| 37.Suurat Ass 'Affat |
| Imeshuka Makka | Ina aya 182 |
| Utangulizi | Sura Nyingine | Faharasa |

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0

1. Naapa kwa wanao jipanga kwa safu.
1

2. Na kwa wenye kukataza mabaya.
2

3. Na kwa wenye kusoma Ukumbusho.
3

4. Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.
4

5. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola
Mlezi wa mashariki zote.
5

6. Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota.
6

7. Na kulinda na kila shet'ani a'si.
7

8. Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila
upande.
8

9. Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu.
9

10. Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo
kinacho ng'ara.
10

11. Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine
tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata.
11

12. Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara.
12

13. Na wanapo kumbushwa hawakumbuki.
13

14. Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara.
14

15. Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri.
15

16. Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?
16

17. Hata baba zetu wa zamani?
17

18. Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili.
18

19. Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona!
19

20. Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo.
20

21. Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha.
21

22. Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu.
22

23. Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu!
23

24. Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa:
24

25. Mna nini? Mbona hamsaidiani?
25

26. Bali hii leo, watasalimu amri.
26

27. Watakabiliana wao kwa wao kuulizana.
27

28. Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia.
28

29. Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini.
29

30. Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa
wapotovu.
30

31. Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika
bila ya shaka tutaonja tu adhabu.
31

32. Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.
32

33. Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja.
33

34. Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu.
34

35. Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu
ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna.
35

36. Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu
mtunga mashairi mwendawazimu?
36

37. Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume.
37

38. Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.
38

39. Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya.
39

40. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa.
40

41. Hao ndio watakao pata riziki maalumu,
41

42. Matunda, nao watahishimiwa.
42

43. Katika Bustani za neema.
43

44. Wako juu ya viti wamekabiliana.
44

45. Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem.
45

46. Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao.
46

47. Hakina madhara, wala hakiwaleweshi.
47

48. Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri.
48

49. Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika.
49

50. Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe.
50

51. Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki.
51

52. Aliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanao sadiki.
52

53. Ati tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndio tutalipwa na kuhisabiwa?
53

54. Atasema: Je! Nyie mnawaona?
54

55. Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu.
55

56. Atasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza.
56

57. Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila ya shaka ningeli
kuwa miongoni mwa walio hudhurishwa.
57

58. Je! Sisi hatutakufa,
58

59. Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa.
59

60. Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa.
60

61. Kwa mfano wa haya nawatende watendao.
61

62. Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum?
62

63. Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu.
63

64. Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu.
64

65. Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani.
65

66. Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo.
66

67. Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka.
67

68. Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu.
68

69. Hakika waliwakuta baba zao wamepotea.
69

70. Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao.
70

71. Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao.
71

72. Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji.
72

73. Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji.
73

74. Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji.
74

75. Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji.
75

76. Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa.
76

77. Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia.
77

78. Na tukamwachia (sifa njema) kwa walio kuja baadaye.
78

79. Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote!
79

80. Kwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema.
80

81. Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
81

82. Kisha tukawazamisha wale wengine.
82

83. Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake,
83

84. Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima.
84

85. Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?
85

86. Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu?
86

87. Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote?
87

88. Kisha akapiga jicho kutazama nyota.
88

89. Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa!
89

90. Nao wakamwacha, wakampa kisogo.
90

91. Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli?
91

92. Mna nini hata hamsemi?
92

93. Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia.
93

94. Basi wakamjia upesi upesi.
94

95. Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe
95

96. ?Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo
vifanya!
96

97. Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo!
97

98. Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio
wa chini.
98

99. Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi;
Yeye ataniongoa.
99

100. Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema.
100

101. Basi tukambashiria mwana aliye mpole.
101

102. Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia:
Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia
wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta
mimi, Inshallah, katika wanao subiri.
102

103. Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji.
103

104. Tulimwita: Ewe Ibrahim!
104

105. Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa
wanao tenda mema.
105

106. Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri.
106

107. Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu.
107

108. Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye.
108

109. Iwe salama kwa Ibrahim!
109

110. Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema.
10

111. Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
11

112. Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa
watu wema.
112

113. Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao
walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi.
113

114. Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni.
114

115. Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa.
115

116. Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda.
116

117. Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha.
117

118. Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka.
118

119. Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka.
119

120. Iwe salama kwa Musa na Haruni!
120

121. Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.
121

122. Hakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini.
122

123. Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume.
123

124. Alipo waambia watu wake: Hamwogopi?
124

125. Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji,
125

126. Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa
zamani?
126

127. Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa;
127

128. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.
128

129. Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye.
129

130. Iwe salama kwa Ilyas.
130

131. Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.
131

132. Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
132

133. Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume.
133

134. Tulipo mwokoa yeye na ahali zake wote,
134

135. Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma.
135

136. Kisha tukawaangamiza wale wengineo.
136

137. Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi,
137

138. Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini?
138

139. Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.
139

140. Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni.
140

141. Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa.
141

142. Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.
142

143. Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu,
143

144. Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa.
144

145. Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa.
145

146. Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye.
146

147. Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi.
147

148. Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.
148

149. Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike,
na wao wanao watoto wa kiume?
149

150. Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?
150

151. Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema:
151

152. Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!
152

153. Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume?
153

154. Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?
154

155. Hamkumbuki?
155

156. Au mnayo hoja iliyo wazi?
156

157. Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli.
157

158. Na wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini
wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa.
158

159. Subhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia.
159

160. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.
160

161. Basi hakika nyinyi na mnao waabudu
161

162. Hamwezi kuwapoteza.
162

163. Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni.
163

164. Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu.
164

165. Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu.
165

166. Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa.
166

167. Na walikuwapo walio kuwa wakisema:
167

168. Tungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani,
168

169. Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi.
169

170. Lakini waliukataa. Basi watakuja jua.
170

171. Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu
walio tumwa.
171

172. Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa.
172

173. Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda.
173

174. Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda.
174

175. Na watazame, nao wataona.
175

176. Je! Wanaihimiza adhabu yetu?
176

177. Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa
walio onywa.
177

178. Na waache kwa muda.
178

179. Na tazama, na wao wataona.
179

180. Subhana Rabbi'l'Izzat Ametakasika Mola Mlezi Mwenye enzi na
yale wanayo mzulia.
180

181. Na Salamu juu ya Mitume.
181

182. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu
wote.
182
| Sura Nyingine | Faharasa |