Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul A'adiyat

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Ninaapa kwa farasi wa Jihadi wendao mbio, na huku pumzi zao zinasikilizana kwa sauti inayo itwa "Dh'abh'an".
Rudi kwenye sura

* 2. Na kwa farasi hao ambao hutoa cheche za moto zinapo gonga kwato zao kwenye ardhi wanapo kwenda.
Rudi kwenye sura

* 3. Na kwa farasi hao wanao washambulia maadui asubuhi kabla jua halijachomoza;
Rudi kwenye sura

* 4. Wakatimua mavumbia mengi, farasi hao, kati ya makundi ya maadui!
Rudi kwenye sura

* 5. Ikawa vumbi limewagubika maadui hata wakaingiwa kiwewe na kufazaika.
Rudi kwenye sura

* 6. Hakika mwanaadamu ni mwingi wa kuzikufuru neema za Mola wake Mlezi ambazo hazikadiriki.
Rudi kwenye sura

* 7. Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka atakuwa mwingi wa kuja jishuhudia huko Akhera kwa kuungama madhambi yake.
Rudi kwenye sura

* 8. Na hakika yeye kwa uchoyo na kuyapenda mali alio nayo, ni bakhili, hatoi kama inavyo mwajibikia katika mali yake.
Rudi kwenye sura

* 9,10. Kwani hajui mwisho wa hali yake, hata hajui wakitolewa maiti waliomo makaburini, na vikakusanywa viliomo vifuani navyo vimekwisha sajiliwa katika madaftari yao, yakiwa mema au mabaya waliyo yatenda?
Rudi kwenye sura

* 9,10. Kwani hajui mwisho wa hali yake, hata hajui wakitolewa maiti waliomo makaburini, na vikakusanywa viliomo vifuani navyo vimekwisha sajiliwa katika madaftari yao, yakiwa mema au mabaya waliyo yatenda?
Rudi kwenye sura

* 11. Kwamba hakika Mlezi wao na Muumba wao bila ya shaka anajua vyema vitendo vyao na malipo yao Siku ya Kufufuliwa na Kulipwa.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani