nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate
kuongoka.
103
104. Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha
mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.
104
105. Wala msiwe kama wale walio farikiana na kukhitalifiana baada
ya kuwafikia hoja zilizo wazi. Na hao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa.
105
106. Siku ambayo nyuso zitanawiri na nyuso zitasawijika. Ama hao
ambao nyuso zao zitasawijika wataambiwa: Je! Mlikufuru baada ya kuamini
kwenu? Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mnakufuru.
106
107. Ama wale ambao nyuso zao zitanawiri watakuwa katika rehema ya
Mwenyezi Mungu. Wao humo watadumu.
107
108. Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki. Na Mwenyezi
Mungu hataki kuwadhulumu walimwengu.
108
109. Na kila kilichomo mbinguni na kilichomo ardhini ni cha Mwenyezi
Mungu; na mambo yote yatarejea kwa Mwenyezi Mungu.
109
110. Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha
mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu
wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini,
lakini wengi wao wapotovu.
110
111. Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi
watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa.
111
112. Wamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana, isipo kuwa wakishika
kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu. Na wakastahiki ghadhabu ya Mwenyezi
Mungu, na wamepigwa na unyonge. Hayo ni kwa sababu walikuwa wakizikataa
Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakiwauwa Manabii pasina haki; hayo ni kwa
sababu waliasi na walikuwa wakiruka mipaka.
112
113. Wote hao si sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo watu
walio simama baraabara, wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku,
na pia wanasujudu.
113
114. Wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha
mema na wanakataza maovu na wanakimbilia katika mambo ya kheri. Na hao
ndio miongoni mwa watenda mema.
114
115. Na kheri yoyote wanayo ifanya hawatanyimwa malipwa yake. Na
Mwenyezi Mungu anawajua wachamngu.
115
116. Hakika wale walio kufuru hazitawafaa kitu mali zao wala watoto
wao mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio watu wa Motoni - humo watadumu.
116
117. Mfano wa vile wanavyo vitoa katika uhai wao wa duniani ni kama
upepo ambao ndani yake ipo baridi ya barafu, ukalisibu shamba la watu walio
dhulumu nafsi zao, ukaliteketeza. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali
wao wenyewe wanadhulumu nafsi zao.
117
118. Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika
nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha
fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa
zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.
118
119. Hivyo basi nyinyi ndio mnawapenda watu hao, wala wao hawakupendeni.
Nanyi mnaviamini Vitabu vyote. Na wanapo kutana nanyi husema: Tumeamini.
Na wanapo kuwa peke yao wanakuumieni vidole kwa chuki. Sema: Kufeni kwa
chuki yenu! Hakika Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo vifuani.
119
120. Ikikupateni kheri huwaudhi. Na ikikupateni shari wanafurahia.
Na nyinyi mkisubiri na mkajizuilia, hila zao hazitakudhuruni kitu. Hakika
Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyazunguka yote wayatendayo.
120
121. Na pale ulipo toka asubuhi, ukaacha ahali zako uwapange Waumini
kwenye vituo kwa ajili ya vita - na Mwenyezi Mungu anasikia na anajua.
121
122. Makundi mawili miongoni mwenu yakaingiwa na woga kuwa watashindwa
- na hali Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wao; na Waumini wamtegemee Mwenyezi
Mungu tu.
122
123. Na Mwenyezi Mungu alikwisha kunusuruni katika Badri nanyi mlikuwa
wanyonge. Basi mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kushukuru.
123
124. Ulipo waambia Waumini: Je, haitakutosheni ikiwa Mola wenu atakusaidieni
kwa Malaika elfu tatu walio teremshwa?
124
125. Kwani! Ikiwa mtavumilia na mkamchamngu na hata maadui wakikutokeeni
kwa ghafla, basi hapo Mola wenu Mlezi atakusaidieni kwa Malaika elfu tano
wanao shambulia kwa nguvu.
125
126. Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara kwenu,
na ili nyoyo zenu zipate kutua. Na msaada hautoki isipo kuwa kwa Mwenyezi
Mungu, Aliye tukuka, Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
126
127. Haya ni kwa ajili awakate sehemu katika walio kufuru, au awahizi
wapate kurejea nyuma nao wamepwelewa.
127
128. Wewe huna lako jambo katika haya - ama atawahurumia au atawaadhibu,
kwani wao ni madhaalimu.
128
129. Na ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo
katika ardhi. Yeye humsamehe na humuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu
ni Msamehevu Mwenye kurehemu.
129
130. Enyi mlio amini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu, na mcheni
Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa.
130
131. Na uogopeni Moto ambao umeandaliwa kwa ajili ya makafiri.
131
132. Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa.
132
133. Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo
upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu,
133
134. Ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na
wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda
wafanyao wema;
134
135. Na ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka
Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao - na nani anaye futa
dhambi isipo kuwa Mwenyezi Mungu? - na wala hawaendelei na waliyo yafanya
na hali wanajua.
135
136. Hao malipo yao ni msamaha kwa Mola wao Mlezi, na Bustani zipitazo
mito kati yake. Humo watadumu, na mwema mno ujira wa watendao.
136
137. Kabla yenu zimepita nyendo nyingi; basi tembeeni katika ulimwengu
muangalie vipi ulikuwa mwisho wa wanao kanusha.
137
138. Hii ni bayana kwa watu wote, na ni uwongofu, na mawaidha kwa
wachamngu.
138
139. Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa
ni Waumini.
139
140. Kama yamekupateni majaraha, basi na hao watu wengine yamewapata
majaraha mfano wa haya. Na siku za namna hii tunaweletea watu kwa zamu,
ili Mwenyezi Mungu awapambanue walio amini na awateuwe miongoni mwenu mashahidi.
Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhaalimu;
140
141. Na pia ili Mwenyezi Mungu awasafishe walio amini na awafutilie
mbali makafiri.141
142. Je! Mnadhani mtaingia Peponi na hali Mwenyezi Mungu hajawapambanua
wale miongoni mwenu walio pigana Jihadi, na hajawapambanua walio subiri?
142
143. Na nyinyi mlikuwa mkitamani mauti kabla hamjakutana nayo. Basi
sasa mmekwisha yaona na huku mnayatazama.
143
144. Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake
Mitume. Je, akifa au akauwawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma? Na atakaye geuka
akarudi nyuma huyo hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atawalipa
wanao mshukuru.
144
145. Na haiwezi nafsi kuwa ife ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kama
ilivyo andikwa ajali yake. Na mwenye kutaka malipo ya duniani tutampa;
na mwenye kutaka malipo ya Akhera tutampa. Na tutawalipa wenye kushukuru.
145
146. Na Manabii wangapi walipigana na pamoja nao Waumini wengi wenye
ikhlasi! Hawakufanya woga kwa yaliyo wasibu katika Njia ya Mwenyezi Mungu,
wala hawakudhoofika wala hawakuwa wanyonge. Na Mwenyezi Mungu huwapenda
wanao subiri.
146
147. Wala kauli yao haikuwa ila ni kusema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie
madhambi yetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara
miguu yetu na utunusuru tuwashinde kaumu ya makafiri.
147
148. Basi Mwenyezi Mungu akawapa malipo ya duniani na bora ya malipo
ya Akhera. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao mema.
148
149. Enyi mlio amini! Ikiwa mtawat'ii walio kufuru watakurudisheni
nyuma, na hapo mtageuka kuwa wenye kukhasiri.
149
150. Bali Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wenu, naye ndiye bora wa wasaidizi.
150
151. Tutazitia khofu nyoyo za walio kufuru kwa vile walivyo mshirikisha
Mwenyezi Mungu na washirika ambao hakuwateremshia hoja yoyote. Na makaazi
yao ni Motoni; na maovu yaliyoje maskani ya wenye kudhulumu!
151
152. Na Mwenyezi Mungu alikutimilizieni miadi yake, vile mlivyo kuwa
mnawauwa kwa idhini yake, mpaka mlipo legea na mkazozana juu ya amri, na
mkaasi baada ya Yeye kukuonyesheni mliyo yapenda. Wapo miongoni mwenu wanao
taka dunia, na wapo miongoni mwenu wanao taka Akhera. Kisha akakutengeni
nao (maadui) ili akujaribuni. Naye sasa amekwisha kusameheni. Na Mwenyezi
Mungu ni Mwenye fadhila juu ya Waumini.
152
153. Pale mlipo kuwa mkikimbia mbio wala hamumsikilizi yeyote, na
Mtume anakuiteni, yuko nyuma yenu. Mwenyezi Mungu akakupeni dhiki juu ya
dhiki, ili msisikitike kwa yaliyo kukoseeni wala kwa yaliyo kusibuni. Na
Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda.
153
154. Kisha baada ya dhiki alikuteremshieni utulivu - usingizi ambao
ulifunika kundi moja kati yenu. Na kundi jengine nafsi zao ziliwashughulisha
hata wakamdhania Mwenyezi Mungu dhana isiyo kuwa ya haki, dhana ya kijinga.
Wakisema: Hivyo tuna lolote sisi katika jambo hili? Sema: Mambo yote ni
ya Mwenyezi Mungu. Wanaficha katika nafsi zao wasiyo kubainishia. Wanasema:
Lau ingelikuwa tuna lolote katika jambo hili tusinge uliwa hapa. Sema:
Hata mngeli kuwa majumbani mwenu, basi wangeli toka walio andikiwa kufa,
wakenda mahali pao pa kuangukia wafe.(Haya ni hivyo) ili Mwenyezi Mungu
ayajaribu yaliyomo vifuani mwenu, na asafishe yaliyomo nyoyoni mwenu. Na
Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo vifuani.
154
155. Hakika wale walio rudi nyuma miongoni mwenu siku yalipo pambana
majeshi mawili, Shet'ani ndiye aliye watelezesha kwa sababu ya baadhi ya
makosa waliyo yafanya; na Mwenyezi Mungu amekwisha wasamehe. Hakika Mwenyezi
Mungu ni Mwenye kusamehe, Mpole.
155
156. Enyi mlio amini! Msiwe kama wale walio kufuru na wakawasema
ndugu zao walipo safiri katika nchi au walipo kuwa vitani: Wangeli kuwa
kwetu wasingeli kufa na wasingeli uwawa. Ili Mwenyezi Mungu afanye hayo
kuwa ni majuto katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu huhuisha na hufisha.
Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona myatendayo.
156
157. Na pindi mkiuliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, au mkifa, hakika
maghfira na rehema zitokazo kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko yote wanayo
yakusanya.
157
158. Na mkifa au mkiuliwa ni kwa Mwenyezi Mungu ndio mtakusanywa.
158
159. Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio
umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya
shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana
nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika
Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea.
159
160. Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni
ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee
Mwenyezi Mungu tu.
160
161. Na haiwezekani kwa Nabii yeyote kufanya khiyana. Na atakaye
fanya khiyana, atayaleta Siku ya Kiyama aliyo yafanyia khiyana, kisha kila
mtu atalipwa kwa aliyo yachuma, kwa ukamilifu; wala hawatadhulumiwa.
161
162. Je! Aliye yafuata ya kumridhisha Mwenyezi Mungi ni kama yule
aliye stahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na makaazi yake yakawa Jahannamu?
Napo ni mahala pabaya pa kurejea.
162
163. Hao wana vyeo mbali mbali kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu
ni Mwenye kuyaona yote wayatendayo.
163
164. Hakika Mwenyezi Mungu amewafanyia wema mkubwa Waumini vile alivyo
waletea Mtume aliye miongoni mwao wenyewe, anaye wasomea Aya zake, na anawatakasa,
na anawafunza Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya hapo walikuwa katika
upotovu ulio wazi.
164
165. Nyinyi - ulipo kusibuni msiba ambao nyinyi mmekwisha watia mara
mbili mfano wa huo - mnasema: Umetoka wapi huu? Sema: Huo umetoka kwenu
wenyewe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.
165
166. Na yaliyo kusibuni siku yalipo pambana majeshi mawili yalikuwa
kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ili awajue Waumini.
166
167. Na ili awapambanue walio kuwa wanaafiki, wakaambiwa: Njooni
mpigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu au lindeni. Wakasema: Tungeli jua
kuna kupigana bila ya shaka tungeli kufuateni. Wao siku ile walikuwa karibu
na ukafiri kuliko Imani. Wanasema kwa midomo yao yasiyo kuwamo nyoyoni
mwao. Na Mwenyezi Mungu anajua kabisa wanayo yaficha.
167
168. Hao ndio walio waambia ndugu zao na wao wenyewe wakakaa kitako:
Lau wengeli tut'ii wasingeli uliwa. Sema: Ziondoleeni nafsi zenu mauti
kama mnasema kweli.
168
169. Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi
Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi.
169
170. Wanafurahia aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na wanawashangilia
wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa
khofu juu yao wala hawatahuzunika.
170
171. Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na ya kwamba
Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini.
171
172. Walio mwitikia Mwenyezi Mungu na Mtume baada ya kwisha patwa
na majaraha - kwa walio fanya wema miongoni mwao na wakamchamngu utakuwa
ujira mkubwa.
172
173. Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni!
Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni
mbora wa kutegemewa.
173
174. Basi wakarudi na neema na fadhila za Mwenyezi Mungu. Hapana
baya lilio wagusa, na wakafuata yanayo mridhi Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi
Mungu ni Mwenye fadhila kuu.
174
175. Hakika huyo ni Shet'ani anawatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope,
bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini.
175
176. Wala wasikuhuzunishe wale wanao kimbilia ukafirini. Hakika hao
hawamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anataka asiwawekee sehemu
yoyote katika Akhera, na yao wao adhabu kubwa.
176
177. Hakika wale walio nunua ukafiri kwa Imani hawatamdhuru kitu
Mwenyezi Mungu, na yao wao ni adhabu chungu.
177
178. Wala wasidhani wale wanao kufuru kwamba huu muhula tunao wapa
ni kheri yao. Hakika tunawapa muhula wazidi madhambi. Na yao wao ni adhabu
ya kuwadhalilisha.
178
179. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwaacha Waumini katika hali mliyo
nayo mpaka apambanue wabaya na wema. Wala haiwi kwa Mwenyezi Mungu kukujuulisheni
mambo ya ghaibu. Lakini Mwenyezi Mungu humteua katika Mitume wake amtakaye.
Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume yake. Na mkiamini na mkamchamngu
mtakuwa na ujira mkubwa.
179
180. Wala wasidhani wale ambao wanafanya ubakhili katika aliyo wapa
Mwenyezi Mungu katika fadhila zake kuwa ni kheri yao. Bali hiyo ni shari
kwao. Watafungwa kongwa za yale waliyo yafanyia ubakhili Siku ya Kiyama.
Na urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anazo
khabari za yote myatendayo.
180
181. Mwenyezi Mungu amekwisha sikia kauli ya walio sema: Mwenyezi
Mungu ni masikini, na sisi ni matajiri. Tumeyaandika waliyo yasema, na
pia kuwauwa kwao Manabii bila ya haki, na tutawaambia Siku ya Kiyama: Onjeni
adhabu ya kuungua.
181
182. kuwadhuluHaya ni kwa sababu ya iliyo tanguliza mikono yenu, na kwamba
Mwenyezi Mungu si mwenye mu waja.
182
183. Walio sema: Mwenyezi Mungu ametuahidi tusimuamini Mtume yeyote
mpaka atuletee kafara inayo teketezwa na moto. Waambie: Walikujieni Mitume
kabla yangu kwa hoja zilizo wazi na kwa hayo mnayo sema, basi kwa nini
mkawauwa ikiwa mlikuwa wakweli?.
1
184. Na wakikukanusha basi walikanushwa Mitume wengine kabla yako
walio kuja na hoja waziwazi na Vitabu vyenye hikima, na Kitabu chenye nuru.
184
185. Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu
kaamili Siku ya Kiyama. Na atakaye epushwa na Moto na akatiwa Peponi basi
huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu.
185
186. Hapana shaka yoyote mtapata misukosuko katika mali zenu na nafsi
zenu, na bila ya shaka yoyote mtasikia udhia mwingi kutokana na walio pewa
Kitabu kabla yenu na wale walio shiriki. Na ikiwa mtasubiri na mkamchamngu
basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimia.
186
187. Na pale Mwenyezi Mungu alipo fungamana na walio pewa Kitabu
kuwa: Lazima mtawabainishia watu, wala hamtokificha, walikitupa nyuma ya
migongo yao, na wakanunua kwacho thamani duni. Basi ni kiovu hicho walicho
nunua.
187
188. Usiwadhanie kabisa wale wanao furahia waliyo yafanya, na wakapenda
kusifiwa kwa wasiyo yatenda, usiwadhanie kuwa watasalimika na adhabu. Yao
wao ni adhabu chungu.
188
189. Na Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi
Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.
189
190. Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku
na mchana ziko Ishara kwa wenye akili.
190
191. Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako
na wakilala, na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi!
Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya
Moto.
191
192. Mola wetu Mlezi! Hakika unaye mtia Motoni umemhizi; na walio
dhulumu hawana wasaidizi.
192
193. Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumemsikia mwenye kuita akiitia
Imani kwamba: Muaminini Mola wenu Mlezi; nasi tukaamini. Basi tusamehe
madhambi yetu, na utufutie makosa yetu, na utufishe pamoja na watu wema.
193
194. Mola wetu Mlezi! Na utupe uliyo tuahidi kwa Mitume wako, wala
usituhizi Siku ya Kiyama. Hakika Wewe huvunji miadi.
194
195. Mola Mlezi wao, akayakubali maombi yao akajibu: Hakika sipotezi
kazi ya mfanya kazi miongoni mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke, kwani
ni nyinyi kwa nyinyi. Basi walio hama, na walio tolewa makwao, na wakateswa
katika Njia yangu, na wakapigana, na wakauliwa, kwa yakini Mimi nitawafutia
makosa yao, na kwa yakini nitawaingiza katika Mabustani yanayo pita mito
kati yake. Hayo ndiyo malipo yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi
Mungu kwake yapo malipo mema kabisa.
195
196. Kabisa kusikudanganye kubakia kutangatanga kwa walio kufuru
katika nchi.
196
197. Hiyo ni starehe ndogo. Kisha makaazi yao yatakuwa Jahannamu.
Na ni mahali pabaya mno pa kupumzikia.
197
198. Lakini walio mcha Mola wao Mlezi watapata Mabustani yanayo pita
mito kati yake. Watadumu humo. Hayo ni makaribisho yao yatokayo kwa Mwenyezi
Mungu. Na vilioko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kwa watu wema.
198
199. Hakika miongoni mwa Watu wa Kitabu wapo wanao muamini Mwenyezi
Mungu na yaliyo teremshwa kwenu na yaliyo teremshwa kwao, wakimnyenyekea
Mwenyezi Mungu. Hawabadili Aya za Mwenyezi Mungu kwa thamani duni. Hao
wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa
kuhisabu.
199
200. Enyi mlio amini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni
macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa.
200
Sura Nyingine | Faharasa |