66.Suuratul Attah'riim |
Imeshuka Madina | Ina aya 12 |
Utangulizi | Orodha ya Sura | Faharasa |
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0
1. Ewe Nabii! Kwa nini unaharimisha alicho kuhalilishia Mwenyezi
Mungu? Unatafuta kuwaridhi wake zako. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe,
Mwenye kurehemu.
1
2. Hakika Mwenyezi Mungu kakupeni Sharia ya kufungua viapo vyenu,
na Mwenyezi Mungu ni Mola wenu. Na Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.
2
3. Na Nabii alipo mwambia mmoja wa wake zake jambo la siri. Basi
alipo litangaza yule mke, na Mwenyezi Mungu akamdhihirishia Mtume, alimjuvya
sehemu na akaacha sehemu nyengine. Alipo mwambia hayo, huyo mke akasema:
Nani aliye kwambia haya? Mtume akasema: Kaniambia Mjuzi Mwenye khabari
zote!
3
4. Kama nyinyi wawili hamkutubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu
zimekwisha elekea huko. Na mkisaidiana dhidi yake (Mtume), basi hakika
Mwenyezi Mungu ndiye kipenzi chake, na Jibrili, na Waumini wema, na zaidi
ya hayo Malaika pia watasaidia.
4
5. Asaa Mola wake Mlezi, akikupeni talaka, akampa wake wengine badala
yenu nyinyi, walio bora kuliko nyinyi, wanynyekevu, Waumini, wat'awa, walio
tubu, wenye kushika ibada, wafanyao kheri, wajane na wanawari.
5
6. Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao
kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi
Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa.
6
7. Enyi mlio kufuru! Msilete udhuru leo. Hakika mnalipwa mliyo kuwa
mkiyatenda.
7
8. Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli!
Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu na akakuingizeni katika Pepo
zipitazo mito kati yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii
na walio amini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao na pande zao za
kulia, na huku wanasema: Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie!
Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.
8
9. Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanaafiki, na kuwa mgumu kwao!
Na makaazi yao ni Jahannamu. Na hayo ni marejeo mabaya.
9
10. Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio kufuru: mke wa Nuhu na
mke wa Lut'i. Walikuwa chini ya waja wetu wema wawili miongoni mwa waja
wetu. Lakini wakawakhuni waume zao, nao wasiwafae kitu. Na ikasemwa: Ingieni
Motoni pamoja na wanao ingia!
10
11. Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio amini - mkewe Firauni,
alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe
na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhaalimu.
11
12. Na Mariamu binti wa Imrani, aliye linda ubikira wake, na tukampulizia
humo kutoka roho yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu
vyake, na alikuwa miongoni mwa wat'iifu.
12
Sura Nyingine | Faharasa |