Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
86.Surat AtT'aariq

Imeshuka Makka Ina aya 17
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa


KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0



1. Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku! 1



2. Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku? 2



3. Ni Nyota yenye mwanga mkali. 3



4. Hapana nafsi ila inayo mwangalizi. 4



5. Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani? 5



6. Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa, 6



7. Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu. 7



8. Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha. 8



9. Siku zitakapo dhihirishwa siri. 9



10. Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi. 10



11. Naapa kwa mbingu yenye marejeo! 11



12 Na kwa ardhi inayo pasuka! 12



13. Hakika hii ni kauli ya kupambanua. 13



14. Wala si mzaha. 14



15. Hakika wao wanapanga mpango. 15



16. Na Mimi napanga mpango. 16



17. Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole. 17


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani