62.Suuratul Al Jumua' |
Imeshuka Madina | Ina aya 11 |
Utangulizi | orodha ya Sura | Faharasa |
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0
1. Viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi vinamtakasa Mwenyezi
Mungu, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
1
2. Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee
Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya
haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.
2
3. Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao. Na Yeye ndiye Mwenye
nguvu, Mwenye hikima.
3
4. Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu anayo mpa amtakaye. Na Mwenyezi
Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.
4
5. Mfano wa walio bebeshwa Taurati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda
anaye beba vitabu vikubwa vikubwa. Mfano muovu mno wa watu walio kadhibisha
Ishara za Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.
5
6. Sema: Enyi mlio Mayahudi! Ikiwa nyinyi mnadai kuwa ni vipenzi
vya Mwenyezi Mungu pasipo kuwa watu wengine, basi yatamanini mauti, ikiwa
mnasema kweli.
6
7. Wala hawatayatamani kabisa, kwa sababu ya iliyo kwisha yatanguliza
mikono yao. Na Mwenyezi Mungu anawajua walio dhulumu.
7
8. Sema: Hayo mauti mnayo yakimbia, bila ya shaka yatakukuteni. Kisha
mtarudishwa kwa Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Hapo
atakwambieni mliyo kuwa mkiyatenda.
8
9. Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi
kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu,
lau kama mnajua.
9
10. Na itakapo kwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila
za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa.
10
11. Na wanapo iona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha
umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara.
Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki.
11
Sura Nyingine | Faharasa |